Swahili AI
JF-Expert Member
- Mar 2, 2016
- 10,174
- 89,364
Katika maisha yetu ya leo, kwa namna moja au nyingine tunatumia Artificial Intelligence- intellijensia ya kutengenezwa(Sijapata Kiswahili Fasaha, wana jamvi waweza saidia) kupitia vifaa vya kieletroniki kama simu, computer, luninga n.k.
Artificial Intelligence (AI) ni nini?
Mwaka 1956, mwana sayansi John McCarty akiwa kwenye mkutano wa Dartmouth alifafanua AI kama sayansi ya kutengeneza mashine ili kufanya kazi na kutenda/kuenenda kama binadamu.
Lakini AI imekua na uhusiano wa moja kwa moja na masiha yetu ya kila siku kupitia vifaa vya kielektroniki tunavyojihusisha navyo katika masiha yetu ya kila siku.
Kwa namna gani?
Unaweza ukawa unajiuliza hivyo, Je ushawahi jiuliza kwanini search engines kama GOOGLE inaweza kukupa matokeo sahihi ya kile unachokiuliza au kukitafuta kupitia mtandao wao?
Zile post feed za instagram au facebook unazopenda kuziangalia ndizo watakazokuletea kwenye search page yako?
Zile suggestions(mapendekezo ya marafiki au matangazo au watu wakuwafuata(follow) mitandao ya kijamii inayokuletea inatokana na nini?
Mfano SIRI na Google Assistant zinavyokuletea matokeo kwa kile unachokihitaji?
Ni kwamba AI ime-base sana kukusanya data katika masiha yetu ya kila siku, hivyo katika ukusanyaji wa data kutoka kwa binadamu ndivyo hivyo mashine hizo zinachakata data hizo na kuzihifadhi kwa matumizi ya baadae kwa watumiaji wa vifaa ivyo pamoja na huduma toka kwenye kifaa husika.
Aina za AIs - Zipo 3.
1. Artificial Narrow intelligence
Aina hii inahusika sana na intelijensia kwa kazi kwa lengo fulani tu, pia hufaamika kama intelijensia dhaifu. Mfano mzuri ni Alexa ambapo.
ina uwezo wa kutambua mwingiliano wa sauti, uchezaji wa muziki, kutengeneza orodha za kufanya, kuweka kengele, utiririshaji wa podcast, kucheza vitabu vya sauti, na kutoa hali ya hewa, trafiki, michezo, na habari zingine za wakati halisi, kama habari. Alexa inaweza pia kudhibiti vifaa kadhaa mahiri ikitumia yenyewe kama mfumo wa kiotomatiki wa nyumbani.
Mfano mwingine ni FACE ID kwenye simu janja, Kuendesha magari/ndege bila dereva.
2. Artificial General Intelligence
Hii ni intelijensia yenye nguvu sana ambapo inahusisha uwezo wa kufanya kazi nyingi za kutumia akili ambazo mwanadamu wa kawaida anaweza kuzifanya.
Mashine zinazotumia aina hii ya AI zina uwezo wa kufanya kazi za kibinadamu na kutumia kaili bila kuwa na uwezo kufikiri kama binadamu. Kwa mfano michezo kama karata, Draughts( maarufu kama drafti) kwenye kompyuta au simu zetu
3. Artificial Super Intelligence.
Aina hii sasa ina uwezo wa kufanya kazi kwa kiwango cha juu sana kupita uwezo wa kibinadamu. Mchawi wa teknolojia, Elon Musk anaamini kwamba ifikapo mwaka 2040 ASI ita-take over dunia nzima.
Itaendelea....