Job K
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 9,314
- 7,149
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HaaaaaaaaaaHahahaha sawa kuna Mzee wangu alikuwa anatumia ya kujengea....nilkuwa sielewi....
Huyu daktari anamwagia kitumbua chako mchanga eeeh? Mbona povu jingi mkuu.[emoji1]Huku Dr. umevamia fani! Tunawajua nyie Vet huku hamwezi!
Kawaida sana hii mkuu maana ingekuwa hivyo madaktari wasingekuwa wanawaandikia wagonjwa dawa pindi wanapomaliza kufanyiwa vipimo maana watakuwa wanaingilia majukumu ya pharmacist.Huyu daktari anamwagia kitumbua chako mchanga eeeh? Mbona povu jingi mkuu.[emoji1]
Karibu sana.Tunashukuru somo zuri
Kuku kudonoana ni shauri ya upungufu wa madini katika mwilli, hivyo unashauriwa kuwapa madini hasahasa calcium na phosphorus (DCP) katika chakula chao.Dr asante kwa huu uzi, mimi ni mfugaji wa kuroila, maswali yangu ni haya
1. Kuku wangu wanang'atana sana mpaka kuuana, nimeshawapa damu iliokaushwa,chokaa,OCT, na pia mara nyingi mlo wao haukosi dagaa, nini tiba?
2. Naomba ufafanuzi pale uliposema kuku mdogo anayetaga anahitaji 4.5 kg kwa muda wa miezi miwili, je hii kg 4.5kg ni kwa siku moja? kama ndio mbona mimi mwenyewe siwezi kula kg4.5 per day?
Asante mkuu, nimepata kitu hasa hapo kwenye chakula mi hua nakadiria tu kwa sababu hawa kuku wanakula mno.Kuku kudonoana ni shauri ya upungufu wa madini katika mwilli... hivyo unashauriwa kuwapa madini hasahasa calcium na phosphorus (DCP) katika chakula chao.....
Pia jaribu kuwapa kuku wako chakula cha kutosha na ikiwezekana wape na mbogamboga hasahasa michicha au lucerna... pia hakikisha unawaweka kuku katika eneo linalowatosheleza kuepuka overcrowding na kama tatizo likiendelea kuwa kubwa basi ni vyema kuwakata midomo
Kuhusiana na chakula kwa kawaida kuku mkubwa na anayetaga anatakiwa kula gm120 kwa siku hivyo bhasi kwa hesabu za haraka kwa miezi 2 anatakiwa kula kiasi cha kilo7.2 na imani nitakuwa nimejibu swali lako mkuu
Wapatie mkuu hakutakuwa na tatizo tatizo huwa linakuja baadaa ya kuwapa chanjo kuku wakiwa wagonjwa ila kama ni wazima ruksa kuwapa then baada ya hapo note tarehe kwa ajili ya kuwapa chanjo kila baada ya miezi mitatu mitatu...asante mkuu, nimepata kitu hasa hapo kwenye chakula mi hua nakadiria tu kwa sababu hawa kuku wanakula mno.
pia nimepitia uzi wako mmoja kuhusu chanjo, nimechelewa kuwapa chanjo ya tat ua newcastle, nimechelewa kwa mwezi sasa, naweza kuwapa au nipotezee?
Nami naomba nichangie kiduchu ingawa mleta uzi amajibu kwaa usahihi na kwa ufupi unaoleweka.Dr asante kwa huu uzi, mimi ni mfugaji wa kuroila, maswali yangu ni haya
1.kuku wangu wanang'atana sana mpaka kuuana, nimeshawapa damu iliokaushwa,chokaa,OCT, na pia mara nyingi mlo wao haukosi dagaa, nini tiba?
2.naomba ufafanuzi pale uliposema kuku mdogo anayetaga anahitaji 4.5 kg kwa muda wa miezi miwili, je hii kg 4.5kg ni kwa siku moja? kama ndio mbona mimi mwenyewe siwezi kula kg4.5 per day?
Mkuu tatizo linalosumbua kuku wako ni avitaminosis ambayo ni upungufu wa vitamini katika mwili....Wakuu kuku wangu wana hali mbaya wanatokewa vidonda kichwani macho yanafumba hawaoni wanakosa nguvu ni kuku wa kienyeji wapo hamsini wote wakubwa wamefikisha miezi saba nifanyeje hapa akili imevurugika kabisa nmewaunua lak sita wote
![]()
Great.... be blessed mkuuNami naomba nichangie kiduchu ingawa mleta uzi amajibu kwaa usahihi na kwa ufupi unaoleweka.
Kung'atana kitaalamu wanaita "cannibalism" hii ni moja ya tabia mbaya kwa kuku wanaofugwa muda mwingi wakiwa ndani.
Hii hutokana na baadhi ya haya yafuatayo
1. Kukosa madini lishe kama fosiforasi na kalisiam, madini haya hupatikani kwa wingi kwenye unga wa mifupa na chokaa ya mifugo.
2. Msongo(Stress), hii hutokana na Msongamano ama mrundikano wa kuku (kuku wengi eneo dogo).
3. Kuweka kuku wa umri tofauti ndani ya banda moja, hii usababisha kuku wakubwa kupiga na kuwadonoa kuku wadogo.
Tiba na kinga.
1. Kuwapa chakula chenye uwiano sahihi wa chokaa na unga wa mifupa.
2. Kuwaongezea nafasi ili wawe na eneo pana la kucheza kuepusha kusongamana.
3. Wapatie mchanganyiko wa maji na vitamini(Anti-stress) kwa kipindi kilichoelekezwa katika mfuko ama kibandiko.
3. Kuwafungia majani ama mboga za majani ili wapate sehemu ya kupunguzia msongo kwa kula majani yaliyo ning'inia.
4. Kuwatenga walioathirika haraka sana maana kuku anapoona damu ile sehemu itashambuliwa sana, kwa hiyo unapomtenga muathirika unaokoa maisha yake.
5. Mpe huduma ya kwanza kuku aliyeathirika kwa kumpaka "iodine tincture" na kumpa mchanganyiko wa maji na vitamini (kipunguza msongo ama "anti-stress").
Kwa kuongezea,Mkuu tatizo linalosumbua kuku wako ni avitaminosis ambayo ni upungufu wa vitamini katika mwili....
Hivyo basi unashauria kuwapa kuku wako majani au mchicha katika kipindi cha kiangazi hii ni baada ya kuwapa chakula chao cha kila siku....
Pili kama majani au majani ya kijani yamekosekana hakikisha unawachanganyia vitamini ambazo utanunua katika maduka ya mifugo na amini tatizo lako litakuwa solved
Karibu sanaa mkuu
Great.... but sidhani kama yaweza kuwa coryza hii mkuuKwa kuongezea,
Wapake ayodini kwa ajili ya kuwaisha uponaji wa vidonda na kuzuia vimelea vingine kupenya.
Kuongozea na mboga za majani ni vyema pia kama utapata Mchanganyiko wa Vitamin (Dukani) hasa zile zenye Kiwango kikubwa cha vitamini A ukatumia.
Wacheki pia kama wanamafua, funua kope ucheki kama kuna utando mweupe...
(Kama majibu yako yatakua ni chanya tumia pia na Dawa za mafua na wasafishe macho)