Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Mark Francis

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
605
Reaction score
310

Nimefungua biashara ya Mgahawa sehemu flani hapa jijini Dar es Salaam, nimeweka wafanya kazi 3; mmoja kwa ajili ya chips na wa2 kwa ajili ya chakula kwa sababu biashara yenyewe bado changa. Eneo ambalo nafanyia biashara lina population kubwa na halina competition kubwa sana. Mimi napitia mida ya jioni kucheki jinsi biashara inavyoendela na kuhakikisha hesabu zinaenda vizuri.

Tatizo mpaka sa hizi ni zaidi ya mwezi na sioni faida yoyote zaidi ya kuwalipa wafanyakazi wangu kwa kipato changu kidogo ambacho ninakipata kwenye kaajira kangu kwa mhindi. Naombeni mnisaidie yafuatayo;
  1. Nifanyaje ili niweke kuvutia wateja zaidi bila kutumia kiasi kikubwa cha fedha?
  2. Nifanyaje ili niweze kupata faida kubwa, yaani kuwa na matumizi kidogo na mauzo mengi?
  3. Nifanyeje ili kuwabana wafanyakzi wangu waisimamie biashara vizuri na kupata faida?
NAOMBENI USHAURI WENU

WADAU WANAOHITAJI MUONGOZO KATIKA BIASHARA HII
Habari wadau,

Napenda kuuliza hivi: Kuuza au biashara ya chakula inalipa au?

Naombeni mawazo yenu.
Habarini,
Kwa wanaofahamu na wenye uelewa na hii kitu naombeni mchanganuo wa hii biashara ya chakula kwa mgahawa wa kawaida, inatakiwa uwe na shilingi ngapi?
Habari zenu ndgugu zangu,

Mimi ni mgeni katika ukurasa huu naomba kufahamishwa ni njia gani na taratibu gani na gharama za kuanzisha au kufungua cafe nzuri ya wastani.

Msaada wenu tafadhali.



MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII

ZAIDI, SOMA:

Jinsi ya kufanikiwa kibiashara kwa kufungua mgahawa

Mgahawa ni wazo zuri kwa kuanza mradi wa biashara, Mara baada ya kujenga na kupata imani, mgahawa utawavutia wateja bila matatizo yoyote. Lakini, kabla ya kuamua kufungua mgahawa unatakiwa kuzingatia mambo kadhaa kama vile kujenga, masuala ya leseni na kisheria pamoja na mahitaji mbalimbali yaliyowekwa na mamlaka za afya mfano TFDA kwa Tanzania. Baada ya kujaza mahitaji yote, unaweza kuanza mradi wako wa biashara katika utulivu wa muda mrefu na kwa umakini kuhakikisha unapata mafanikio.

1 -. Kama miradi mingine yoyote, eneo la biashara ni kipengele muhimu kwa ajili ya mgahawa. Chagua sehemu ambayo ni katika eneo la msongamano ambapo kuna mzunguko wa mara kwa mara na idadi kubwa ya watu.. lazima pia kuwa na maegesho mazuri, ambayo itaruhusu watu kuhifadhia vinywaji vichache na vitafunwa

2 -. Huduma za Mgahawa zitolewe katika njia ya kisasa, ili kuvutia watu kutembelea na kuchunguza yaliyomo ndani yake sababu mgahawa utakuwa ukijitangaza wenyewe kwa uzuri wa huduma zake (wahudumu wakarimu, waelewa na wasio wepesi wa kuonesha kuudhika). Aina ya vyakula na vinywaji ni lazima izingatie uhitaji wa wateja na mchanganyiko wake uwe wa kisasa. Ni lazima pia kuwa na nafasi ya kutosha katika mgahawa wako ili kutoa nafasi inayoweza kuenea wageni zaidi wakati wa masaa ya biashara. Unaweza kuweka/kuongeza eneo la bar sehemu ya wazi kwa ajili ya vinywaji ili kutoa nafasi ya kutosha kwa wateja wanaohitaji vinywaji pekee.

3 -. Kama utahitaji kuuza vileo katika bar, lazima kupata vibali muhimu kwa ajili ya matumizi ya pombe kabla ya kufungua . Pamoja na taratibu za kisheria, unatakiwa kuwa makini na mambo mengine kuhusiana na taratibu za afya. Ni muhimu kujijengea uaminifu na kulinda afya ya wateja wako pia kwa kuzingatia maelekezo yote yanayoamriwa na idara ya afya kamavile kuhakikisha jiko na eneo la kuhifadhi chakula viko katika mahali maalum na katika hali ya usafi. Pia vyombo vinavyotumika na kila kitu kinachohusika katika mgahawa wako view katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja na usafi binafsi wa wahudumu.

4 - Daima angalia mshindani wako analenga kufanya nini au amefanya nini ili wewe ufanye ubunifu wa tofauti kuwavuta wateja wengi kwako. Kabla ya ufunguzi wa mgahawa pia ni muhimu kufahamu washindani wa karibu ambao utapambana nao kibiashara kwa ajili ya kuanzisha mgahawa wako katika namna mpya. Tathmini kabisa faida na hasara katika kusimamia kazi,maamuzi na utekelezaji wa mikakati ya biashara.

