CLASICO SINZA DERBY...
Game: Abajalo Vs Sinza Stars
Stadium: Estadio Kinesi Urafiki
Date: 11/9/2021
Ni mchezo wa ufunguzi Ligi daraja la 3 kati ya Mwamba wa Soka Sinza na Dar es salaam kwa Ujumla klabu ya Abajalo yenye kumiliki mataji mengi zaidi mchangani dhidi ya majirani zao Sinza Stars ambao hawana historia ya kuifunga Abajalo Mnyama Mkubwa.
Rekodi zinaonesha katika Mchezo mmoja wa kuaga Mwaka kati ya mahasimu hao wawili, Sinza Stars walifungwa, kisha Van Dame akawachapa na mwisho wa yote Abajalo waling’oa magoli ya uwanja wa Sinza Stars na kwenda kuyasimika katika uwanja wao wa Nyumbani wa Estadio de Mashujaa...