Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Ni ngumu kuanzisha biashara ukaiacha ijiendeshe. Jua kwamba unaemwajil nae anandoto za utajir kama zako, tafuta mda hata wa wiki, either mkeo au ndugu yako afanye evaluation hapo.

But safi, quantity & quality ya chakula na customer care ni baadhi ya uchawi wa biashara hiyo.
 
Nimefungua biashara ya Mgahawa sehemu flani hapa mjini DSM, nimeweka wafanya kazi 3; mmoja kwa ajili ya chips na wa2 kwa ajili ya chakula kwa sababu biashara yenyewe bado changa. Eneo ambalo nafanyia biashara lina population kubwa na halina competition kubwa sana. Mimi napitia mida ya jioni kucheki jinsi biashara inavyoendela na kuhakikisha hesabu zinaenda vizuri.

Tatizo mpaka sa hizi ni zaidi ya mwezi na sioni faida yoyote zaid ya kuwalipa wafanyakazi wangu kwa kipato changu kidogo ambacho ninakipata kwenye kaajira kangu kwa mhindi. Naombeni mnisaidie yafuatayo;
  1. Nifanyaje ili niweke kuvutia wateja zaidi bila kutumia kiasi kikubwa cha fedha?
  2. Nifanyaje ili niweze kupata faida kubwa, yani kuwa na matumizi kidogo na mauzo mengi?
  3. Nifanyeje ili kuwabana wafanyakzi wngu waisimamie biashara vizuri na kupata faida?
NAOMBENI USHAURI WENU.

Ndugu hebu lete mrejesho basi.
 
Mojawapo ya sababu ya wahindi kufanikiwa sana kwenye biashara ni kwamba wahindi huwa wanamchukulia kila mtu wanayemuajiri kuwa ni potential "mwizi". Hata siku moja mhindi hamuamini mfanyakazi wake kwenye pesa.

Ukiwa unaenda jioni tu tayari unawapa mwanya wafanyakazi wako wa kujifanyia watakavyo. Wanaweza wasikuibie pesa lakini wakahonga chakula, kufanya uvivu, kutokutumia lugha nzuri kwa wateja etc.

Be there yourself to set the standards you require. Kama umeshindwa kabisa kufanya hivyo basi show up unexpectedly, usiwe na muda maalum.

Define kundi unalotaka liwe wateja wako halafu wapikie chakula cha bei na flavour zinazoendana na matakwa yao.

Hongera sana kwa kutoa ajira.

Kitendo cha kuanza ni uthibitisho tosha kuwa unaweza. Just get closer to your business and "spy" your employees.

Teua kiongozi kati yao, halafu mwingine ongea naye chamber kuwa yeye ni "spy" wako kwa wengine - be ready to reward his work. Watatu aliyebaki tafuta mbinu ajione ana bidii na thamani kuliko wengine. That way unapunguza uwezekano wa wao kushirikiana kukuibia au kufanya uzembe.

Wewe mtu ni hatari sana

Naona hapo mwisho umedondosha nondo hatari sana jinsi ya kuroga biashara yako mwenyewe
I SALUTE YOU mkuu ZeMarcopolo

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
Siku zote katika biashara kuna vitu vya kuzingatia hasa 1.Quality 2. Location 3. Price ya chakula. Naomba niongelee issue ya quality. Hapa zingatiaa quality ya chakula pia usafi wa wafanya kazi.chakula kinawezaa kuwa kizuri but wafanya kazi wachafu, Nguo hazina ubora walizo vaa.

Pia kuna kitu kinaitwa customer relationship management. Ni namna gani wafanya kazi wako wanazungumzaa na wateja.mfano mtu anagiza chakula then mfanyakazi anajibu kwa kinunaa, hapo wateja hawarud na marejesho hupunguaa.

Nakusihi angalia ubora wa chakula, angalia bei ulioweka inaendana na watu wa eneo hilo, angalia uzungumzaji wa wafanya kazi na wateja, angalia usafi wa wafanya kazi.
 
