Fahamu kuhusu kada ya Biotechnology (bioteknolojia) na majukumu ya wataalamu wa Bioteknolojia

Fahamu kuhusu kada ya Biotechnology (bioteknolojia) na majukumu ya wataalamu wa Bioteknolojia

Joined
Apr 6, 2020
Posts
16
Reaction score
48

[IMG alt="Dyf"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/351/351123.jpg?1564308877[/IMG]
Dyf
Senior Member

Monday at 5:51 PM

Utangulizi
Bioteknolojia ni aina ya teknolojia inayotumia elimu ya biolojia kwa manufaa ya binadamu. Ni teknolojia ya uvumbuzi wa mambo mbalimbali kwa manufaa ya binadamu, kwenye upande wa afya, kilimo, mazingira na viwanda na ilianza kutumika tangu mwaka . 1919 na mwanasayansi mjerumani aitwae Karl Ereky ikiwa na makampuni (biotech companies) zaidi ya 2300 USA, zaidi ya makampuni 100 India, Canada, China, Ujerumani, Italia hadi afrika ya kusini. Watalamu wa bioteknolojia wanazalishwa na vyuo vingi duniani kwa sababu ni uwanja (field) inayokua kwa kasi sana kutokana na uhitaji wake kua mkubwa.

Mtalamu wa bioteknolojia ameandaliwa kua mtafiti katika sayansi ya maisha (Life Science) huyu ndie anaeleta utatuzi katika maeneo mbalimbali hasa afya ya mwanadamu, uvumbuzi wake unatumika katika kuboesha mbinu za matibabu, mbinu za upimaji magonjwa, nk kwa sababu ni mwanasayansi pekee aliesoma sayansi katika ngazi ya MOLEKULI (MOLECULAR LEVEL).

Historia fupi

Hizi ni mifano michache kati ya maelfu ya uvumbuzi katika bioteknolojia:

1928 Alexander Fleming aligundua fangasi (fungi) wanaoweza kuzuia ukuaji au kuua bakteria. Dawa zote za penisilini kama amoxicillin, ampicillin, nk. zimetokana na uvumbuzi wake.

1944 Kary Mullis aligundua mbinu iitwayo Polymerase chain reaction (PCR) inayotumika kupimia magonjwa mbalimbali mfano . COVID 19, HIV, Hepatitis B, Dengue, na mengine mengi, mbinu hii ni ukombozi wa dunia katika afya ya mwanadamu kutokana na ufanisi wake.

1978 Insulini bandia (artificial insulin) iligunduliwa na mtalamu wa bioteknolojia na mpaka leo wagonjwa wa kisukari (diabetic patients with hyperglycemia) wanaitumia duniani kote kushusha kiwango cha sukari kwenye damu.

1950 Alec john Jeffreys alivumbua mbinu ya kumtambua binadamu au viumbe wengine kwa kutumia vinasaba (DNA) mbinu inafahamika kitalamu kama genetic fingerprinting and DNA profiling ambayo inatumika dunia nzima na watu wa usalama kama polisi kuwatambua wahalifu mfano F.B.I marekani wako vizuri sana katika hili.

Majukumu ya mtalamu wa bioteknolojia kwa upande wa afya.

Kubuni mbinu mpya za upimaji wa magonjwa, zenye ufanisi mkubwa na zinazoweza kugundua maambukizi ya muda mfupi sana mfano Polymerase chain reaction (PCR) na vipimo vya haraka (Rapid tesk kits). Kipimo cha PCR kinatakiwa kufanywa na mtaalamu wa bioteknolojia tu maana yeye ndie mtalamu katika eneo hilo.

Kugundua na kuzalisha dawa na kinga/chanjo (Vaccine) za magonjwa mbalimbali. Ugunduzi wa madawa na chanjo ni mchakato mrefu wa tafiti na majaribio ya maabara, na si jukumu la tabibu (daktari), ni jukumu la wana bioteknolojia (Laboratory scientists, waliosomea tafiti).

Utengenezaji wa hataki (Reagents) za maabara zinazotumika kupimia magonjwa katika maabara za binadamu na wanyama (clinical laboratory reagents). Mfano monoclonal antibodies and enzymes. Serikali inatumia pesa nyingi sana kununua hizi hataki kutoka nje ya nchi.

