SWALI: Je virusi vya corona vitafika Tanzania?
Jibu: Ndiyo, haionekani njia ya kuvizuia
Swali: Je tutakufa sote?
Jibu: Mpendwa, sote tunakufa siku moja, lakini si shauri ya virusi hivi. Maana wengi wanaweza kuambukizwa, na wengi wataona matatizo kidogo kama mafua, wengine hawatasikia kitu. Ila wengine (labda 10-20 kati ya 100) watagonjeka, na wengine kati ya hao watagonjeka sana, na 2-3 wanaweza kufa. Asilimia 98 -97 tutaishi – hadi kufa anyway.
Swali: Je tufanye nini?
Jibu: Tunza akili yako na usianze kuogopaogopa. Mara habari za kufika kwa virusi Tanzania zinapatikana, tumia busara, fuata hatua zifuatazo:
• kunawa mikono mara kwa mara kwa angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni. Ukiwa nayo tumia dawa yenye alikoholi (si chini ya asilimia 60) kusafisha mikono.
• usiguse macho, pua na midomo kwa mikono kama hujanawa
• epukana kuwa karibu sana na wagonjwa
• wakati ugonjwa unazuru katika nchi ulipo, epukana kuwasalimu wengine kwa kushika mikono
• kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga chako ni dhaifu katika hali hii, uko hatarini zaidi)
• tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya choo / toilet paper) uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
• safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (vikiwa pamoja na kikombe, deski, simu yako); kama unayo, tumia dawa la alikoholi (spirit – si konyagi!), lowesha karatasi nayo, futa, tupa