Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Takribani wiki ya tatu sasa mataifa mbalimbali ulimwenguni yamekuwa yakichukua hatua mbalimbali kukabiliana na usambaaji wa Virusi vya Corona nchini mwao.
Virusi hivi vinavyoshambulia mapafu na kusababisha homa kali, mafua, kikohozi pamoja na upumuaji wa shida viliibukia huko China katika Mji wa Wuhani na kuonea katika mataifa mbalimbali ulimwenguni kwa kasi ya ajabu.
Mpaka sasa yapata zaidi ya wiki tatu virusi hivi vimeshaenea katika mataifa mbalimbali ya bara la ulaya, Bara la Afrika, Bara la Amerika, Bara la Australia na maeneo mengine mengi ulimwenguni.
Kufuatia athari mbalimbali za ugonjwa huu kama vile vifo vya maelfu ya watu, kuumwa kwa idadi kubwa ya watu na usambaaji wake wa kasi, Mataifa mbalimbali ulimwenguni yamekuwa yakichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha janga hili linatokomea na halileti athari kubwa.
Katika uzi huu, nitakuwa nikileta hatua tofauti tofauti zinazochukuliwa na mataifa tofauti ulimwenguni kama njia ya kukabiliana na jang hili. Zifuatazo ni baadhi ya hatua zilizochukuliwa na nchi hizo:
NCHI ZA BARA LA ASIA:
Inaelezwa kuwa virusi vya Corona vimesambaa katika mataifa mbalimbali ya bara la Asia na nchi hizo zimeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuweza kukabiliana na janga la Covid 19. Hizi ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na nchi zifuatazo:
China
Nchi hii ndiko ambako virusi vya Corona vilianzia. Licha ya kupata wagonjwa wengi lakini serikali ya nchi hii ilijitahidi kujenga hospitali ya dharura kwa lengo la kuitumia kuhifadhi na kuwatibia watu walioambukizwa virusi vya Corona.
Sambambna na hilo, Mji ambao ndiko ugonjwa huu ulianzia (Wuhani) nchi hii ilifunga mipaka na kuhakikisha hakuna mtu anayeingia wala kutoka katika nchi mji huo ili kutoeneza mahali kwingine. Vilevile, shughuli zote za kimichezo na mikusanyiko imezuiliwa mpaka pale itakapo tangazwa kwa mara nyingine.
Zaidi ya hayo, licha ya taarifa za wiki iliyopita kueleza kuwa hali imeanza kuwa shwari na shughuli kurejea nchini China lakini bado leo hii mamlaka za Mji wa Hong Kong zimeeleza hadi kufikia jumatano ya wiki hii watu ambao sio wakazi wa Mji huo (Hong Kong) hawatoruhusiwa kuingia.
Urusi
Licha ya Urusi kuwa na zaidi ya watu milioni 146 lakini inaelezwa kuwa na kesi zipatazo 239 za Covid 19. Aidha inaelezwa kuwa Urusi iliamua kufunga mipaka yake na China tangu Januari 30 na kutengeneza Karantini za kuwatenga waathirika kwa muda kwa lengo la kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.
Sambamba na hilo, Urusi imeendelea kuwasisitiza watu wake kujifungia na kutokuwa katika msongamano ya watu ili kueouka janga hilo kuenea nchini humo.
Zaidi ya hayo, Urusi imetoa vifaa na matabibu mbalimbali na kupeleka nchini Italia ili kusaidia kukabiliana na Virusi vya Corona sehemu ambayo inaelezwa kuathirika zaidi na virusi hivyo ulimwenguni.
Qatar
Serikali ya Qatar imetangaza zuio la wiki mbili kwa watu wote wasio Raia wa nchi hiyo kuingia ndani ya nchi yao pamoja na kuwekeza dola takribani bilioni 20 katika wizara ya Afya kwa lengo la kuongeza nguvu katika kukabiliana na Virusi vya Corona.
Sambamba na hilo taifa hilo limezuia safari za ndege zote kutoka nje ya nchi kuingia Qatari kwa wiki mbili isipokuwa kwa zile tu zenye raia wa nchi hizo. Hizi hatua zote zimelenga kupambana na usambaaji wa virusi vya Covid nchini mwao.
India
Waziri Mkuu wa India ameagiza wananchi wote kukaa nyumbani kwa muda wa siku 21 kuanzia leo. Mkakati huo unalenga kudhibiti maambukizi ya COVID-19 nchini humo ambapo hasi sasa watu zaidi ya 500 wameripotiwa kuwa na maambukizi na 11 wamefariki dunia.
Sehemu za ibada, maduka, masoko na ofisi zote nchi nzima zitafungwa. Huduma na usafiri wa umma nazo zitasitishwa wa muda wote ambao nchi nzima imewekwa karantini
NCHI ZA BARA LA ULAYA
Nchi mbalimbali za Ulaya zimeathirika na Ugonjwa huu, Idadi kubwa ya vifo pamoja na kesi za ugonjwa huu zimeripotiwa kutoka bara hili. Aidha, kutokana na gonjwa hili kuenea kwa kasi kubwa na kusababisha kifo cha maelfu katika bara hili nchi mbalimbali zimechukua tahadhari mbalimbali.
Italia
Inaelezwa hili ndilo t6aifa lililoathirika zaidi na Covid 19, huku kukiwa na idadi kubwa ya kesi zilizoripoitiwa pamoja na vifo vya zaidi ya watu 5000.
Licha ya kuwa viongozi wa nchi hii wamekiri kuwapo kwa ugumu wa kupambana na ugonjwa huu lakini bado raia wa nchi hiyo wamesisitizwa kuendelea kujifungia ndani huku ulinzi mkali ukifanywa kuhakikisha watu hawachangamani.
Zaidi ya hayo, Nchi ya Italia imefunga mipaka yake kwa raia wowote wa kigeni na kuzuia raia wake kusafiri ili kuhakikisha virusi vya Corona haviongezi athari katika nchi yao. Vile vile, shirikisho la michezo la nchi hiyo limesimamisha shughuli zote za kimichezo na kuelekeza nguvu zake katika sekta ya afya ili kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya jnaga hili.
Uingereza
Taifa limezidi kuchukua tahadhari kwa kuboresha huduma za afya ili kuwatibu raia walioathirika na ugonjwa huo. sambamba na hilo, raia wa kigeni waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo kwa sababu mbalimbali ikiwamo masomo n.k wamelazimika kurudi katika mataifa yao.
Zaidi ya hayo, nchi hi imezuia mikusanyiko mbalimbali ya raia ikiwamo kusimamisha michezo ya ligi zote ili kuhakikisha raia wake hawachangamani.
Leotarehe 25-03-2020, Uingereza yawataka watu kukaa ndani. Mikusanyiko zaidi ya wawili marufuku.
Watu wameambiwa kuwa wanaweza kwenda kufanya mazoezi nje mara moja kwa siku, kwenda ofisini panapo ulazima, kwenda dukani kwa mahitaji muhimu na kwenda hospitali.
Ukraine
Shirika la reli ya nchi hiyo limepiga marufuku treni za abiria za mataifa mengine kuingia katika nchi hiyo ili kuzuia ueneaji wa Covid 19.
Zaidi ya hayo, Serikali ya Ukraine imepiga marufuku ndege zote kutoka mataifa mengine kuingia katika nchi hiyo na wageni mbalimbali kutoka mataifa mengine mpaka mnamo Aprili 3.
Ujerumani
jimbo la North Rhine Westphalia limetangaza kuwa shule zake zote zinapaswa kufungwa ifikapo Jumatano ijayo hadi mwishoni mwa likizo ya Pasaka.
Na mshambuliaji wa klabu ya Paderborn ya Ujerumani Luca Kilian amegundulika kuambukizwa virusi vya Corona , akiwa ni mchezaji wa kwanza katika ligi ya Bundesliga kuathirika.
Taarifa hizo zimetolewa muda mfupi baada ya shirikisho la soka Ujerumani DFL kuahirisha michezo ya wikiendi hii ya ligi kuu na ligi ya pili. Ujerumani sasa inaungana na England, Uhispania, Italia, na Ufaransa kusitisha ligi yake kutokana na maradhi hayo.
NCHI ZA BARA LA AMERIKA
Nchi mbalimbali za bara hili zimeripoti kesi mbalimbali za kuwapo kwa watu wenye Virusi vya Corona. Aidha, kutokana na janga hili nchi nyingi zimezuia safari za nje na zimesimamisha kupokea wageni kutoka mataifa mengine. Zifuatazo ni baadhi ya hatua zilizochukuliwa na nchi hizi:
Marekani
Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kutokana na kuenea kwa virusi vya corona, pamoja na upatikanaji wa karibu dola bilioni 50 kama msaada zaidi wa serikali ya shirikisho kupambana na ugonjwa huo.
Trump ametoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari na kusema kwamba hali nchini humo inaweza kuwa mbaya zaidi na kwamba "wiki nane zinazofuata zinaweza kuwa mbaya sana".
Trump amekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wataalamu juu ya hatua za kujivuta na zisizo na ufanisi katika kushughulikia janga hilo.
Hatua za hivi karibuni za Marekani zimekuja siku mbili baada ya Trump kupiga marufuku watu kuingia nchini humo hususan wakutokea Ulaya.
Trump ambaye hapo awali alionekana kusimama kando ya afisa wa Brazil ambaye ameambukizwa COVID-19, amesema kwamba hata mwenyewe atafanyiwa vipimo haraka iwezekanavyo, lakini akaongeza kwamba hatojiweka karantini kwasababu hana dalili zozote.
Zaidi ya hayo, ligi za michezo mbalimbali ikiwamo ligi mchezo pendwa wa kikapu NBA nchini Marekani imetangazwa kusitishwa mpaka pindi pale hali hii itakapotulia.
26-03-2020, Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha Dola za Kimarekani Trilioni 2 kwa ajili ya kusaidia mifumo ya afya, wafanyakazi na biashara zilizoathiriwa na mlipuko wa #corona
Marekani ina jumla ya maambukizi 68,489, vifo 1,032 na waliopona ni 394. Nchi hiyo ina idadi ya Watu milioni 329 na Watu 418,810 wamepimwa hiyo inamaanisha mtu mmoja kati ya 785 waliopimwa, ameathirika
Serikali ya Urusi imeiagiza Mamlaka ya Anga nchini humo kusitisha safari zote za Kimataifa za ndege zinazoingia na kutoka kuanzia Kesho Machi 27
Thailand imetangaza maambukizi mapya 111 na kufanya nchi hiyo kuwa na maambukizi 1,045 huku ikizuia wale wote wasio raia, Wanadiplomasia au wenye vibali vya kutofanya kazi nchini humo kutoingia.
NCHI ZA BARA LA AFRIKA
Nchi mbalimbali za Afrika zimeendelea kutangaza kufunga mipaka yake pamoja na kuzuia shughuli za kijamii zinazowafanya watu wengi wachangamane. Mpaka sasa inaelezwa kesi za Corona zaidi ya 700 zimesharipotiwa katika nchi mbalimbali za Afrika. Hizi ni baadhi ya hatua zilizochukuliuwa na baadhi ya nchi.
Nigeria
Taifa hilo limeeleza kuwa litafunga shule zote pamoja na kuzuia mikusanyiko mbalimbali ikiwamo mikusanyiko ya kidini.
Zaidi ya hayo nchi hiyo imeamua kuweka kizuizi kwa mikusanyiko katika Mji wa Lagos. Aidha, mamlaka zimekiri ugumu wa kuzuia mikusanyiko katika mji huo kutokana na kuwepo maelfu ya watu wanaofanya ibada katika maeneo hayo na kubana kwa nyumba lakini mamlaka zimesisitiza kuwa zitaendelea kuzuia mikusanyiko ya watu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Afrika Kusini
Serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuwa itaweka uzio wa kilomita 40 kati yake na nchi ya Zimbabwe ili kuhakikisha kuwa hakuna maambukizi yanayoingia kutoka nchi jirani.
Aidha, Rais wa nchi hiyo Cyrill Ramaphosa ametangaza siku 21 za wananchi wote kujifungia ndani ilikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya #COVID19 nchini humo kuanzia leo tarehe 24/03/2020.
Rais Ramaphosa amesema wakati wa mpango huo ambao unatarajiwa kumalizika Aprili 16 hakuna mtu ataruhusiwa kutokana nyumbani na watakosimamia jambo hilo ni idara ya maafa ya nchi hiyo.
Katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa Idara ya Majanga, Polisi na Watumishi wa Afya ambao watakuwa wakiwazungukiwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu ambayo ni pamoja na chakula
Mauritania
Serikali ya nchi hiyo imefunga viwanja vyake vya ndege na kuzuia ndege kwenda na kuingia kutoka nje ya nchi. Sambamba na hilo nchi hiyo imetangaza kufunga shule zake zote na kuzuia shughuli za mikusanyiko ya watu.
Senegal
Nchi hii imetangaza jumla ya kesi 38 za Covid-19. AIdha serikali hiyo ilitangaza kufunga misikiti yote iliyopo katika mji mkuu wa Dakar hadi taarifa zaidi zitakapotolewa.