Hawa madogo wanakwenda alfajili sana kukusanya kuku waliokufa mabandani na kuwaandaa vizuri. Kisha wanaondoka na hao vibudu mpaka town Ktk migahawa na kuuza kwa bei ya kutupa. Sisi tunafakamia kwa bei nafuu. Uliza wafugaji aw kitunda wakupe Siri hii Kama kuna kuku wanafukiwa huko wakifa.

Aiseeeh!
 
Mojawapo ya sababu ya wahindi kufanikiwa sana kwenye biashara ni kwamba wahindi huwa wanamchukulia kila mtu wanayemuajiri kuwa ni potential "mwizi". Hata siku moja mhindi hamuamini mfanyakazi wake kwenye pesa.

Ukiwa unaenda jioni tu tayari unawapa mwanya wafanyakazi wako wa kujifanyia watakavyo. Wanaweza wasikuibie pesa lakini wakahonga chakula, kufanya uvivu, kutokutumia lugha nzuri kwa wateja etc.

Be there yourself to set the standards you require. Kama umeshindwa kabisa kufanya hivyo basi show up unexpectedly, usiwe na muda maalum.

Define kundi unalotaka liwe wateja wako halafu wapikie chakula cha bei na flavour zinazoendana na matakwa yao.

Hongera sana kwa kutoa ajira.

Kitendo cha kuanza ni uthibitisho tosha kuwa unaweza. Just get closer to your business and "spy" your employees.

Teua kiongozi kati yao, halafu mwingine ongea naye chamber kuwa yeye ni "spy" wako kwa wengine - be ready to reward his work. Watatu aliyebaki tafuta mbinu ajione ana bidii na thamani kuliko wengine. That way unapunguza uwezekano wa wao kushirikiana kukuibia au kufanya uzembe.

Na kama kampuni ni kubwa unafanyaje? Ukubwa kama wa McDonalds?
 
Na kama kampuni ni kubwa unafanyaje? Ukubwa kama wa McDonalds?

McDonald's ni chain. Migahawa yayao ina wamiliki wengi sio yote iko chini ya management moja.

Hata hivyo, kampuni kubwa inakuwa na resources za kutosha kuwa na professional administration.
 
Nataka fungua biashara ya restaurant lakini nataka muweka mtu ndo awe manager wa pale wakati huohuo awe ni mfanyakazi.

Biashara itauza vyakula
1. Asubui vitafunwa aina zote na chai/maziwa
2. Mchana milo takriban 4 au 5
3. Usiku Milo mitatu pamoja na chips
4. Vinywaji vya aina zote

Naombeni ushari kulingana na maswali ninayo jiuliza.

1. 5mil itatosha?
2. Business locatio (mimi mkazi wa dsm,mbagala)
3. Who is manager (specifications of manager)?
4. Number of workers?
5. Business monitoring method?
6. Daily correction amount

Nisaidieni mawazo yenu.
 
Naomba niwe meneja, namba 3 hapo kwenye maswali unayojiuliza nimepajibu!

Namba 5, tutatumia njia ya kila kiendacho kwa mteja kiandikwe.
Namba 6, unamaanisha Makusanyo au Masahihisho?( Correction / Collection).
Niko siriaz ndugu, sina kazi!
 
Naomba niwe meneja, namba 3 hapo kwenye maswali unayojiuliza nimepajibu!

Namba 5, tutatumia njia ya kila kiendacho kwa mteja kiandikwe.
Namba 6, unamaanisha Makusanyo au Masahihisho? (Correction / Collection).
Niko siriaz ndugu, sina kazi!
Nilimaabisha collection
 
Hakikisha anakaa mkeo au ndugu yako unae muamini jaribu kununua viti hasa vitafunwa kuliko kupika mwenyewe
watu watatu wanatosha na mkeo wa nne.
 
