Rehema Kimwaga
New Member
- Jan 2, 2017
- 4
- 1
Nilitaman kuona feedback
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umesema kweli maana mpaka sasa sina mchango niliopata hahahaaUkitaka kuona wabongo tusivyojali mada za maana humu jf hii thread watajitokeza wachache tu kuongelea lakini kama zingekuwa stori za mambo ya ajabu ungekuwa na replies za kufa mtu.
Nimekukubali bure kabisa and i have taken this note.. Thank u na Mungu akubariki sanakabla ya kuwa na hivyo vitu fanya survey ya sehemu unayotaka kuwekeza hakikisha kuna mzunguko wa fedha au eneo lenye mkusanyiko wa watu kama stand ya daladala, vyuo, soko, makanisa makubwa(RC, Luth, etc), mikusanyiko ya taasisi na maeneo yote yenye makutano ya barabara zinazofanya hata bodaboda wajazane(boda boda ni indicator kubwa ya kuonyesha sehemu potential ya biashara hiyo), ukijirizisha andaa vifuatavyo
1. viti vya plastic 20
2. meza 5 za kulia chakula za plastic ni nzuri japo sio lazima hata mabenchi yaeza faa
3.jiko la gesi zuri la kilo 30
4.jiko ya mkaa 4 (jiko moja chapati, la maharage, la supu, la maji ya kunawa wateja) chai tumia jiko la gesi
5. flam pen na vyombo vya kukaangia (ya maandazi, ya chapati, ya kukaangia mayai, etc)
6. sufuria kubwa tatu(ugali, wali na maharage) na visufuria vidogo hata 7
7. stand ya kunawia wateja na ndoo yake
8. blenda ya kutengezea juice na kuponda nyanya
9. sahani na vijiko vya kulia chakula 50
10.stirer ya kuchanganyia changanyia bagia, mikate,etc
11. frizer kubwa (ndogo inafaa kishida shida), ukiwa na oven sio shida
12.case ya kubebea vyombo(usafi zaidi)
13. tengeneza sehemu nzuri ya kupikia(mazingira yanayohamasisha usafi)
14.tumia muda wako kujifunza hii shughuli tafuta wafanyakazi wenye ujuzi wa kupika aina tofauti za chakula na wasafi
15. ulizia mahali wanapika vyakula vitam hasa vya kipemba watu wengi wanapenda sana
16. kuwa mbunifu usiwe bahili wekeza fedha na walipe vizuri na kwa wakati wafanyakazi wako
KUMBUKA NI HATARI KUPIMA KINA CHA MAJI KWA KUTUMBUKIZA MIGUU YOTE - anza taratibu kwa kuweka vitu vidogo vidogo huku ukiusoma mchezo the more the response the more u invest boresha huduma na waelekez wafanyakazi wawe na majibu mazuri na kuvutia wateja slowly utakuta demand inakuwa kubwa kulko suply na hapo ndio unaongeza uwekezaji.
yangu ni hayo tu
Wakuu Kutokana na Changamoto ya ajira nataka nijiajiri kwa kufungua mgahawa mdogo
Ambao nataka niuze
Chai
Chapati
Wali &Ugali Nyama/mboga za majani
Supu
Msaada wa kimawazo Kwa Kilo 2 ya Mchele inaweza Kutoa sahani ngapi?/ Faida kiasi gani? Given price 1,200 na 1,500.
Kilo moja ya Unga wa Ngano inatoa Chapati ngapi? Na faida Kiasi gani kama market value ya Chapati ni 2500
NAJUA HILI JUKWAA NI LA SIASA NIMEPOST HUKU ILI NISAIDIWE MODERATORS NAOMBENI UKAE KWA MUDA. Kwani Majukwaa mengine nikipost kitu kinakaa hadi kinapotea mtu haja jibu.
Daah Asante kwa kunitoa gizaniKilo moja ya mchele inatoa sahani 5 hadi sita...na kilo ya ngano inatoa chapati hadi 16..sasa hapo angalia na soko la sehemu ya biashara yako kama ni uswahilini watu wanataka kushiba so unaweza toa sahani 4 tu za wali...hiyo biashara ni nzuri ukiwa na eneo zuri ila inahitaji usimamizi wako wa karibu
Hongera kwa kuchukua hatua, naamini utapiga pesa mpaka ushangae[/QUO Kwa hiyo umechangia nini?
Sawa rafiki, asante.Kwa Dodoma ni mtihani mno!! Kwani centre zote nzuri wameshawahi na ukitaka kuanzisha inabidi uwe mbunifu wa hali juuu
Asante kwa ushauri ndugu, appreciated!!Dodoma sehemu sahihi ni katikati ya mji ambapo kweli sehemu jamaa wengi wamechukua hivyo utakutana na kizingiti cha kupata sehemu bora ya kufanyia biashara yako but pia nikupe wazo unaweza kuweka mgahawa wako pembezoni mwa mji ukawa una supply lunch maofisini direct means unapaswa uwe na chakula bora then uende kwenye maofisi mbalimbali kuwaconvice uwe unawapelekea chakula packaging direct katika maofisi yao ili mchana wasiangaike kwenda kwenye migahawa hii njia unaweza kutusua but inahitaji uwe na vitendea kazi kama bodaboda au bajaji ili kuzunguka katika maofisi mbalimbali