Fahamu kuhusu Fao la Kukosa Ajira Tanzania (Unemployment Benefit)

Ni mbaya toka Magufuli amezileta ulitumika ubabe kwasababu wana madaraka, huwezi kumzuia mtu kuchukua 9M wakati wabunge wanazoa zaidi ya 250M, ni uhuni huu
Sababu kubwa inayofanya Unemployment benefits kulipwa hivyo, ni kulinda mwanachama asipoteze sifa ya kuwa pensioner.... Kuwa na wazee wengi tegemezi ni mzigo katika taifa lolote lile duniani.
 
Sababu kubwa inayofanya Unemployment benefits kulipwa hivyo, ni kulinda mwanachama asipoteze sifa ya kuwa pensioner.... Kuwa na wazee wengi tegemezi ni mzigo katika taifa lolote lile duniani.
Hii ni kwa stable job sio mikataba yetu ya miezi 6 au mwaka 1, unamaliza mkataba unakaa mtaani miaka kibao huna ajira wakati una pesa yako nssf watu wanatumia tu, hizi sheria ni za kipuuzi sana, hakuna wanacho linda zaidi kuzuia pesa na kutumia watakavyo
 
Sasa hapa tatizo ni upatikanaji wa ajira nyengine .... Ndio tatizo sio sheria...!?
 
Sasa hapa tatizo ni upatikanaji wa ajira nyengine .... Ndio tatizo sio sheria...!?
Tatizo ni sheria kwasababu mtu analipwa mshahara mdogo kusave ni ngumu, sasa anapomaliza kazi apewe nssf yake akafanye mambo yake badala ya kuendelea kusubiri ajira za kuunga unga, shida watunga sheria wao wanapata pesa watakavyo wanataka kuzuia masikini wasipate
 
Hapana, baada ya kulipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho, utasubiri miezi 18+ ukitafuta ajira, ukikosa ndio utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki
I Mean unalipwa kwa mkupuo au unalipwa kila mwezi 33.3% ndani ya miezi sita?
 
Ilichukua muda gani kulipwa mkuu baada ya kujaza fomu ya withdrawal benefits supplementary?
 
Elimu nzuri kwa Wahusika
 
Ilichukua muda gani kulipwa mkuu baada ya kujaza fomu ya withdrawal benefits supplementary?
Ndani ya miezi miwili, nilifungua mwezi wa 10 mpaka December katikati ikawa tayari, hiyo form uliyotaja (withdraw benefits.. ) sikujaza ila niliandika barua ya kuhamisha michango yangu niwe mcyangoaji wa hiari na kuomba kulipwa mafao yangu yote na nikaambatanisha viambatanisho vya "letter of service" na kiapo alafu nikasikilizia baadae nikaitwa kuweka sahihi ya dole gumba kwenye biometric machine. Baadae nikatia timu bank kuchukua japo elfu hamsini nashangaa salio lina digit sita
 
Asante sana mkuu. Itakua utaratibu umebadilika ila ndio hivyo tu maana saa hivi unaanza kuandika barua ya kuomba kuhamisha michango kweny uchangiaji wa Hiari unasubiri uitwe then ndio inafuata hiyo ya kujaza form ya withdrawal benefits.
 
Okay ila haichukui muda mrefu kikubwa uwe umetimiza vigezo na masharti vya umemaliza miezi 18, alafu unapigwa kalenda kidogo za njoo baada ya wiki 2 alafu unarudi tena unapigwa kalenda ya njoo wiki ijayo. Mie ilichelewa kwa kuwa walipoteza document zangu ikabidi niandike barua upya na nikatoa tena copy ya kiapo baada ya muda mfupi wakanipa hela zangu na niliombea nje ya eneo ambalo nilikuwa nafanya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…