kama ni hivyo mkuu Petro E.Mselewa naona kama kutakuwa na kasoro ktk hili,maana ktk vyuo vikuu mfano vya Tanzania tulitegemea tungepata wawakilishi ambao wangeweza kuwakilisha mawazo ya wanafunzi wa vyuo vikuu hadi shule za msingi,hii ingesaidia kupata maoni toka kwa vijana wasomi ambao ndio viongozi wa kesho.
maana naona wafanya kazi na mashirika ya dini wao wana wawakilishi wao
sijui wewe unalionaje hili ukiwa kama ni mtaalamu wa sheria
Kwani wanaoshiriki hawakuwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari au vyuo?
Umesha weka neno HAWAKUWA,tunaongelea hawa waliopo sasa mashuleni na mawazo yao yanatakiwa kubebwa na wawakilishi wao ktk bunge la katiba
Kwa hiyo wafungwa nao wanahitaji mwakilishi?