Hakikisha anakaa mkeo au ndugu yako unae muamini jaribu kununua viti hasa vitafunwa kuliko kupika mwenyewe watu watatu wanatosha na mkeo wa nne.

Asisahau wapishi makini wenye kujua taste ya chakula na viungo maridhawa manake hapo ndio ulipo moyo wa biashara hiyo ukiacha usafi na mazingira rafiki kwa wateja.

Akifuata ushauri wako na huu biashara ya chakula hakitupi mtu hata siku moja.
 
Wapishi wazuri lazima aende kuiba restaurant za Wahindi, Wahindi hawawalipi vizuri.
 
1. Inategemeana na location, location nyingine zinaweza kukugharimu pesa nyingi zaidi ya hiyo.

Je, eneo ni lako au utakodi/kua mpangaji wa eneo la mtu?
Je, hilo eneo liko tayari kwa biashara au bado na litahitaji ukarabati kuliweka liendane na mazingira ya mgahawa?
Je, samani zipo tayari au unahitaji kununua mpya zako?

Hayo maswali machache yatatoa majibu kama hiyo 5m inatosha au la.

2. Manager inatgemeana, unataka ufanye biashara wewe mwenyew au umkodishe mtu awe anakulipa wewe daily?
Kama unatoa wewe mtaji kwa kuanzia muweke mtu unaemuamini kiasi ili awe anakusanya wewe jioni unapokea makusanyo unatoa matumizi na kufanya manunuzi kisha unatenga faida.

Au unaweza kumpa mtaji ukampa malengo ya pesa atakayokua anakulipa kila siku kwa hiyo anakua na ka semi autonomous kial kitu anafanya yeye,yaani kama daladala,bosi unachotaka ni mahesabu yako tu.

3. Inategemeana na ukubwa wa eneo na idadi ya wateja,kukiwa na influx ya wateja lazima uwe na idadi kubwa ya wafanyakazi kuendana na mahitaji mteja asifike akakaa dakika 5 hajasikilizwa wala kupewa huduma.

Maswali mengine yanategemea na maelezo yangu hapo juu.

Kua na mgahawa mzuri ni pamoja na kua na wapishi wazuri, uwe wa pekee na chakula chako kiwe na ladha ya pekee,biashara ya mgahawa inahitaji sana kujitofautisha, usinunue chakula ukauza,pika mwenyewe.

Nunua vitu kama vitumbua,mandazihalf cake,donalti,chapati pika mwenyewe au uwe unanunua kwa mpishi yule yule kila siku. Nyama na chakula kingine kama wali,ugali,sammaki,supu ya kuku uwe na wapishi wako mwenyewe.

Nunua samani za kisasa nzuri,viti vya kili na pepsi na koka achana navyo, nenda cello pale keko kuna viti vizuri na vya kisasa vitakavyokufanya uonekane wa tofauti.

Zingatia usafi ,huduma nzuri kwa wateja, kauli nzuri, chakula kiwe tayari kwa wakati, sio sa 6 ndio wanabadnika sufuria la ugali na wali bado hujaiva, sa mbili chai bado utaishia kwenda kwa waganga na mwisho utafilisika.
 
Hakikisha anakaa mkeo au ndugu yako unae muamini
jaribu kununua viti hasa vitafunwa kuliko kupika mwenyewe
watu watatu wanatosha na mkeo wa nne...

Sorry, restaurant yake afu ananunua vitafunwa kwingine? Inalipa?
 
Ina save time na vitu vingi. Mfano unanunua maandazi kwa mtu andazi moja 150
we unauza andazi 300. Hapo faida yako ni 150 bila kununua unga wala kupoteza mda wa kupika.

Ooohhhh okay, thanks
 
Hii ni nzuri sana lakini inahitaji close supervision KWAUSHAURI NILIOSHAURIWA HII BIASHARA WA KUWEKWA MKEO AU MTU UNAYEMUAMINI SANA HAPO ATAKUSANYA KIHALALI NAWE UTAONA FAIDA
 
Back
Top Bottom