Fahamu falsafa ya Order out of chaos inayotumika kuleta utaratibu mpya baada ya machafuko

Fahamu falsafa ya Order out of chaos inayotumika kuleta utaratibu mpya baada ya machafuko

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habari zenu waungwana.....

Order Out of Chaos (au Ordo ab Chao ) kama ilivyosemwa kwa Kilatini, ni moja ya kauli maarufu na Kauli hii ina maana kwamba mgogoro au machafuko yanaweza kutumika kama njia ya kuleta "utaratibu" au "mabadiliko" ambayo ni yenye manufaa kwa wale walio katika madaraka.

Asili ya Kauli: Kauli ya Ordo ab Chao inasemekana kuwa ilitumiwa na Jamii za siri kama sehemu ya falsafa zao, hii inaweza kuhusishwa na mawazo ya mageuzi ya kijamii na kisiasa ambapo shida na machafuko ni sehemu muhimu ya mabadiliko.

Kauli au falsafa hii inahusisha wazo kwamba mashirika makubwa, serikali za kimataifa, au vikundi vya siri vinatengeneza au kuchochea machafuko ili kupata nafasi ya kuanzisha utawala mpya. Hii inaweza kuwa ni kupitia vita, majanga ya asili, au mabadiliko ya kijamii.

Mfano wa Historia: Unaweza kuona mifano katika historia ambapo machafuko au vita vikubwa vimezalisha mabadiliko makubwa ya kisiasa au kijamii. Mfano mzuri ni vita kuu ya Pili ya Dunia, ambapo mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisiasa yalijitokeza baada ya vita, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Albert Pike ni jina linalohusishwa na mifumo mingi ya siri, na yeye pia anatajwa mara nyingi katika muktadha wa dhana ya "Order Out of Chaos" (au Ordo ab Chao), kauli aliyo itumia katika kitabu chake cha morals and dogma (1870) ambapo alieleza ni namna gani wanaweza ktumia machafuko kutengeneza tawala na sharia mpya ulimwenguni.

Albert pike ni nani?

Albert Pike alikuwa mwanasheria, mfalme wa Freemasonry huko Marekani (33°), na mwanafalsafa maarufu wa karne ya 19. Alizaliwa mwaka wa 1809 na alifariki mwaka wa 1891, lakini jina lake linaendelea kuwa maarufu katika muktadha wa jamii za siri.

Albert Pike aliandika kuhusu oeder out of chaos akihusisha na "Three World Wars" (vita tatu za dunia), ambapo anadai kwamba kila vita kubwa itatokea kwa mpango wa kutengeneza machafuko na hatimaye kuleta mabadiliko katika utawala wa dunia.

Vita ya Kwanza ya Dunia: Ilikuwa ni njia ya kuangusha utawala wa kifalme wa Ulaya na kuanzisha Umoja wa Mataifa kama njia ya kudhibiti ulimwengu kwa njia ya kidiplomasia.

Vita ya Pili ya Dunia: Inasemekana ilikusudiwa kuharibu ngome ya ujerumani ilikuchochea ushindi wa Marekani na kuanzisha utawala wa kisasa wa kiuchumi na kisiasa (kwa mfano, Benki ya Dunia na IMF).

Vita ya Tatu ya Dunia: Inadaiwa kuwa ni vita ya kiitikadi kati ya Uislamu na Ulimwengu wa Magharibi pamoja na israel dhidi ya arabs, ambayo ingetumika kama hatua ya mwisho ya kutengeneza utawala mpya wa kisiasa na kifedha wa kimataifa.

Sasa dunia ipo katika hatua ya mwisho katika mambo hayo aliyoeleza Albert pike, ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanatokea hivi sasa na kudhihirisha matumizi ya falsafa ya order out of chaos.

Wahamiaji Haramu Kama Chombo cha Kudhoofisha Umoja wa Ulaya.

Wimbi la wahamiaji haramu katika mataifa ya ulaya huweza kusababisha yafuatayo:-

• Kuchochea Mgawanyiko wa Kijamii: Uwingi wa wahamiaji haramu unaosababisha ongezeko la idadi ya watu katika miji au maeneo fulani unaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa katika jamii. Wahamiaji haramu wanaposhindwa kuunganishwa na jamii za mwenyeji (kwa sababu ya tofauti za kiutamaduni, lugha, na rasilimali chache), hii inaweza kuchochea mivutano ya kijamii, kama vile vurugu za kijinsia, ubaguzi, na migogoro ya kikabila.

• Kutetereka kwa Usalama: Wahamiaji haramu wanaweza kuwa sehemu ya mabadiliko katika mifumo ya usalama wa ndani. Miji mingi inakumbwa na matukio ya uhalifu, vikundi vya uhalifu, na hata magaidi wanaoweza kutumia mtindo huu wa uhamiaji kama njia ya kupenya nchi na kuanzisha hatari kwa usalama wa wananchi.

Hii itatoa mwanya wa kinadharia kwa wale wanaotaka kutumia machafuko ya kijamii kama sehemu ya mipango yao ya kudhibiti hali ya usalama kwa njia ya udhibiti wa kimataifa.

Katika muktadha huu, machafuko ya kijamii na kuongezeka kwa vikwazo vya usalama vinatoa nafasi kwa serikali kuu au mashirika ya kifedha kuwa na nguvu kubwa zaidi katika udhibiti wa nchi au ulimwengu.

Mfano mwingine ni Covid-19, ambapo WHO iligeuka na kuwa mtoa taarifa na kupanga nini kifanyike dunia kote juu ya janga au tatizo la ugonjwa huo, mataifa yalipokea oder kutoka WHO na kuzifuata.

WHO ipo chini ya nani? UN pamoja na WB, IMF zipo chini ya nani?

Jibu ni kwamba taasisi hizo zipo chini ya watumiaji wa falsafa ya order out of chaos, na kwa maana hiyo, dunia itashuhudia machafuko zaidi katika sekta ya uchumi (inflation), Afya (pandemics) pamoja na sekta ya usalama (war).
 
Unamtongoza mwanamke anakukataa unampiga vibao anaanza kukuwaza mwisho anakukubalia "order out of chaos"
FB_IMG_1731268030942.jpg
 
Labda kum weka trump madarakani ni miongoni mwa steps za kuachive mipango yao
 
Back
Top Bottom