Fahamu kuhusu Bunge Maalum la Katiba

Fahamu kuhusu Bunge Maalum la Katiba

Ndugu Petro, bunge hilo litafanyika upande gani wa muungano? Zanzibar au Tanganyika? je kutakuwa na asilimia ya wabunge sawa kutoka pande zote za muungano?
Kwanza,kwa taarifa zilizopo,Bunge Maalum la Katiba litafanyika katika Ukumbi wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ndiyo kusema,litafanyika Tanzania Bara (Tanganyika).Pili,wajumbe kutoka Zanzibar hawatakuwa katika idadi sawa na wale wa Tanzania Bara.Imeshajidhihirisha hivyo katika uteuzi uliokwishafanywa
 
Maslahi ya wabunge wa Bunge maalum la Katiba yamekaaje? Je wale wabunge 166 wa kuteuliwa na Rais watalipwa sawa na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi?
Mkuu Sawia,bado maslahi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba hayako wazi.Yaweza kuwekwa bayana hapo baadaye kidogo.Lakini,kila mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba atapata maslahi sawa na mwenzake.Kwakuwa wote watakuwa na hadhi sawa isipokuwa labda kwa Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Makatibu wa Bunge
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom