1. Inategemeana na location,location nyingine zinaweza kukugharimu pesa nyingi zaidi ya hiyo.
Je, eneo ni lako au utakodi/kua mpangaji wa eneo la mtu?
Je, hilo eneo liko tayari kwa biashara au bado na litahitaji ukarabati kuliweka liendane na mazingira ya mgahawa?
Je, samani zipo tayari au unahitaji kununua mpya zako?
Hayo maswali machache yatatoa majibu kama hiyo 5m inatosha au la.
2. Manager inatgemeana, unataka ufanye biashara wewe mwenyew au umkodishe mtu awe anakulipa wewe daily?
Kama unatoa wewe mtaji kwa kuanzia muweke mtu unaemuamini kiasi ili awe anakusanya wewe jioni unapokea makusanyo unatoa matumizi na kufanya manunuzi kisha unatenga faida.
Au unaweza kumpa mtaji ukampa malengo ya pesa atakayokua anakulipa kila siku kwa hiyo anakua na ka semi autonomous kial kitu anafanya yeye,yaani kama daladala,bosi unachotaka ni mahesabu yako tu.
3. Inategemeana na ukubwa wa eneo na idadi ya wateja,kukiwa na influx ya wateja lazima uwe na idadi kubwa ya wafanyakazi kuendana na mahitaji mteja asifike akakaa dakika 5 hajasikilizwa wala kupewa huduma.
Maswali mengine yanategemea na maelezo yangu hapo juu.
Kua na mgahawa mzuri ni pamoja na kua na wapishi wazuri,uwe wa pekee na chakula chako kiwe na ladha ya pekee,biashara ya mgahawa inahitaji sana kujitofautisha, usinunue chakula ukauza,pika mwenyewe.
Nunua vitu kama vitumbua,mandazihalf cake,donalti,chapati pika mwenyewe au uwe unanunua kwa mpishi yule yule kila siku. Nyama na chakula kingine kama wali,ugali,sammaki,supu ya kuku uwe na wapishi wako mwenyewe.
Nunua samani za kisasa nzuri,viti vya kili na pepsi na koka achana navyo, nenda cello pale keko kuna viti vizuri na vya kisasa vitakavyokufanya uonekane wa tofauti.
Zingatia usafi,huduma nzuri kwa wateja,kauli nzuri,chakula kiwe tayari kwa wakati,sio sa 6 ndio wanabadnika sufuria la ugali na wali bado hujaiva,sa mbili chai bado utaishia kwenda kwa waganga na mwisho utafilisika.