Fahamu faida 10 za kupumzika baada ya uchovu wa kazi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, watu wengi hawapati muda wa kutosha wa kupumzika. Mara nyingi mtu anapozidiwa hupunguza zaidi muda wa kupumzika ili akamilishe majukumu yake. Ikiwa unataka kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida 10 za kupumzika.

1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu
Ubongo wa mwanadamu unahitaji kupumzika ili uweze kujijenga na kufanya kazi vyema. Ikiwa mtu hatapata muda wa kutosha wa kupumzika, uwezo wake wa kutunza kumbukumbu utapungua.

2. Huondoa hatari ya kupata kiharusi
Kiharusi ni ugonjwa unaosababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo ya damu kwenye ubongo; hili husababisha damu kuvuja ndani ya ubongo.

3. Hulinda afya ya moyo
Kupumzika kuna manufaa makubwa kwenye afya ya moyo wako. Ni wazi kuwa kasi ya usukumaji wa damu wakati wa kufanya shughuli mbalimbali ni tofauti na wakati unapokuwa umepumzika.

4. Hutoa muda wa mwili kujijenga
Miili yetu inahitaji kujijenga kila mara hasa baada ya shughuli nyingi. Kwa njia ya kupumzika utaweza kuupa mwili wako nafasi nzuri ya kujijenga na kurejeshha tena nguvu iliyotumika wakati wa shughuli mbalimbali.

5. Huongeza hamasa ya utendaji
Nani anapenda kufanya kazi akiwa amechoka? Naamini hakuna. Kupata muda wa kutosha wa kupumzika kutakuwezesha kujisikia vizuri na kuwa tayari kutekeleza majukumu yaliyoko mbele yako.

6. Huimarisha misuli
Tunapopumzika misuli yetu inajijenga na kurudisha ute wake uliopotea wakati wa shughuli mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kila baada ya kazi tunapata muda wa kutosha wa kupumzika ili tuboreshe afya za miili yetu.

7. Huimarisha kinga mwili
Kinga mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga mwili kujijenga na kujiimarisha.

8. Huondoa msongo wa mawazo
Chanzo kimojawapo cha msongo wa mawazo ni uchovu, na chanzo kimojawapo cha maradhi mbalimbali ni msongo wa mawazo.

9. Hutuwezesha kula vizuri
Ni ukweli usiopingika kuwa tukiwa tumechoka hatuwezi kula vizuri. Hivyo kupata muda mzuri na wakutosha wa kupumzika kutakuwezesha kula chakula vyema.

10. Huepusha ajali za barabarani
Je, ulishasikia ajali zilizosababishwa na madereva wanaosinzia? Uchoovu na kukosa muda wa kupumzika (hasa kulala) humfanya mtu akose utulivu na uwezo wa kumudu chombo anachoedesha.
 
Hustawisha ndoa
 
Pendael24 best pita hapa
Asante sana mpendwa, niaze mazoezi kwa kweli, muda wangu wa kumpumzika ni mdogo sana yaani.
Wanashauri wataamu wa afya walao tulale kwa muda wa saa 8 kwa siku, lakini kwangu kidogo hio haipo nikizidi sana kwa siku na lala kwa saa 3 mpaka 4.
Asante pia mleta mada, barikiwa sana.
 
Anza kufanya hivo kwa ajili ya afya yako mkuu!
 
Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, watu wengi hawapati muda wa kutosha wa kupumzika. Mara nyingi mtu anapozidiwa hupunguza zaidi muda wa kupumzika ili akamilishe majukumu yake. Ikiwa unataka kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida 10 za kupumzika.

1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu
Ubongo wa mwanadamu unahitaji kupumzika ili uweze kujijenga na kufanya kazi vyema. Ikiwa mtu hatapata muda wa kutosha wa kupumzika, uwezo wake wa kutunza kumbukumbu utapungua.

2. Huondoa hatari ya kupata kiharusi
Kiharusi ni ugonjwa unaosababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo ya damu kwenye ubongo; hili husababisha damu kuvuja ndani ya ubongo.

3. Hulinda afya ya moyo
Kupumzika kuna manufaa makubwa kwenye afya ya moyo wako. Ni wazi kuwa kasi ya usukumaji wa damu wakati wa kufanya shughuli mbalimbali ni tofauti na wakati unapokuwa umepumzika.

4. Hutoa muda wa mwili kujijenga
Miili yetu inahitaji kujijenga kila mara hasa baada ya shughuli nyingi. Kwa njia ya kupumzika utaweza kuupa mwili wako nafasi nzuri ya kujijenga na kurejeshha tena nguvu iliyotumika wakati wa shughuli mbalimbali.

5. Huongeza hamasa ya utendaji
Nani anapenda kufanya kazi akiwa amechoka? Naamini hakuna. Kupata muda wa kutosha wa kupumzika kutakuwezesha kujisikia vizuri na kuwa tayari kutekeleza majukumu yaliyoko mbele yako.

6. Huimarisha misuli
Tunapopumzika misuli yetu inajijenga na kurudisha ute wake uliopotea wakati wa shughuli mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kila baada ya kazi tunapata muda wa kutosha wa kupumzika ili tuboreshe afya za miili yetu.

7. Huimarisha kinga mwili
Kinga mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga mwili kujijenga na kujiimarisha.

8. Huondoa msongo wa mawazo
Chanzo kimojawapo cha msongo wa mawazo ni uchovu, na chanzo kimojawapo cha maradhi mbalimbali ni msongo wa mawazo.

9. Hutuwezesha kula vizuri
Ni ukweli usiopingika kuwa tukiwa tumechoka hatuwezi kula vizuri. Hivyo kupata muda mzuri na wakutosha wa kupumzika kutakuwezesha kula chakula vyema.

10. Huepusha ajali za barabarani
Je, ulishasikia ajali zilizosababishwa na madereva wanaosinzia? Uchoovu na kukosa muda wa kupumzika (hasa kulala) humfanya mtu akose utulivu na uwezo wa kumudu chombo anachoedesha.
Yet kuna watu saa tina na nusu ya usiku wanaamsha watu na kuwaambia waamke eti nje kumekucha na usingizi wao si wa maana bali swala ni muhimu kuliko usingizi wao.
 
Hii ina ukweli gani, mbona tunalazimishwa tuamke alfajiri saa kumi kwenda kuswali, hapo mtu umetoka kazini usiku na kurudi nyumbani saa 8 za usiku lakini saa kumi alfajiri loud speaker zinakuamsha uamke uende kusali msikitini.
 
Ahsante kwa muongozo, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom