Fahamu Globus sensation "Maumivu ya koo''

Fahamu Globus sensation "Maumivu ya koo''

MIGUGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
2,137
Reaction score
3,931
Hii ni hali ya kuhisi maumivu kooni kama kuna kitu kimekwama kooni (lump in a throat). Uchunguzi unaweza kufanya lakini ukagundulika hauna kitu chochote kooni. Kwa kipindi hiki cha gonjwa la Corona watu wengi wanaweza kushikwa na uoga wakihisi hii hali ya Globus sensation.Globus sensation inaweza kusababishwa na haya:

- Kuwa na acid kali tumboni kwa hiyo unaweza kuhisi kiungulia kikali (Gastroesophageal reflux disease-GERD)
- Matatizo ya kisaikolojia kama sonona,wasiwasi(Wengi wakiwa ka stress,anxiety wanapata kama fundo hapa kooni linauma balaa)
- Mafindofindo

Ukipatwa na hii hali usiwe na wasiwasi ukahisi Covid 19 imekuvamia. Nenda hospital onana na daktari wa masikio, pua na koo (Ear,Nose and Throat-ENT)
 
Asante kwa taarifa ndugu. Wengi itatusaidie
 
Ahsante Mkuu.
Mkuu hii inatofauti gani na Soar Throat au kitu ni hicho hicho?
Soar throat husababishwa mara nyingi na virus wa flu na cold hasa kipindi cha baridi.Lakini Globus watafiti wanasema kama sio GERD yaani kuwa na acid nyingi basi ni tatizo la kisaikolojia.

Mfano unafukuzia tenda mahali Fulani halafu inachelewa huku una madeni kibao.Basi Globus sensation baadhi ya watu huwashika kwa mazingira hayo ya kashikashi za stress.
 
Back
Top Bottom