Kuzuia tatizo la aleji kwa kufanya uoanishaji wa dawa na genetiki ya mgonjwa (Pharmacogenetics/ personalized medicine). Wagonjwa wengi wanapewa dawa ambazo zinawaletea madhara (aleji) kutokana na kutokujua nani anapaswa kupewa dawa gani kulingana na asili ya miili yao. Hapa biotechnologist anasimama kama mshauri wa daktari kabla ya kumpatia dawa mgonjwa.

Wapo wagonjwa wanatibiwa bila kupona (Infectious diseases), kitalamu tatizo hili linajulikana kama drug resistance. Tatizo la usugu linatatulika kwa mbinu za kibioteknolojia mfano DNA sequencing and alignment na uoteshaji wa vimelea vya magonjwa (bakteria na fangasi) maabara kisha kuangalia vinaweza kufa kwa dawa gani (microbial culture), na kupima wingi wa vimerea katika mwili mfano HIV viral load tests (HVL) na early infant diagnosis (EID).

Kufanya shughuli zote za vinasaba (DNA au RNA), ikiwa ni pamoja na kutibu magonjwa kwa njia za jenetiki, (gene therapy), kumechi kati ya mzazi na mtoto, au ndugu na ndugu kupitia DNA. Hii inaondoa utata katika kujua nani ni mzazi wa nani au nani ni ndugu wa nani mfano janga la moto la msanvu morogoro.

Kufanya tafiti za afya ya binadamu na kutoa elimu kwa watumishi wa afya / kutoa ripoti za tafiti kwa watumishi wengine wa wizara za afya. (Madaktari, nk).

Mgawanyiko wa majukumu baina ya watumishi wa wizara ya afya:

WATAFITI (researchers)
: Hili ndilo kundi la kwanza linalotoa majawabu na mbinu mpya za kupambana na magonjwa mbalimbali, hili ni kundi la wanasayansi waliobobea katika maeneo mbalimbali (classified scientists) mfano: Microbiologists, Molecular biologists, biochemists, chemists(Pharmacists), Immunologists, Bioinformaticians, Bio Statisticians, epidemiologists, Physicist and Botanists. Unaposema Biotechnologist ni mwanasayansi alieandaliwa katika maeneo yote tajwa, hivyo anauwezo mkubwa sana katika kufanya tafiti.

NB: Katika eneo la madawa mfamasia (Pharmacist) amebobea sana katika kemia ya madawa, hivyo hufanya kazi na mtaalamu wa biolojia na fizikia katika uvumbuzi. Biotechnologists wanaweza fanya kazi zote za maabara ya binadamu (clinical laboratory activities), ila ni kuanzia hatua ya uchakataji wa sampuli na si kuanzia hatua ya kuonana na mgonjwa moja kwa moja japo baadhi ya vyuo katika mitaala yao vinawaongezea mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa moja kwa moja.

WATOA HUDUMA ZA AFYA (Medical personel):
Hili ni kundi la watalamu wa afya walioandaliwa mahususi kwa ajili ya kutoa huduma za afya moja kwa moja kwa mgonjwa, watalamu hawa wanategemea moja kwa moja majibu na mbinu kutoka kwa watafiti ili kuzitumia katika kutibu wagonjwa.

Daktari (Medical doctor),
Huyu amefundishwa masomo mbalimbali yaliyopatikana kutokana na tafiti za wanasayansi mbalimbali tajwa hapo juu. Daktari wa binadamu si mtafiti/mvumbuzi, ameandaliwa kumtibu mgonjwa kwa kutumia mbinu zilizopitishwa na kukubalika baada ya tafiti mbalimbali. Na ni daktari pekee ndie anaejua namna ya kumtibu mgonjwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote za jinsi ya kutibu ili kuokoa maisha. Kitalamu ni daktari pekee ndie amebobea katika kutibu ila si kutafiti na kufanya uvumbuzi isipokua yule alie specialize katika research na kuachana na kutibu moja kwa moja.