5 -. Ni vyema kuchukua uongozi na ushauri kutoka kwa mtu ambaye tayari ana uzoefu katika kuendesha mgahawa wenye mafanikio au café. Mara nyingi mshindani wako hawezi kukupa ushauri utakaokufaa. Watu ambao wana uzoefu wa kufanya kazi na migahawa watakwambia baadhi ya vidokezo muhimu na vitendo kwa ajili ya kuanzisha biashara ambayo itakuwa na mchakato rahisi sana. Kama wewe utaendelea sana zaidi na kupata maarifa ya kutosha unaweza kuwa hata mshauri biashara kwa watu wengine.

Chanzo: inamotoselfemployment
 
Mkuu biashara ya mgahawa inaendana na vitu vifuatavyo.

  • Location
  • Usafi
  • Chakula
  • Wahudumu
  • Bei
  • Uniqueness/ Je, kwenye mgahawa wako kuna kitu cha ziada
1. Lazima kuwe na chakula chaenye ubora na si bora chakula
2. Location yake lazima iwenzuri na ya kuingilika na wateja.
3. Wahudumu lazima wawe na kauri nzuri na lazima wawe wasafi mda wote
4. Hotel lazima iwe safi time zote na muda ambao wateja unakuta wamepungua au kukata wanapitisha dekio ili kuweka mazingira ya usafi

Kuhusu kuto pata faida labda nikujibu ifuatavyo.
1. Inategemeana na bei ya msosi wako. Je umeweka bei ya kuvutia tu wateja bila kuajali kama kuna profiti?
2 au umeweka bei ya juu kiasi kwamba wateja wanashindwa kuingia?
angalia bei yako kama ina meet cost na kutengeneza profit kidogo
3. hao wahudumu wako je niwaminifu kiasi gani? Je ni ndugu zako wa karibu sana? But kwenye pesa hakuna cha undugu hata mke wako anaweza kuchakachua tu.
  • jaribu kuspend siku nzima pale na ucheki wateja wanao ingia ni kiasi gani na pesa inayo patikana ni kiasi gani.
  • then hapo utaweza fanya analysisi ya kujua kama huwa wanakuibia au
nb: Biashara ya hotel ni moja ya biashara ambazo kwa kweli huwa hazina hasara kubwa na ni moja ya business ambazo huwa zinatengeneza profit kwa haraka sana ukilinganisha na biashara za duka
 
Hongera mkuu biashara ya hoteli na chakula inalipa sana manake mtu yeyote lazima ale na ashibe kwa hiyo sio biashara ya kukuingiza hasara.

Sasa ushauri fanya hivii chukua likizo huko kazini kwako siku 30, nenda kasimamie mwenyewe kwenye hizo siku hakikisha unaweka hesabu vizuri kama chips agalia guia la viazi umenunua kwa kiasi gani umeliuza kwa mda gani umepata faida ya kiasi gani na unapata faida ya kiasi gani hapo utaweza kuielewa vizuri biashara yako kuna viti vingi vya kujua, kama usafi, ugha wanayotumia watu wako huo,pia unasikiliza mawazo ya wateja kwa kweli wateja huaga wana bonge ya mawazo ambayo ni ya manufaa sana.
 
Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua?

Je, bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.
 
Pamoja na yote waliyoongea wachangiaji waliotangulia, hakikisha chakula kinachopikwa ni kizuri kwa maana ya taste.
Jaribu kuangalia aina ya wateja ulionao na upange bei kuzingatia vipato vyao.

Unaweza kutenga sehemu mbili, moja ikawa na special foods ukaset price yake na sehemu nyingine ikawa na vyakula vya kawaida na bei yake.

Pata muda ukusanye maoni ya wateja na wape trainning ya customer care hao wahudumu wako.
NB: biashara nyingi mwanzo huwa ni ngumu na huna budi kukubali hasara.
 
1. Usisahau kulipa kodi TRA, na nyinginezo
2. BIASHARA KAULI hao wahudumu kama hawajui kuuza maneno walah mtume huuzi!
3. Kwenye biashara kuna ushirikina sana (i) utafute kimzizi pemba, bagamoyo, sumbawanga, nk kikusaidie kuvuta wateja

AU (ii)MAOMBI OMBEA BIASHARA YAKO ITAFANIKIWA.

NB: HAPA MJINI CHUMA ULETE NI NYINGI SANA ZINGATIA NO 3 (ii)
 

Useful contribution. Excellent!!!
 
Malila hebu eleza zaidi hapo kwenye RED
 
Mkuu nimependa hapo kwenye blue-I salute you-JF ,KUNA VICHWA VYA MAANA KWELI HUMU!,sikulijua hili![QUOTE=Malila;2249518]Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua? Je bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.[/QUOTE]
 

Kama alivyoshauri jamaa mmoja hapo chiini au juu. Inabidi uchukue likizo kama yamiezi 2, hatakama sio ya malipo.
Simamia mwenyewe kuanzia unaponunua sukari, chumvi mpaka vyakula na vyombo vya hapo mgahawani.

