Fahamu immobilizer system kwenye gari

Fahamu immobilizer system kwenye gari

Labda nifahamu, funguo zilizopo nitaendelea kutumia?

Funguo utatumia hizo hizo,ila tu kutakua na sensor ambayo inatakiwa ikae kwenye holder moja na funguo ili uweze kuwasha gar,bila hicho ki sensor kuwepo gar haiwaki
 
Funguo utatumia hizo hizo,ila tu kutakua na sensor ambayo inatakiwa ikae kwenye holder moja na funguo ili uweze kuwasha gar,bila hicho ki sensor kuwepo gar haiwaki
ok, na je kwenye gari yenyewe inafanywa nini? control box itabakia ile ile?
 
Kwenye gar hamna kitu kinachobadilika,zaidi ni hicho ki control cha immobilizer ndo kitaongezeka
ok, naomba unielezee kwa ufasaha, ninayo land cruiser 2016 model na hiyo IST, land cruiser inatumia hiyo system ya immobilizer, lakini IST nimefunga car alarm system nzuri sana na pia inayo alarm system ilikuja nayo toka Japan. Kwa mtizamo wako, ipo haja ya kufunga hiyo system ya imobilizer?
 
ok, naomba unielezee kwa ufasaha, ninayo land cruiser 2016 model na hiyo IST, land cruiser inatumia hiyo system ya immobilizer, lakini IST nimefunga car alarm system nzuri sana na pia inayo alarm system ilikuja nayo toka Japan. Kwa mtizamo wako, ipo haja ya kufunga hiyo system ya imobilizer?

Hapana,maana ufanyaji kazi wa alarm system hautofautiani sana na hizi immobilizer za kufunga
 
Je ulishawahi kusikia watu au fundi anakuambia gari limeingia kwenye immobilizer na ukashindwa kufahamu nini?

Immobilizer ni mfumo wa security ya funguo katika gari. Mfumo huu umewekwa ili kudhibiti wizi wa magari, kwani mtu akichonga funguo aina sawa na gari hawezi kuliwasha.

JINSI MFUMO UNAVOFANYA KAZI

Mfumo huu unafanya kazi kutokana na sensor(transponder) ambayo inakua kwenye funguo wa gari husika, sensor hii hutumika kama utambuzi wa funguo ni sahihi wa gari hilo au la,kama ni sahihi basi sensor hiyo hutoa signal kwenye immobilizer, na immobilizer huruhusu mfumo wa mafuta, spark na ignition kufanya kazi na kuwezesha gari kuwaka.

Kama funguo itakua ni tofauti, basi immobilizer hupata signal tofauti, hivyo basi huzuia mfumo wa mafuta, spark na starter kufanya kazi na kupelekea gari kuto kuwaka.

VITU VINAVYO SABABISHA GARI KUINGIZA FAULT YA IMMOBILIZER

Kwanza kabisa ni ufunguo wa gar kupotea, hii husababisha gari kutokuwaka hata pale utakapochonga ufunguo sawa na wa mwanzo. Kwani inahitajika kuprogram sensor nyingine ambayo itawekwa kwenye ufunguo ili kuwezesha gari kuwaka.

Kudondosha funguo mara kwa mara hii husababisha sensor kuvunjika kwa ndani, pia funguo kuingiliwa na maji kwani hua yanatengezeza unyevu ambao pia una haribu ile sensor na kusababisha gari kuto kuwaka.

BAADHI YA ALAMA ZA TAA KWENYE GARI ILI KUJUA GARI KAMA IMEINGIA KWENYE IMMOBILIZER
9626ce6e847a4927b56237fef894f6c9.jpg
8202bd9564cfe57ee09806a39af309e2.jpg
1330d3fd01797f349fd693096a9817a3.jpg

*KAMA UNA SWALI USISITE KUULIZA*
Wekeni contact zenu,mf. simu, instagram accnt, FB....etca watu waweze kuwatafuta maana si kila mtu anapitia hizi uzi za JF.
 
Mueleweshe kuwa ukipoteza ufunguo kuna code wamekuandikia unaituma japan wanakuletea funguo nyingine. Kusema za ukweli hii ni ulinzi tosha wa gari na wengine imetusaidia sana
Sasa mbona bado magari yanaaibiwa kama kawa... Umeandika uongo?
 
Dah, hii ishu ilinitoka laki 3.5 hivi hivi kizembe zembe,..nilimrushia funguo muosha magari akashindwa kuidaka ikaanguka, utumbo wa ndani ukatoka. Kaiokota kairudisha fresh tu, kujakuiwasha gari ngoma haiwaki (inatekenyeka lakin haipokei). Kwenye dashboard kuna kialama cha funguo kina blink. Kumbe kuna kidude kidogo sana ndio sensa kimepotea funguo ilipo anguka. Laki3 na nusu hivi hivi zikanitoka ili fundi kuchokonoa control box na kuiprogram upya. Niliumia sana kwa uzembe wangu.
Laki tatu point five?
Alinunua kifaa chochote ama hiyo yote ilikua hela ya ufundi
 
Kwa gari zenye ufunguo wa sensor hawezi,maana ina process ndefu ya kufanya programming. Inachukua masaa mawil hadi sita kwa baadhi ya gari
548bb8f5579bb5e1a1d55f334f11b4f0.jpg
3c7d96022e2f574b8d24eb226b56fa0c.jpg
We jamaa sikuelewi ujue.
Mbona daily nasikia taarifa za magari tena hadi ya kisasa watu wanaibiwa?
Halafu unasema eti hawawezi kuiba.
 
hivi mkuu kibongo bongo naweza pata kweli mtu wa kunifundisha hiyo kitu?? sitaki kufundishwa kuprogram kwa kucopy na kupaste .but mm nataka niandike data mwenyewe inamaana niwe naweza kutengeneza file mwenyewe kwa kuandika kwenye eeprom na chip ya kwenye funguo.

sijui kama utakuwa umenielewa mkuu labda nikupe mfano huu. nikupe eeprom ya kwenye dash board ambayo ni mpya haina data hata moja then nikwambie uniandikie data ilinikiweka eeprom kwenye cluster isome 967208KM trip A 380 Trip B 100. ndio kitu nataka mm kufaham hivyo mkuu
Ulifanikiwa kupata mtu akakupiga pindi?
Uli hustle sana?
 
mashine gani ya nini na ufundishe nn?? mm na mashine ya digpro 3 ya kushushia KM inanizingua sana
Kumbe we jamaa unafanya kazi za kissenge na magendo namna hii za kushusha kilometers za ODOMETER.

Kwanini unafanya hivi... Kwa faida ya nani
 
Back
Top Bottom