Fahamu aina 14 za hasira walizonazo wanawake

Nilikuwa na demu Ana hasira kichizi, anatembea na kiwembe, akikasirika mashuka, magodoro na nguo zako nzuri ndio umevikosa hivyo
 
H
.

Kikawaida kila binadamu aliekamilika kaumbiwa hasira,hasira ambazo zipo Kwa maana na kazi maalumu kuliko vile ambavyo wengi hudhania kua hasira zipo Kwa ajili ya kuleta matatizo laa hasha..!!
Hasira ndizo zinatufanya tupambanie haki zetu has a pale tunapodhulumiwa,hasira ndizo zinatuondelea unyonge na kuonekana watu Wa kukubali kushindwa..ila jambo LA muhimu LA kisisitiziwa ni kutozidisha kiwango.
Zifuatazo ni Baadhi ya hasira za wanawake....


1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao!

7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote!

8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka wanaharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia kwenye maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa…. Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

Haya wanajamvi kazi kwenu wewe mwanamke uliopo humu hasira yako ipo namba ipi?? Na wewe mwanaume mwenza wako anaangukia kwenye namba ipi??
 
Dah wakwangu ananuna hata wiki
 
Wa kwangu anatoka nje ya ndoa
 
Hasira za kwenye mahaba siyo? Au hata kazini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…