Congo DRC
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza hali ya dharura na kuufunga mji mkuu wa Kinshasa au kujitenga katika hatua ya kupambana dhidi ya maambukizi ya corona.
Rais Félix Tshisekedi ametangaza kuchukua hatua hizo siku ya Jumanne jioni kupitia televisheni ya taifa.
Bwana Tshisekedi amesema kuwa pamoja na kufunga mipaka ya nchi, kusitisha safari za ndani na nje ya mji mkuu zikiwemo za mabasi, ndege na maji, utekelezaji wa haraka unahitajika.
Wiki iliyopita Jamhuri ya Afrika ya kati ilitoa amri kwa raia wake kutokuwa na mizunguko.
Mpaka sasa DRC imeripotiwa kuwa na wagonjwa 48 wa covid-19 na watu watatu kufariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo.
Mji mkubwa wa pili wa taifa hilo, Lubumbashi, ulifungwa kwa saa 48-siku ya jumatatu baada ya watu wawili kukutwa na maambukizi ya Covid-19.
Mmoja alikuwa mwanamume mwenye miaka 47 na mtoto wake wa kiume wa miaka 13, walikuwa wametokea mji mkuu wa Kinshasa siku ya Jumapili.
Na siku hiyohiyo , kifo cha pili kilichotokana na ugonjwa wa corona kilitangazwa na waziri wa afya, Eteni Longondo huku wengine 30 walikutwa na maambukizi ya ugonjwa huo tangu March 10, 2020.
ETHIOPIA
Zaidi ya wafungwa 4,000 wameachiwa huru nchini Ethiopia ikiwa ni hatua ambayo serikali hiyo imechukua ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Mwanasheria Mkuu alisema siku ya Jumatano kuwa wafungwa wote walioadhibiwa kwa kesi ndogondogo na wanawake ambao wana watoto ndio wataoachiwa huru.
Wageni ambao walishtakiwa kwa makosa ya usafirishaji haramu na dawa za kulevya wataachiwa huru pia na kurudishwa katika nchi zao.
Hatua nyingine ambazo Ethiopia imezichukua kukabiliana na maambukizi ya corona ni wafanyakazi wengi kufanyia kazi nyumbani pamoja na kufunga mipaka yake yote.
Abiria wote wanaowasili Ethiopia wanapaswa kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hoteli ambazo zimechaguliwa na mamlaka.
Zaidi ya wasafiri 400 wameanza kukaa katika karantini kwa lazima, kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini humo.
Taifa hilo limefunga kumbi zote za starehe za usiku.
Mpaka sasa Ethiopia ina wagonjwa 12 wa Covid-19.
NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
Mpaka kufikia sasa nchi zote za Afrika Mashariki zikiwamo Kenya Tanzania, Rwanda na Uganda zimethibitisha kuwapo kwa visa kadhaa vya Corona Virus katika nchi zao. Kufuatia visa hivyo nchi hizi zimechukua hatua mbalimbali kama sehemu ya kujikinga na janga hili.
Kenya
Rais wa nchi hii ametangaza kuzuia safari za nje ya nchi kwa siku 30. Sambamba na hilo, Rais Kenyatta amezitaka taasisi za elimu za nchi hiyo kufungwa kwa siku 30 pamoja na kufunga sehemu za mikusanyiko ikiwamo Baa na Vilabu vya starehe vyote.
Sambamba na hilo safari za kimataifa za kuingia katika nchi hiyo zitafutwa kuanzia Jumatano, Mach 25, 2020. Kila atakayetembelea Kenya atawekwa karantini mara baada ya kuwasili. vilevile, Kenya Airways imesitisha safari zote za kimataifa.
Zaidi ya hayo nchi hiyo imepanga kutengeneza sanitizer na kuzigawa bure kwa wananchi ili waweze kujilinda dhidi ya virusi vya corona.
Tanzania
Mpaka sasa kesi za Corona zilizothibitishwa ni 12. Serikali kupitia Waziri Mkuu ndugu Kassim Majaliwa ilitangaza kufunga shule zote kuanzia ngazi ya awali mpaka Vyuo vikuu kwa siku 30 kama sehemu ya kukabiliana na Usambaaji wa virusi vya Corona.
Vilevile, Serikali inaendelea kuonya na kutoa elimu kwa watu kuhusu umuhimu wa kuepuka mikusanyiko na kunawa mikono kwa sanitizers ili kuhakikisha raia wake wanabaki salama.
