MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
"Branding" katika biashara ni matumizi ya jina (name), maneno (terms), alama (symbols) na mitindo (designs) kwenye kutambulisha bidhaa au huduma sokoni.
"Branded Product/Service" ni bidhaa au huduma ambayo hutumia muunganiko wa jina, alama na mtindo maalum na hutambulika sokoni kwa sifa hizo.
Katika maelezo yanayofuata nitatumia neno bidhaa, nikimaanisha "both branded product and branded service"
Kuifanya bidhaa yako kufahamika na kukubalika sokoni unapaswa kuhakikisha zinakuwa na uborawa hali ya juu (quality product/service) pia kufanya matangazo kwa maana ya "promotion" mara kwa mara.
Pindi unapofanya juhudi ya kufanya bidhaa zako kufahamika na kukubalika sokoni, kuna hatua za kupitia. Hatua hizi ni kama ifuatavyo;
1. Kukataliwa (rejection) . Hii maana yake ni kwamba umepeleka bidhaa zako sokoni, bahati mbaya wateja wamezikataa. Kukataliwa kwa bidhaa zako kunaweza kusababishwa na muonekano mbaya, au kupeleka bidhaa kwenye soko ambalo si sahihi.
Ijapokuwa, SIO bidhaa zote zinapitia hatua hii, kuna bidhaa zimekubalika sokoni mara tu baada ya kuingizwa.
2. Kutokutambulika kwa bidhaa (brand nonrecognization). Kuna nyakati ni watu wa kati tu (middlemen) wanaweza wakawa wanatambua uwepo wa bidhaa zako, lakini watumiaji wa mwisho wakawa hawana taarifa juu ya uwepo wake. Hivyo ni sula la muda na matangazo litapekelea kuondoka kwenye hatua hii na kwenda hatua inayofuata.
3. Kutambulika kwa bidhaa (Brand Recognition) Hii hutokea kipindi ambacho wateja wanaanza kukumbuka bidhaa zako pindi wanapotaka kufanya manunuzi. Wakati mwingine wanaweza wasikumbuke, ila pindi waionapo, huikumbuka.
4. Kuchagua/kupendelea bidhaa zako (Brand preference) Hali hii hutokea kipindi ambacho wateja wanaanza kuchagua bidhaa zako dhidi ya bidhaa zingine.
5. Msisitizo kwenye bidhaa zako (Brand insistence) Hali hii hutokea kipindi ambacho wateja wanaanza kutafuta bidhaa zako tu pindi wafanyapo manunuzi.
Kufikia HATUA hii ndio lengo la kila mmiliki wa biashara.
Kuanzisha BRAND na kuifanya ikubalike ni gharama, na hii hupelekea baadhi ya wafanyabiashara kununua BRAND zilizoanzishwa na kukubalika (acquire established brands)
BRAND ni "asset" muhimu sana kwa kampuni. Hivyo ni vyema kuhakikisha unakuwa na "brand" zenye kubeba upekee ili kujitofautisha na washindani wako na ikibidi (fanya usajili) . Kinyume na hapo brand yako itakuwa ni mali ya umma (public property)
AHSANTE.
OMAR MSONGA (BA. PPM & CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training.
Call +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania