Hongera kwa kufikiria kuanzidha biashara ya chakula ambayo ndio biashara inayolipa kwa wakatu huu kwani lazima ule kwa njia yoyote. ili uipatie hii biashara ziangatia ushauri ufuatao.
1. Mpishi. Lazima uwe na mpishi ambaye atapika vyakula vikuu kutoka na na sehemu husika na vyenye ladha ambayo hata mtu akiwa tegeta asijisikie vibaya kuja bunju kula plate ya ubwabwa kwa dada naniliu.
2.Viungo. Matumizi sahihi ya viungo na kwa mapishi gani? nilishaona sehemu wametia binzari ya mchuzi kwenye chai wakidhani tea masala. usipike chai ya rangi ukatia maji na majani hamna hata karafuu, maganda ya iliki, mdalasini wala mchaichai.
3.Usafi. Usafi wa mpishi, sehemu unayofanyia biashara, vyombo vya kupikia na vyombo vya kulia vyakula chakula. sio vyombo vichafu vinasuuzwa baada ya kuoshwa na kufanya rangi ya sahani imebadilika na unaweza ukajiongeza kwa kuvizuuza na maji ya uvuguvugu kuuwa bakteria.
4. Bei. kwa kuwa unaanza hakikisha bei zako ni rafiki pamoja na kuwa ladha ya chakula chako ni tofauti na banda la mama lishe.
5.Vitendea kazi. Lazima uwe na vitende akazi tofauti kama blenda, microwave, jiko la gesi dogo na mtungi wake, sio mteja anataka chakula anapata chakula cha baridi japo kuwa amekujamida ambayo sio ya kibiashara kivile.
6. Mahitaji. Hakikisha unakwenda kwenye masoko makuu kwa mahitaji na epukakununua mahitaji mengi sana kwa wakati mmoja kama samaki na kuku unawaweka kwnye friza mwezi mzima kwani huwa wana tabia ya kuwa na kaharufu ambacho hakikati hata umuunge vp. usinunue mchicha jumapili uje kupika ijumaa hapana, Jitahidi japo mara mbili kwa week sio mbaya uwe unakwenda mwenyewe marikiti.
6. Jiongeze. Usiuze chakula kikuu tu kama wali pilau, la ongeza najuice za viwandani na za kutengeneza mwenyewe matunda mengi ni kupata ujuzi tu, tengeneza salad baada ya kachumbari kwa kulia chakula, tengeneza pilipili za kupikana sio mteja atake pilipili umpe nzima akate mwenyewe, kwani kuna vitu vidogo vinavutia wateja sana na kama sio mjuzo sana ingia hata you tube utaona mapishi ya tofauti.
Kama kuna la ziada njoo PM nitakupa maujuzi zaidi.