Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
MJUE RAIS MTEULE WA MALAWI MH LAZARUS MCCARTHY CHAKWERA
Na Elius Ndabila
0768239284
Nchi ya Malawi wiki hii ilifanya uchaguzi ambao matokeo rasmi yametangazwa leo na kumpatia ushindi Mh CHAKWERA. Ikumbukwe Malawi imefanya Uchaguzi huu baada ya mahakama ya juu ya Malawi kutengua matokeo yaliyo mpa ushindi Mh Mutharika kuwa yaligubikwa na stofahamu nyingi. Malawi inakuwa nchi ya pili kwa Afrika kwa matokeo yake kutenguliwa na Mahakama, ilikuwa hivyo kwa Kenya mwaka 2017. Mwanzo baada ya matokeo kutenguliwa moja ya makala zangu nilizungumzia historia ya Malawi na viongozi mbalimbali waliowahi kuwa Marais wa Malawi. Leo nataka niwapitishe kidogo kwa Rais Mteule Mh CHAKWERA.
Mh CHAKWERA hajaandikwa sana kwenye historia ya Malawi, hasa kutokana na uchanga wake kwenye masuala ya kisiasa. Lakini nimejitahidi kupitia maandiko mbalimbali yaliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza na Kichewa ili kuweza kupata walau mambo machache yanayo mhusu. Mh CHAKWERA alizaliwa 5/4/1955. Dini yake ni Mkiristo ambaye anaumini katika kanisa la Assemblies of God. Alikuwa Rais/ Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God nchini Malawi tangu mwaka 1989 mpaka 2013, na Mwaka 2013 alichaguliwa kuwa Rais wa chama cha Malawi Congress Party, na pia alichaguliwa kuwa Kiongozi mkuu wa Upinzani bungeni (KUB).
CHAKWERA amezaliwa katika mji wa Lilongwe ambao ni mji mkuu wa Malawi. Kaka zake wawili walifariki kwa infancy, lakini babake aliamini CHAKWERA ataishi na akampatia jina la LAZARUS ambalo Kiblia lina maana kubwa(Who was raised from the dead). Kwenye familia amebahatika kuishi yeye na Dada yake.
CHAKWERA alifanikiwa kuoa mke wake anayejulikana kwa jina la Monica na wamejaliwa kupata watoto wanne na wajukuu.
Alihitimu elimu yake mwaka 1977 Bachelor of Arts (Philosophy) katika chuo kikuu cha Malawi. Alijaliwa kusoma katika vyuo mbalimbali vikiwemo vyuo vya elimu ya dini. Kwa hiyo ni mtu ambaye pia ni mtaalamu wa mambo ya dini aliyosoma kwenye chuo cha The Pan Africa Theological Seminar.
CHAKWERA alikuwa instructor wa chuo cha Assemblies of God cha Theology mwaka 1983 hadi 2000 ambapo mwaka 1996 alipanda na kuwa Principal. Kutokana na kukulia kwenye dini iliwashitua watu wengi mwaka 2013 alipoamua kuingia kwenye siasa ijapo alipata Wafuasi wengi kwenye chama cha MCP kutokana na historia yake. Wakati huo alikuwa bado ni Rais wa Assemblies of God, hata alipogombea uongozi wa chama hicho alishinda kwa kishindo/ landslide Victory.
Ilimchukua muda mrefu kuingia kwenye siasa, ijapo kwa muda mrefu vyombo vya habari vya Malawi vilikuwa vikiandika juu yake kutaka kuingia kwenye siasa. Hata Wafuasi wa MCP walianza kumuomba kwani waliamini kutoka na umaarufu alionao angewasaidia. Ni kweli alipojiunga na chama hicho, chama kilipata nguvu na wawakilishi wengi mwaka 2014 alipoongoza chama hicho kwenye uchaguzi.
Uchaguzi wa Mwaka 2014 walisema ameshinda na Wafuasi wake walitaka kuingia barabarani kushinikiza kubatilisha matokeo ili atangazwe yeye. Lakini aliwatuliza Wamalawi kutokufanya fujo na kuwasihi kuwa gharama ya kuondoa amani Malawi mbaya kuliko yeye kupewa Urais. Aliwaambia Kama Mungu hajaamua acheni, wakati wa Mungu utakapofika hatutahitaji kumwaga damu ili tupate kuiongoza Malawi. Aliendelea kuwa Mbunge wa jimbo la Lilongwe North West. Wakati huo wote akiwa anafanya siasa alikuwa ameshaachana kuliongoza kanisa tangu mwaka 2013 kwani alisema this would enable him to concentrate more on front-line politics.
CHAKWERA aliamini ili kushinda uchaguzi Malawi wanapaswa kuungana, ndiyo maana aliamua kuungana na DKT SAULOS CHILIMA kwa uchunguzi wa june 2020 baada ya janja janja ya Mutharika na Wafuasi wake kukwama.
Nchi ya Malawi ambayo sasa ilikuwa imeyumba sana hasa kwenye suala la uchumi wanaamini CHAKWERA atasaidia kuuinua.