masahihisho kidogo. petroli yote inayouzwa ni unleaded, kwa maana kwamba haijaongezwa tetraethyllead (TEL), hii additive ilikua inaongezewa kwenye petroli ili ku boost octane ratings za petroli na hivyo kuongeza ufanisi wa injini, lakini baada ya madhara ya lead kuonekana ni makubwa katika uchafuzi wa mazingira nchi nyingi duniani zilipiga marufuku matumizi ya leaded gassoline, nchi pekee ambazo bado leaded gassoline inarihusiwa ni Afghanistan, Argeria, Iraq, North korea, Myanmar na Yemen. sasa ni nini tofauti ya "unleaded" na "super unleaded" petrol?
super unleaded petrol (super) inakuwa na ongezeko la octane ratings (RON), ongezeko hilo la octane rating hua linaongeza engine performance na kupunguza matumizi ya mafuta. ingawa kiuhalisia tufauti hua ni ndogo sana hususani kama wewe ni mtu wa kuchanganya mafuta leo regular unleaded (a.k.a unleaded) kesho super unleaded (a.k.a super), hutaona tofauti yoyote. pia sina uhakika kwa hapa Tanzania kama kuna petrol station wanayouza super unleaded petrol zaidi ya mabango tu yanayosema "super", kwasababu kiuhalisia super ni gharama zaidi kuliko regular unleaded petrol