Fahamu kuhusu gari aina ya Land Rover Freelander

consigliori

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2010
Posts
392
Reaction score
89
Heshima mbele wakuu,

Nataka kununua used Freelander, lakini watu wengi niliowauliza wanasema eti ni gari mbovu. sina utaalamu wa magari hivyo naomba ushauri kwa mtu yoyote anayeijua vizuri freelander.
Natanguliza shukrani.
==
SAME CASES:
---
---

==
MAONI YA WADAU:
Freelander kimeo,niliwahi kuwa nalo kikavunjika kioo cha nyuma. Ilikuwa shughuli kukipata,Nairobi kilikuwa kinauzwa Kshs 99999/-. Nikabahatisha Kampala kwa bei ya chini kidogo. Labda kama una uwezo mkubwa
---
Kiongozi Freelander ni gari isiyopenda shida! Kwa sababu hii basi ikiwa wewe ni mwenzangu na mimi unayefukia ramps kwa mwendo wa kumbeep Israel tegemea kulipaki juu ya mawe likiwa jipya! Spea zake ziko juu
---
---
---
 
kwa nini usifikirie kununua gari under Toyota logo unakuwa na uhakika wa spare na mahali popote pale.
 
kwa nini usifikirie kununua gari under Toyota logo unakuwa na uhakika wa spare na mahali popote pale,

Mkuu, nimeipenda ndiyo maana nataka kujua kama ina matatizo, nikiona ndivyo nitarudi kwenye Toyota zetu.
 
Nunua kitu toyota kulger, nzuri kuliko freelander. freelander itakutesa bure, zina matatizo ya engine pamoja na mfumo wa umeme.
 
consgrioli, ushauri wa ujumla ni kununua magari ya TOYOTA, maana vipuri vyake vinapatikana kiurahisi (new na used spares), halafu mafundi hata wa uchochoroni wanaziwezea kufanya matengenezo/service, lakini kama LADHA yako ipo kwa Freelander basi nunua hiyo ambayo kitu roho inapenda mkuu,then utapata uzoefu ukishaimiliki.
 
Freelander kimeo,niliwahi kuwa nalo kikavunjika kioo cha nyuma. Ilikuwa shughuli kukipata,Nairobi kilikuwa kinauzwa Kshs 99999/-. Nikabahatisha Kampala kwa bei ya chini kidogo. Labda kama una uwezo mkubwa
 
poleni wanajf na shuruba zooote za mwaka 2012.
Nawashakuru wanajf mmekuwa mhimili mkubwa wa kazi zangu na maisha yangu kwa ujumla.

Kuna hizi gari aina ya landrover freelender, kuna mwanajf mwenzangu anataka aniuzie, sinauzoefu nazo katika upatikanaji wa spea, utumiaji wa mafuta, uimara wake nk. Naombeni wana jf mnisaidie kuzifahamu vizuri.

Ahsanteni
 
spea za landrover siyo issue zimejaa tele na bei yake ni poa nenda libya street kuna maduka ya spea za magari ya ulaya very cheap you cant imagine
 
spea za landrover siyo issue zimejaa tele na bei yake ni poa nenda libya street kuna maduka ya spea za magari ya ulaya very cheap you cant imagine

nimekupata mkuu, vipi ubora wa gari aina hiii ukoje?
 
Nasikia zinachemsha balaa.sijui kama ni rejeta au zaidi
 
Tatizo lipo kwenye rejeta unaweza endesha gari rejeta likastop kufanya kazi nini kinachofata injini kuchemsha
 
Zile za mwanzo zilikuwa na matatizo sana (Fleelander 1) ....utabalisha head gasket sana na wakati mwingine cylinder head-hii ni 1.8L na 2.5 V6 petrol engines (Rover Engine). Lakini za baadae zenye BMW engine hazina shida.
 
rejeta kweli ina tatizo? tatizo linaeza kuvuja na sio kugoma kugoma rejeta ni water pump igome sio rejeta mkuu, wengi wetu tunatia maji kwenye rejeta halafu sio safi inapelekea kuziba hiyo rejeta
Tatizo lipo kwenye rejeta unaweza endesha gari rejeta likastop kufanya kazi nini kinachofata injini kuchemsha
 
Ninaamini hapa nitapata majibu mazuri. Mimi pia nilikuwa nahitaji sana kujuzwa juu ya uimara na upatikanaji vipuri kwa Freelander
 
Wataalam, naomba kujua kama Land Rover Freelander ni gari nzuri kwa matumizi ya kawaida hapa kwetu Tanzania.
 
Kama una uwezo wa kwenda kwenye garage za maana nunua, otherwise uswahilini kwa wagonganyundo watakwambia, "hizi gari mbovu saaaana badilisha injini"!!
 
Pointi yako nimeichukua mkuu, ngoja tusubiri wengine pia wanasemaje maana hizi Garage za maana kwa sasa hazihepukiki. Magari mengi hata Toyota za 2007 lazima utaenda kwenye garage ya maana tu kwani hata RAV4 ya 2007 haitengenezeki mtaani kwa wagonga nyundo.

Kama una uwezo wa kwenda kwenye garage za maana nunua, otherwise uswahilini kwa wagonganyundo watakwambia, "hizi gari mbovu saaaana badilisha injini"!!
 
Kiongozi Freelander ni gari isiyopenda shida! Kwa sababu hii basi ikiwa wewe ni mwenzangu na mimi unayefukia ramps kwa mwendo wa kumbeep Israel tegemea kulipaki juu ya mawe likiwa jipya! Spea zake ziko juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…