Zaidi ya hayo, Rais Magufuli ametangaza kusimamisha shughuli za mbio za mwenge na kuhimiza kuwa pesa hiyo iende wizara ya Afya ili kuongeza nguvu ya kupambana dhidi ya virus vya Corona.
Hata hivyo, Rais ameeleza kuwa shughuli za ibada na biashara zitaendelea katika nchi hiyo kama kawaida.
Rwanda
Serikali ya Rwanda imechukua hatua zifuatazo ambazo kupiga vita maambukizi ya #CoronaVirus nchini kwao. Hatua hizi zimeanza kutekelezwa Machi 21, na zitadumu kwa wiki mbili
Pia, nchi imeagiza malipo kufanyika kwa njia ya mtandao kila inapowezekana badala ya ATM. Wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi wametakiwa kufanyia kazi nyumbani, isipokuwa wale wanaotoa huduma muhimu tu.
Matembezi yasiyo ya lazima nje ya nyumbani halikadhalika yamekatazwa
Mipaka yote imefungwa, isipokuwa kwa mizigo inayoingia Rwanda, au wanyarwanda wanaorudi nyumbani, ambao pia watapaswa kutengwa kwa siku 14. Kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine imezuiliwa isipokuwa kwa sababu za kimatibabu
Maduka na masoko na baa zote zimefungwa, masoko ya bidhaa za usafi na madawa yameruhusiwa. Bodaboda haziruhusiwi kubeba abiria, ila wanaruhusiwa kupeleka mizigo kwa wateja ‘delivery’
Migahawa imeruhusiwa kutoa huduma ya chakula kwa ‘take away’ na sio kulia mgahawani.
Vyombo vya usalama na serikali wametakiwa kuhakikisha sheria hizo zinafuatwa
Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kupiga marufuku mikutano mikubwa ya umma ikiwa ni pamoja na harusi, huduma za kanisa na Jumat kwa siku 32 zijazo kwa nia ya kusaidia kuzuia kuenea kwa coronavirus.
Museveni pia alitangaza kufungwa kwa shule ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu akitoa mfano wa hitaji la kuzuia kuongezeka kwa kesi kutoka nchi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Benki, hospitali, maduka makubwa na masoko hazijaathiriwa na maagizo, lakini zile zinazofanya kazi lazima zifuate hatua za usafi na pia wape wafanyakazi wao na wale wanaokuja kwenye uanzishwaji wao na watendaji wa usafi.
Vizuizi vya harakati vitaathiri sikukuu za Pasaka na huduma za kidini - lakini Museveni alisema ni bora kwa raia kuchukuwa tahadhari.
Zaidi ya hayo, leo tarehe 25-03-2020 Rais Yoweri Museveni amesema kuwa katika kupambana na #Covid_19 wanasitisha usafiri wa Umma zikiwemo Daladala, taksi, bajaji na bodaboda kwa siku 14
Usafiri utakaoruhusiwa ni binafsi tena wasipande zaidi ya watu watatu na dereva akiwa amejumuishwa kwenye idadi hiyo
Magari mengine yatakayoruhusiwa kutembea ni magari ya mizigo na yale yanayofanya ‘delivery’ na yakiwa yamebeba bidhaa muhimu kama chakula. Hata bajaji na bodaboda kama zitabeba mizigo muhimu kama chakula zitatuhusiwa
Magari mengine yatakayoruhusiwa kufanya kazi ni magari ya Jeshi, Zimamoto na Polisi, magari ya kuzoa taka na baadhi ya magari ya idara za Serikali kwa ajili ya kufanya kazi za jamii.
Zanzibar
Serikali visiwani humo imesema licha ya kutegemea Utalii katika uchumi wake imezuia safari zote za watalii kuingia.
Aidha, serikali ya Zanzibar imesisitiza kuwa yeyote atakayewasili visiwani humo atakaa karantini kwa siku 14 kwa gharama zake.
Zaidi ya hayo, Zanzibar yafunga kumbi zote za starehe na mikusanyiko ya aina mbalimbali. Sambamba na hiilo watu wote wanaokwenda sokoni wamesisitizwa kutogeuza soko kuwa sehemu ya mazungumzo na ukomo wa muda wa masoko ni saa 12 jioni
Aidha, Zanzibar imepiga marufuku mikusanyiko yote inayokutanisha watu wengi kwa pamoja ikiwemo Michezo, harusi na mikutano.
===
Nini maoni yako kutokana na hatua iliyochukuliwa na nchi yako?