Fahamu kuhusu Bunge Maalum la Katiba

Fahamu kuhusu Bunge Maalum la Katiba

kama ni hivyo mkuu Petro E.Mselewa naona kama kutakuwa na kasoro ktk hili,maana ktk vyuo vikuu mfano vya Tanzania tulitegemea tungepata wawakilishi ambao wangeweza kuwakilisha mawazo ya wanafunzi wa vyuo vikuu hadi shule za msingi,hii ingesaidia kupata maoni toka kwa vijana wasomi ambao ndio viongozi wa kesho.
maana naona wafanya kazi na mashirika ya dini wao wana wawakilishi wao
sijui wewe unalionaje hili ukiwa kama ni mtaalamu wa sheria

Kwani wanaoshiriki hawakuwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari au vyuo?
 
Kwani wanaoshiriki hawakuwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari au vyuo?

Umesha weka neno HAWAKUWA,tunaongelea hawa waliopo sasa mashuleni na mawazo yao yanatakiwa kubebwa na wawakilishi wao ktk bunge la katiba
 
Kwa hiyo wafungwa nao wanahitaji mwakilishi?

wazo zuri sana,kumbuka kuwa wafungwa nao ni binadamu na wanahaki ya msingi ya kutoa maoni ktk jambo lolote lile,si wote maisha yao yataishia jera,lakini hata wale waliopo huko wangetaka katiba iseme jambo juu ya wafungwa,kwa mfano haki ya kufanya tendo la ndoa kwa wafungwa waliokuwa na ndoa halali na mambo mengine mengi tu
 
Back
Top Bottom