Fahamu kama namba yako ya NIDA ilitumika kusajili laini za simu usizozifahamu kwa mawakala wajanja wa kusajili laini

Fahamu kama namba yako ya NIDA ilitumika kusajili laini za simu usizozifahamu kwa mawakala wajanja wa kusajili laini

Hellow, naomba kuuliza coz na mm ni muhanga,
Je, nikitumia option ya remove, inamaana namba ake unafungwa tena. Or hadi nikachome Customer care

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kuzifuta ila hakikisho nenda kwenye shop ya huo mtandao Unaweza kuta jamaa alotumia line kwa ajili yako ameshaifanyia utapeli.
 
tuma hela kwenye namba hii jina litakuja Big Soap. ni kamchezo kanacho endelea. mawakala wa usajiri wanapoteza uaminifu. yaani wanakwambia weka tena kidole (finger print) kumbe ushasajirishwa line bila kujua. piga *106# akiki nambazi zilizosajiliwa na kitambulisho chako. msaidie ndugu zako na watu wa karibu kuhakiki. asante
 
N

Nenda shop yao ukazifunge
 
Msaada. Kama unataka kuangalia namba Zote za mitandao Zote zilizosajiliwa na Nida yangu nafanyaje. Km MTU kasajili na halotel na Nida yangu Mimi Sina halotel laini kuhakiki nitajuaje?
 
Msaada. Kama unataka kuangalia namba Zote za mitandao Zote zilizosajiliwa na Nida yangu nafanyaje. Km MTU kasajili na halotel na Nida yangu Mimi Sina halotel laini kuhakiki nitajuaje?
Piga,*106# kisha chagua ANGALIA NAMBA ZILIZOSAJILIWA MITANDAO YOTE
 
Msaada. Kama unataka kuangalia namba Zote za mitandao Zote zilizosajiliwa na Nida yangu nafanyaje. Km MTU kasajili na halotel na Nida yangu Mimi Sina halotel laini kuhakiki nitajuaje?
Piga *106#
Then kuna Sehemu wanakupa option ya kuondoa hiyo namba
 
Wasalaam.

Ili kujua unabonyeza *106# kisha usajili wa NIDA (Utaingiza NIDA ID yako), baada ya hapo zitakuja namba zote zilizosajiliwa kwa ID yako ya NIDA. Kama namba haijui siyo yako maana yake wakala (agent) alifanya ujanja kutumia ID yako kusajili line nyingine.

Ukishaona kwenye list namba haijui basi unaenda kwenye shop iliyokaribu nawe una claim, then customer care anakuambia uweke finger print kisha hiyo namba inafutwa.

Kutokana na watu wengi kutokuwa na NIDA, mawakala wengi walitumia ujanjaujanja wa kusajili line kwa kutumia ID ya mtu mwingine na kuuza hizo line kati ya elfu 5 hadi elfu 20, inategemea watakavyokuona na uhitaji wako.

Mawakala wanafanyaje ujanja? Ukienda kusajili line yako atakwambia weka dole gumba lako baada ya dakika atakwambia network inasumbua hebu ingiza tena, ukifanya hivyo basi hapo jua umeumia, ile ya kwanza amesajili line ya mtu mwingine na ya pili anasajili line yako, kama haujui hiyo mbinu hauwezi kumstukia maana wapo very smart.

Kwahiyo, wote mlionunua line kwa mawakala zilizosajiliwa kwa NIDA maarufu kama Take Away, mjiandae kisaikolojia.

Utabonyeza mbili halafu utaweka namba yako ya NIDA, mwisho utatumiwa SMS ya namba zako zote ulizozisajili kama kuna namba haujaisajili utaenda kwenye shop yoyote ya kampuni ya simu ambayo wewe ni mteja wao halafu utapewa fomu ya ku-remove namba ambazo huzitambui.

Jumanne NJEMA.
Shukurani sana mkuu
 
Back
Top Bottom