Fahamu hasara za marafiki wabaya

Fahamu hasara za marafiki wabaya

Joined
May 16, 2022
Posts
22
Reaction score
57
Siku ya Leo nitazungumzia juu ya madhara ya marafiki wabaya na kuwa nao katika maisha yako. Kwa kawaida katika maisha Kuna rafiki mzuri na rafiki mbaya ,sifa za rafiki mzuri ni kama kutunza Siri, uaminifu, uwazi, upendo na kutokuwa mnafiki.

Yafuatayo ni madhara ya marafiki wabaya ktk maisha:

1. Marafiki wabaya huvujisha Siri; watu wengi ktk jamii zetu za Kila siku wamekuwa wakilizwa na marafiki,washikaji na hata ndugu zao wa Karibu Kwa sababu wanawapatia Siri zao na mwisho kuzivujisha. Kulingana na moja ya mafundisho ya Joel nanauka alipozungumzia kuhusu aina za maadui ,alieleza kuhusu adui Delilah ambaye huchukua Siri na kuzitoa nje. Hivyo rafiki mbaya hutoa siri na kuzivujisha.

2. Marafiki wabaya humfanya mtu kuingia katika makundi mabaya; wazazi na walimu wamekuwa wakilaumiwa na wanajamii kuhusu watoto wao na tabia zao bila kujua kwamba tabia za marafiki wa watoto hao ndizo huchochea mabadiliko ya watoto wao.Mathalani makundi maovu kama ya wizi, ukahaba na madawa ya kulevya huvutia vijana Kwa sababu hupata pesa Kwa haraka sana na hivyo watoto hujihusisha na makundi hayo.

3. Marafiki wabaya ni chanzo cha kuvunjika Kwa mahusiano ya watu; suala hili linaonekana Kwa wanavyuo wengi ambapo marafiki wanaovujisha Siri na wachonganishi wamekuwa wakivujisha Siri na kupeleka maneno yasiyo ya kweli baina ya pande mbili hivyo hufanya mahusiano kuharibika katika jamii.

4. Marifiki wabaya huchochea usaliti na chuki; suala hili linaonekana hata katika mitaani kwetu ambapo marafiki huingia katika chuki na usaliti baada ya kuchonganishwa. Hivi Sasa jambo hili linaonekana Kwa wasichana ambao huitana "mashosti" lakini baadae huingia katika chuki na usaliti mkubwa.

NB: Kwa ujumla marafiki ni muhimu kutazamwa kwani ni moja kati ya vigezo vya kuzingatia katika maisha na ndio maana waingereza husema show me your friends and I will tell who you are! Asanteni. Tafadhali unaweza ongeza hasara nyingine unazofahamu
 
Just avoid people altogether 😄. Everyone comes with their baggages. Sema nini, I really hate umbea, and 90% of people's conversations ni umbea, otherwise people will find you very boring. So naonaga bora kukaa mwenyewe au kuwa msikilizaji kama siwezi kutoka Hilo eneo mf. Ofisini, ukikutana na ndugu, marafiki!
NB: kumpasha habari mumeo/mkeo sio umbea 😅
 
Just avoid people altogether 😄. Everyone comes with their baggages. Sema nini, I really hate umbea, and 90% of people's conversations ni umbea, otherwise people will find you very boring. So naonaga bora kukaa mwenyewe au kuwa msikilizaji kama siwezi kutoka Hilo eneo mf. Ofisini, ukikutana na ndugu, marafiki!
NB: kumpasha habari mumeo/mkeo sio umbea 😅
Hata nikimpasha habari shost angu sio umbea 🤣🤣 Lenie
 
Marafiki nilionao wa salamu na kuulizana na kusaidiana mambo muhimu tu, lakini wa umbea mmmmh sinaga. Hajui hata nilivyo nipoje poje [emoji3]
 
Safi sana. Kwa kweli jf tunapeana maarifa sana. Uliyoongea yana ukweli kabisa.

Mimi binafsi nina rafiki tumejuana siku nyingi sana na pia sisi ni watumiaji wa maji ya Ilala (bia). Sasa huyu muheshimiwa muamala ukisoma anakuwa yuko busy sana hatuonani, kumbe anakula matunda ya kazi ya mikono yake.

Lakini akishaishiwa atajifanya kukutafuta na kujifanya au kutunga jambo la kukusisitiza ili muonane hapo anajua anauhakika wa kula bia. Ila nili note hiyo kitu nikamrekebishia mazingira na alijua kuwa nimemstukia janja yake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom