Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Mtaji unatosha kabisa, issue hapo location.

Kama utapata sehemu nzuri ambayo chakula unaweza kuuza Tsh 2000, ongeza na vinywaji baridi, pia weka na kijana wa chips maana wadada wengi ndo chakula chao
Nashukuru
 
Kwa ufahamu wangu kikubwa ni usimamizi. Kuanzia manunuzi ie ubora wa materials, bei nk mpaka mauzo cz chakula hakina hesabu kamili inategemea idadi ya sahani (kama ndo kipimo). Bila hivyo andika maumivu.
 
Kwa ufahamu wangu kikubwa ni usimamizi. Kuanzia manunuzi ie ubora wa materials, bei nk mpaka mauzo cz chakula hakina hesabu kamili inategemea idadi ya sahani (kama ndo kipimo). Bila hivyo andika maumivu
Sawa
 
Biashara sio mtaji mkubwa.

Biashara ni kujua wanunuaji/wateja wako

Unaweza kua na huo mtaji lakini ukapigwa gepu na mama ntilie mwenye mtaji wa laki 1, MAMA ntilie akalaza kila siku faida ya 50k wewe ukalaza 20k ukijitahidi sana 30k

Muhimu ni Kujua wateja wako wanahitaji mtaji huo 5M Yawezekana wateja wako wanahitaji mtaji wa 1M tu..

Biashara ya CHAKULA/MGAHAWA ukitaka upige hela biashara yako iwe katika makundi haya mawili

1. Kawaida/chini: hapa ndio kuna kina mama ntilie na wauzaji wengine kibao wenye migahawa local na wateja wa kundi hili ndio wengi katika nchi yetu ya Tanzania.

2. Juu/kubwa:hapa kuna ma expert wanaoijua hii biashara so investment yao si ya kitoto toto na wateja wa kundi hili ni Madon wenye nchi yao wazeee wakufyatu hela..Mfano wa mgahawa wa kundi hili ni wa IRENE UWOYA "last minute"

Chagua kundi moja kati ya hayo mawili then FANYA BIASHARA.

Biashara ya mgahawa haina cha kuonja onja eti uweke mgahawa in a way LOCAL PEOPLE waingie na wale PRO LEVEL waingie HAMNAGA HIYO...lazima uchague aina ya wateja wako kama ni LOCAL au PRO then wape mamboz.

Ukisema uweke mgahawa haueleweki huu ni wa madon au raia wa kawaida aseee Utamaliza siku nzima umeuza sahani 1 ya chakula na soda mbili.

Mil.5 ni nyingi kwa mgahawa wa kawaida tena nyngi sanaaaaaaaa(hauihitaji hela nyingi ivyo) ila Mil.5 ni ndogo sana kwa mgahawa wa kundi B so kabla hujaendelea SEMA unawalenga wateja gani ktk hiyo biashara.
 
Sidhan kama upo serious. Vijana unaowatetea wanasmartphone za hadi laki tano,wananunua bando kila siku. Kwa kufupi inawezekana kuanza na mtaji mdogo. Mfano mimi nilifungua mgahawa kwa sh laki tisa tu na hapo nikiwa nmelipa kodi ya chumba miez 3 na kununua kila kitu. Na mgahawa huo ulinipatia sh. Elfu kumi kila siku ambayo nachukua sh 70,000/ kila jumapili hii ni sawa na sh. 280,000/ kwa mwezi hapo utashindwaje kulipa ada za shule kwa watoto? Shida ni kwamba wengi wetu hasa tuliajiriwa hizi biashara ndogo ndogo tunaziona ujinga.
Nikupe mfano mwingne kilo moja ya unga sh 1,400/ inatoa chapati za sh. 5,000/ zile chapati za 2 miatano so ukiuza supu na chai asubuh,mchana wali na ugali na ukakomaa mwenyewe baada ya miaka miwil unafungua hotel


Hii biashara naiwazia kila siku, mpaka hapa nishapata muelekeo! Pia nina frem mpya barabarani maeneo ya Mlandizi, je nifungue tigo pesa na sim au nianze na tg pesa kwanza kwani mtaji haujakuwa sana
 
Wadau naombeni mnisaidie mimi ni kijana wa chuo nimemaliza mwaka jana naombeni mtu anayeweza anisaidie eneo ambalo litakuwa ni zuri kiasi kwa kufungua mgahawa nipo Arusha na ninaitaji maeneo ya mjini au mushono msaada wa eneo mnisaidie ndugu zangu
 
SAA ingine ukute faida IPO ila wafanyakazi wanapiga panga..ndiyo shida ya biashara bongo
 
Habari nyingi sana wakuu

Mwaka ujao nina mipango mingi sana moja wapo ni hili la Kufungua MGAHAWA

Huu mgawahawa nataka niufanye wa kisasa sana lakini utakuwa na vyakula mchanganyiko yaani vya kizungu pamoja na kiasili...hapa kwenye vyakula vya asili kitu kikubwa nilichokiona ni ugali wa MUHOGO sisi wasambaa tunaita UGALI WA BADA sjui wengine mnauitaje?

Sajaju bajeti yake inaghalimu Sh ngapi kwa pesa ya Tanzania 🇹🇿..

Naombeni ushauri wenu wenye uzoefu wa hii biashara. Location Tanga Tanzania.
 
Kutokana na uwepo wa magonjwa mengi yanayosababishwa na Milo mibovu katika maisha ya kila siku....

Fungua natural Foods.... Ila zingatia Sana Location.. sio unaenda kuwauzia Natural food makondakta na wauza maji....

Nenda maeneo ya watariii unaweza kucapture market.

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Ukifanikiwa kufungua utasema. Siku nikiwa na trip tanga nipite kwako kula mijichakula
 
1,200,000.mkuu inatosha kabisa kwa kuanza at initial stage then biashara itakapokuwa na uhitaji kuongezeka ndio unaweza ukafanya more investment for your business.
 
1,200,000.mkuu inatosha kabisa kwa kuanza at initial stage then biashara itakapokuwa na uhitaji kuongezeka ndio unaweza ukafanya more investment for your business.
Mkuu shukran wacha nitembee nayo
 
Back
Top Bottom