Mteknolojia wa maabara ya binadamu (medical laboratory technologist):
Hili ni kundi la watalamu walioandaliwa kwaajili ya kufanya upimaji wa magonjwa mbalimbali ya binadamu (diseases diagnosis), hawa pia ni unclassified scientists hawajaandaliwa kua wavumbuzi au watafiti, wameandaliwa kutoa huduma za upimaji magonjwa, kwa sababu hawakuandaliwa katika sayansi ya MOLEKULI (Molecular level science) wao wanasoma applied sciences.

Muuguzi (Nurse):
Hili ni kundi la wataalamu walioandaliwa kuwatibu wagonjwa kwa kufuata maagizo au kujadiliana na daktari, kufanya uangalizi wa wagonjwa muda wote, kufuatilia hali zao na mabadiliko yeyote pindi wanapokua wakipatiwa matibabu, hawa ni watu muhimu sana.

NB: Kundi la kwanza la watafiti ni kundi ambalo hua halijulikani licha ya kua na mchango mkubwa sana katika kufanikisha matibabu ya mgonjwa, kwa sababu Daktari ndie mtu wa mwisho mtoa maamuzi hivyo jamii inampa nafasi kubwa sana na kufikiri ndie anaejua kila kitu, na hata kufikiri mchakato wa upatikanaji wa dawa mpya au chanjo ni jukumu lake kitu ambacho sio kweli na kwamba hilo ni jukumu la watafiti.

Changamoto iliyopo Tanzania kwa wataalamu wa Bioteknolojia(WATAFITI).
Wizara ya afya haitambui uwepo wa wataalamu hawa, ambao ni kitovu cha tafiti za afya duniani kote. Wizara ya afya haijawapatia nafasi ya kufanya kazi zao katika maeneo yao, Wizara haijawapatia leseni za kufanya kazi zao. Hakuna mfumo wa kuwatambulisha moja kwa moja.

Vipimo vinavyohusisha vinasaba (DNA /RNA) Tanzania havifanywi na watalamu wa bioteknolojia ambao ndio walioandaliwa kufanya vipimo hivyo na wizara ya afya haitaki kuwaona wakifanya kazi katika maabara za binandamu licha ya kua na uwezo wa kufanya hivyo na bado haitoi ufafanuzi wakafanye kazi zao wapi.

Hitimisho:
Ni jukumu la wizara ya afya Tanzaia kuwapatia leseni wataalamu wa bioteknolojia ili watatue changamoto za wizara ya afya katika utoaji wa huduma za afya kama ambavyo dunia nzima inawatumia vizuri. Tubadilike na teknolojia

ALIANDIKA
Modern Scientist :
Moshi RN Contact : 0758406251 Email moshingamba@gmail.com
 
Bongo kuna kundi maalum sana la biologist ambao ni nyenzo kubwa sana kuijenga life science hapa bongo lakini serikali haiwatambui kabisa wanapoteza dira sababu hawana ajira rasmi inayowatambua moja kwa moja kma professionals wa hii discipline .
Nadhani hao hata leo hii kwenye janga hili la Covid19 wangekuwa msaada mkubwa mno kuliko kuwaachia wanasheria km ummy kuongoza hili janga anyway just saying...
 
Bongo kuna kundi maalum sana la biologist ambao ni nyenzo kubwa sana kuijenga life science hapa bongo lakini serikali haiwatambui kabisa wanapoteza dira sababu hawana ajira rasmi inayowatambua moja kwa moja kma professionals wa hii discipline .
Nadhani hao hata leo hii kwenye janga hili la Covid19 wangekuwa msaada mkubwa mno kuliko kuwaachia wanasheria km ummy kuongoza hili janga anyway just saying...
Umenena vyema Dampa
 
Itafika kipindi aliyesoma hii kozi atatafutwa na tochi mchana!!
Ndio ukweli ni kwamba bado kwa nchi masikini biotechnology haijawa specialization yenye soko. Waliosoma kozi hii inabidi wawe flexible kufanya mambo mengine yasiyohusiana moja kwa moja na kozi hii. Kozi hii ipo zaidi ki-research na nchi maskini hazifanyi research sana.
 
Back
Top Bottom