Hivi ni kweli kuna bearings feki na original? Ntajuaje sasa,na bei zake zikoje mfano za swift.
Ndio kuna bearing origino na fake
jinsi ya kujua kama bearing ni fake,
cha kwanza, tambua hio bearing inatoka nchi gani, Country of origin. kama kwenye package ya bearing hakuna label iliyoandikwa imetoka nchi gani, basi tambua hio bearing ni fake.
Pili, bearing zina part number, kiwanda chochote kinachotengeneza bearing kuna part number wanaziweka kwa ajili ya kutambua ubora wa bidhaa yao. ukiona bearing haina namba hio ni fake.
tatu, nunua bearing kwa supplier ambaye ana distributorship certificate au kwa maneno mengine nunua bearing kwa authorised dealer.
pamoja na hayo maelezo lakini bado imekuwa changamoto kubwa kuziondoa hizo fake bearing sokoni, na hii ni kwasababu wabongo wenyewe tunapenda kupata vitu kwa bei rahisi, na hii inasababisha wafanyabiashara watafute bearing za bei chini ili waweze kuuza na kupata faida hawaangalii bearing zinatoka wapi.
hizo bearing za swift nipe namba zake