HISTORIA YAKUSISIMUA YA MJI WA ROMA NA (Derby Della Capitale)
#LAZIO; hii ni kanda nyingine kati ya zile 20 inayopatikana ndani ya nchi ya Italia ni yapili kwa wingi wawatu baada ya Lombardy, ndani ya Lazio kuna miji mikubwa minne ambayo ni Frosinone,Latina,Rieti na Rome apa zaidi ntaiongelea Rome ambako tunaikuta ile derby yetu bora kabisa kati ya Lazio Vs As Roma!
??#Rome.. Huu ndio mji mku nchi Italia na unaongoza kwa kuingiza mapato mengi ndani ya nchi hio ngoja nikupe story kidogo ya historia ya huu mji ili twende pamoja...
Kama unavyoona hio nembo ya mbwa mwitu wakike akiwanyonyesha watoto wawili hapo hio ndio nembo ya mji wa Rome pia ni nembo ya timu ya As Roma wakienzi watoto mapacha Romulus na nduguye Remus je ni kina nan hawa watu?
⚫Romulus na Remus hawa ni watoto walioziliwa Alba Longa kwenye mji wa Ancient Latin na mama ya akiwa ni Rhea Silvia ambae alikua mtoto wa mfalme Numitor, baada yakuzaliwa mapacha hao kaka wa mwanamama huyo ambae ndio alikua mfalme kwa nyakati hizo Amulius alitoa agizo watoto hao wauliwe...
Kama unavyojua zamani walikua na tabia yakutelekeza watoto msituni au mtoni basi watoto hawa walienda telekezwa katika mto “Tiber" ila waliweza kubaki Salama wenye wanasema walisaidiwa na Miungu ya MTO huo kwajina la “God Tiberinus" km ushawahi tizama season moja inaitwa VIKING utajionea haya mambo, watoto hao walikuja kusaidiwa na kunyonyeshwa na mbwa mwitu “She Wolf"!!
✔Inasemekana hawa ndugu wawili ndio walifanya kazi kubwa ya kuutengeneza mji wa Rome mpk Leo hii moja ya miji tajiri dunia na hiyo ni historia ya kweli iliopo kwenye vitabu vya mbalimbali ukifatilia utapata, turudi kwenye Derby ya mjii huo wa Rome
Fransisco Totti ndie kinara aliecheza michezo mingi kwenye Derby hio akicheza Mara(44) pia ndie kinara wa magoli akifungana na Dino Costa wote wanamagoli(11) na Vincenzo Montella ndie aliwahi kuweka rekodi yakufunga magoli mengi kwenye mchezo mmoja katika derby hio akifunga magoli(4) kwenye ushindi Roma 5:1 dhidi ya Lazio,
As Roma anamakombe ya ligi kuu sirieA(3),Copa Italia (9),Super Copa Italia (3)
Lazio anamakombe ya ligi kuu sirieA (4),Copa Italia (7) super Copa Italia (4) na UEFA cup winner(1) na UEFA super cup(1).
Na hawa majamaa wanatumia uwanja mmoja na uwanja huo ni wamaspaa ya mji wa Rome pia ndio uwanja wa taifa nchini italia wengi tunaujua ni Stadio Olimpico hawa ni km simba na yanga tu!