Hapo utajua kuwa hio boashara inalipa au hailipi, na kama inalipa basi kwa siku ni kiasi gani, na ni chai ya namna gani wateja wanaipenda au chakula gani cha mchana au siku wateja ndio wanunua sana.

Kuanzisha biashara ni bomba ila unatakiwa ujue hio business inaingiza roughly kiasi gani kwa siku, hapo itakua rahisi kuwabana wasimamizi kama kuna short.
 
[/QUOTE]hiyo cocept kailezea vizuri robert kiyosaki ktk poo dad, rich dad 2, the cashflow quadrant. Napendekeza ukisome
 
Ndugu unatakiwa ugeuze baadhi ya vyakula na vinywaji au uongozee baadhi yake ili upate wateja zaidi na pia ni uzuri kutizama migahawa ilioko kabli yako wanatumia mbinu gani ili kupasi kuchukuwa ujuzi wao ila pia pengine sehemu wenyewe inawezekana kuwa si ya kuvutia kabisa kwa hivyo ndugu nakushauri ufanye mabadilisho ili uweze kuendelea na biashara yako
 
Sema maeneo tuweze kukusaidia vizuri. Kuna maeneo mengine yanaitaji vyakula vizuri, maeneo mengine yanaitaji matangazo, maeneo mengine kuna aina ya vyakula wanavyopenda.
 
Tunaposema biashara ni kununua sio kuuza,tuna maana kuwa bei ya soko inajulikana kwa hiyo ni lazima upate faida kabla hujauza bidhaa zako kwa kununua kwa bei nzuri/chini kiasi toka ktk chanzo(supplier mzuri).

Mfano, Kilo moja ya mchele ni Tsh 1600/ soko la Kariakoo na mchele huo huo ni Tsh 1350/ pale Tandika na wewe mgahawa wako uko Buguruni, yaani nauli ya daladala ni sawa. Tayari huyu wa Tandika ameshaokoa Tsh 250/ kwa kila kilo atakayo nunua. Kwa hiyo mkija Buguruni ktk migahawa yenu,mnaanza kutafuta faida kwa kuuza wali ktk soko kwa bei moja,mwenzio ana Tsh 250/ aliyoiokoa ktk manunuzi na wewe una Tsh 0/.

Kwa hiyo utaona huyu wa Kariakoo lazima apunguze kipimo cha sahani moja au aongeze ufundi ktk mapishi, sasa huyu wa pili anachofanya ni kuongeza ukubwa wa kipimo cha sahani kidogo na anaimarisha mapishi, ni lazima apate wateja wengi kila siku bila kulaza chakula, mwisho anapata muda wa kutosha kufanya maandalizi ya kesho na kupumzika, kufanya usafi wa eneo lake la biashara nk.

Siku moja nenda Kitunda/Kivule/Majohe asubuhi sana uone vijana wa mjini wanachofanya?
 
Helo wadau naomba ushauri wenu niko hapa dar nina kama mil 1 nataka kufungua biashara ya mama lishe, nimwajili mtu wa kupika. Je, itanilipa?
 
Nimekuwa nikiwashauri wajasiriamali wengi kwamba furaha yako katika biashara isiwe katika fedha/faida unazopata; lazima kuwe ni jambo la zaidi linalokusukuma kuanzisha biashara. Fursa yeyote ya biashara hutokana na uhitaji wa huduma/bidhaa katika eneo husika, hivyo basi biashara yako inapaswa kulenga au kufikia zaidi jamii inayokuzunguka kulinga na uhitaji wao.

Kila biashara inalipa, bali hutegemeana na uhitaji uliopo katika eneo husika, ikiwa umeona uhitaji wa kuwepo kwa huduma hiyo katika eneo husika basi utapata faida tu; bali kama huduma hiyo inapatikana katika eneo husika na unahitaji kuongeza ushindani tu, inabidi ujipange vizuri.
 
Songa mbele na kazi maana biashara ya chakula lazima watu wale tu. Ila kama alivyoshauri Mgombezi angalia uhitaji wa huduma katika eneo husika au soko la bidhaa yako. Lakini pia kumbuka suala la chakula lazima liambatane na usafi wa hali ya juu, yaani mazingira pamoja na vifaa utakavyotumia.

Pia usisahau kumwomba Mungu akusaidie na kuibariki biashara yako, ila fungu la KUMI umtolee usimwibie. Baada ya hapo mafanikio ni lazima tu.
 
Biashara hyo nzuri mtaji ulionao usikupe hofu ili uweze kucompete vizur biashara hyo inahitaji mambo kadha yawe sawasawa.

1. Usafi unahitajika wa hali ya juu (mazingira ya mgahawa,wahudumu, vyombo na upishi)
2. Kauli nzuri
3. Ubunifu katika upishi
4. Weka huduma za ziada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…