Mungu anachukia dhambi, hachukii wadhambi "usihukumu usije ukahukumiwa" inamaanisha tuchukie dhambi, tusichukie watenda dhambi sababu kesho wanaweza kubadilika. Ukimuua mtenda dhambi kwa kumhukumu haitakuepo tena nafasi yake kubadilika.
Mtenda dhambi anaweza kuokolewa au kupata uponyaji. Tuchukie matendo na sio watu wanaotenda maovu kwa sababu vita vyetu si juu ya damu na nyama bali juu ya roho inayoleta uharibifu.
USHUHUDA; Benjamin alifwatwa na mtumishi wa Mungu kanisani na kumwambia "Unaroho ya ushoga ndani yako" aliguswa na mtumishi wa Mungu na alidondoka chini na baada ya muda mfupi Mungu alimweka huru
Baada ya wiki moja alifika kanisani kushuhudia ukuu wa Mungu kwa jinsi alivyo sikia mabadiliko kwenye fikra na mwili wake.
Benjamin alikua akifanya kazi na wenzake maeneo ya kijijini kipindi akiwa na miaka 16 na siku moja usiku mfanyakazi mwenzake alitumia nguvu kama kutaka kumlawiti. Wakati akipambana kijinusuru aliwekewa kitu usoni ambacho kilimfanya kupoteza fahamu. Alsubuhi ndipo aligundua kilicho tokea baada ya kujikuta hana suruali na imetupwa chini. "Tangu hapo roho chafu iliingia ndani yangu, nilipoteza affection kwa manawake na nilianza kuvutiwa na wanaume wenzangu." Alijitahidi kwa akili na uwezo wake kupingana na hali hiyo lakini ilishindika, anasema hii hali ilikua nje ya uwezo wake
USHAURI WA BENJAMIN "Yeyote anae pitia tatizo kama langu asijisumbue wenyewe, ukiwa na tatizo la kiroho unahitaji suluhisho la kiroho ili kuwa huru kabisa."
USHUHUDA WA PILI
Chika anashuhudia, alibakwa akiwa na miaka 12. Kitendo hicho kilimfanya awachukie sana wanaume.
Baadae alianza kuota ndoto akifanya mapenzi na wanawake wenzake na baada ya kujiunga sekondari alikuwa akitongoza wanafunzi wenzake na kushiri nao mapenzi.
Aliamua kutafuta wachungaji na watumishi baada ya kujitathmini na kugundua kwamba hayo sio aina ya maisha anayo tamani kuishi. wengi walimuombea lakini halikua jambo rahisi. Hakupata uponyaji..wakati mwingine baada ya maombi hayo hali yake ilibadilika na kuwa mbaya zaidi kuliko mwanzo
Baadae ilikutana na mtumishi mmoja ambaye baada ya kumuona tu alimpa unabii wa shida yake na alipo mwombea alipata uponyaji wapapo kwa hapo. Hisia za kuvutiwa kimapenzi kwa wanawake wenzake zilikoma palepale.
USHAURI WAKE: Vijana wenzangu wazingatie haya "Kama utajikuta kwenye hali kama yangu usiogope, Yesu Kristo pekee ndiye anaweza kukuponya na kukutoa katika hali hiyo". Alishauri pia wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuwafundisha jinsi ya kuepukana na mambo kama hayo tangu wakiwa wadogo.
USHUHUDA WA TATU:
Baada ya mapepo kulipuka kijana miaka 19 anasimulia " Nilikutana na rafiki wa rafiki yangu wa karibu, hakuwa mwanafunzi kama mimi. Kipindi cha likizo alilazimisha sana twende kwake tukamtembelee na kutoka out" tulizoeana sana na alikua akitupa fedha, siku moja kipindi cha likizo nikiwa nyumbani kwake alinisogelea karibu na bila kutarajia kwa ghafla alinibusu shavuni. Huo ndio ulikua mwanzo wa tatizo langu
Nilianza kuwa na affection ya kuwaingilia wanaume wenzangu na hiyo roho ilinipa nguvu ya kugundua mtu anaye jihushisha na ushoga kwa kumtazama tu na sikusita kumfwata moja kwa moja.
Yule rafiki aliniingiza kwenye genge moja la kishirikina, nilipewa assignment ya kueneza hiyo spirit, na kabla ya ku-release aina flani ya miziki au pornography hunenewa maneno ya kipepo na mtu akitazama au kuskiliza ghafla anaanza kupata hisia tofauti na bila kujua tabia ziaanza kubadilika taratibu."
Nilianza kuwa mkorofi shuleni, natoroka na kwenda nightclubs, ufaulu wangu ulishuka na niliamua kuacha shule...
Mama yangu hapa ni shahidi kwamba nikisikia nyumbani wanataka kusali nakimbilia chumbani kwangu na kujifungia. Nilichukia sana kusali. Tabia zangu zilibadilika hadi wazazi kulaani matendo yangu lakini sikujali.
Baada ya uponyaji na kufunguliwa, sasa niko huru na hisia zangu kwa wanawake zimerudi. Hisia kwa wanaume wenzangu hazipo tena.
Namshukuru sana Bwana Yesu kwa kuniweka huru. Amen
Ndugu uliesoma ujumbe huu, niliguswa kutoa ajumbe huu sababu tatizo limekua kubwa na kufwatia mkumbo unaweza kuingia huko bila kujua. Sasa kwa kiasi flani unaweza kujiepusha, kuepusha wengine na hata kuwasaidia wale ambao wako kwenye tatizo kuutafuta mkono wa Mungu ili wawe huru.
Biblia inasema na ndivyo ilivyo kwamba "hakuna lisilo wezekana kwa Mungu" hata mtu awe ameathiriwa vipi!, Kukata tamaa ni dhambi kubwa zaidi. Iambie nafsi yako, mimi nitabadilika na kurudiwa na hisia alizonipa Mungu tangu mwanzo.
Wewe mwenyewe kila ukiskia hali hiyo ikatae ndani yako, ipinge kwa vitendo na tafuta watu unao waamini wakusaidie kiroho. Jishughulishe na mambo yako na kwenye nafsi yako teta na Mungu kimya kimya, mwambie Mungu sipendi hii dhambi, najua wewe unaweza yote, nikutanishe na mtumishi wako uliye mkusudia wewe mwenyewe afanyike njia ya kunikomboa kwenye usagaji, ushoga n.k
Ukiguswa pia kunishirikisha tatizo lako au la ndugu yako, rafiki usisite kunitafuta. Usiogope, nitumie ujumbe nami nitakuelekeza chakufanya na tatizo lako litaisha. Tatizo hilo ni roho tu imewekwa ndani yako, wewe sio tatizo wala wewe pekeyako huwezi kujikomboa.
Yesu tu anaweza kukuweka huru leo. Wengi pia wameamua kubaki na matatizo yao sababu hata wale wanao waamini hawana vifua vya kuwatunzia siri!!! Nafahamu hilo na ni kweli. Hutakiwi kumshirikisha kila mtu tatizo lako. Watu wengine wanaweza kukuathiri zaidi badala ya kusaidi
Mungu awabariki sana