Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
5,558
Reaction score
1,456

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Wakuu naomba kufahamishwa, ni mahala au muda gani natakiwa kutumia OverDrive funcionality kwenye auto transmission. Ni kwa Ufahamu tu

Nawasilisha
---
Hello GREAT THINKERS!
Nimekutana na huu ubishani kuwa ni wakati gani Over drive facility inatumika katika gari? Je ikiwa off inaonekana vipi kwenye dashboard? Thanks
---
wakuu

ni nini hasa matumizi ya Over Drive kwenye gari yenye automatic gear (transmition), je hutumika wakati gani haswa yaani ni wakati gani na speed gani inatakiwa iwe on au off... what are the pros and cons?

Ahsanteni
---

UFAFANUZI WA JUMLA WA MATUMIZI YA OD

Overdrive ni nini?
Overdrive ni gia katika mfumo wa gari ambayo uifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Over drive ni kama gia ya ziada itakayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya engine yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea na mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo mana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya engine. Mfano katka gari ya kawaida yani 180km/h ili ufikishe speed 120km/h basi rpm inaweza kua 4000rpm. Katka barabara tambarare. ila ukiweka over drive unaweza tembea speed hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara tambarare.

Utajuaje kuwa Overdrive ipo On au Off?
Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako inamaanisha kuwa Overdrive ipo off na pindi Kitaa cha overdrive kisipoonekana basi overdrive ipo on. Overdrive imewekwa Kama option yakutumia wakati ukiwa unatembelea speed chini ya 60km/h.



Matumizi ya Overdrive ni yapi?
Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe gari yako inakuwa imepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.

Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au On na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gear kubwa na speed less than 60km kwahio unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.

UFAFANUZI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
---
---
---
---
---
---
---
---
---
---
---
 
Mkuu Over drive inakuja unapotaka kwenda speed zaidi ya 80,so gari inakuwa na uwezo wa kuingia gia no 5
 
Kwa hiyo mkuu utaona kuwa kwa mazingira yetu ya Dar mara nyingi OD inabidi iwe on (na ikiwa off huwa inawaka taa either kwen dashboard) kuonyesha kuwa iko off na u have to think kwa nini iwe off.

Mi binafsi naiweka off kama ninataka kuachieve speed kubwa kama kuovertake chap chap kisha kuirudisha on. Ikiwa off inakula sana wese.

Source: Wikipedia.
 
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita motakaa nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe motakaa yako inakuwa umepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka uklisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
 
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi...

Mkuu Mbalamwezi Shule kubwa sana hii na inabidi watu wengi zaidi waifahama maana kila kukicha bei ya Mafuta inapaa kama Ndege ya Uchumi ya EL.

Asanteni wakuu kwa maelezo yenu mazuri na Jengefu
 
mimi nilikuwa naitumia kwenye rafu roads kwani nikiweka huwa gari inakuwa zito hivyo nikitaka kuwahi huwa nazima kweli wajapani tunawahitaji kwa maelezo ya product zao
 
hii thread imenielimisha sana jamani,asante kw aalieuliza na waliotoa majibu mazuri na murua kabisa,ninatumia auto sometimes so nitaiweka OD on mda wote!!
 
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi....
Mkuu asante umesomeka vizuri sana.
 
hii thread imenielimisha sana jamani,asante kw aalieuliza na waliotoa majibu mazuri na murua kabisa,ninatumia auto sometimes so nitaiweka OD on mda wote!!

JF ni kila kitu, Majibu ya Maswali yako yote yako hapa Jamvini Mkuu, wewe ni sula la ku initiate, Watu si Wachoyo hapa.

Asanteni
 
Ila drive gari manual kuna raha yake. Bongo siku hizi waendeshaji ni wengi sana, madereva ni wachache. Nilikuwa na gari yangu manual kutaka kuiuza kila mtu akiiona anasema ingekuwa automatic angenunua kwa bei ninayotaka mimi, vinginvyo nipunguze bei. Nikaamua kuahirisha mpango wa kuiuza LOL!
 
huyo aliyesema ukivuka 80 kpm unatumia mafuta kidogo sidhani kama ni mkweli.unavyokanyaga zaidi ndo mafuta yanakwenda zaidi.theory hiyo inawork kama uko kwenye speed kubwa zaidi kama 140 kmp au zaidi au chini ya 80.otherwise overdrive ni kwenda gear number 5 na kwa mazingira ya day iweke off daima kwani wataalam wanasema kuiacha on saa zote ina damage engine kinamna achilia mbali suala la consumption kubwa
 

 

Mdudu,

acha kudhani dhani juu ya mambo ya kitaalam. motakaa katika hali ya kawaida, na kwa wastani, inatumia mafuta mafuta kidogo kabisa ikiwa kwenye mwendo wa kati ya 70 km kwa saa na 110 kwa saa. Ukizidi hapo, unakuwa kwenye matumizi ya juu kabisa.

RPM (Revolution per minute) ni kiwango cha mzunguko wa injini. Ikiwa unatumia gia namba 4 hadi mwendo kasi wa 70 km kwa saa, basi inawezekana, kama injini ni nzuri, RPM ikawa kwenye 2600-2800 hivi kama uko kwenye mpango wa OD, basi motokaa yako itabadili gia na kuingia kwenye 5, ambayo ni OD, na ukizidisha hadi kati ya 80 na 90 hivi, basi RPM itapungua hadi kufikia 2200 hadi 2500 hivi.

Maana yake nini? Maana yake injini sasa itazunguka mara chache zaidi kwa mwendo kasi zaidi (70km/h hadi 110 km/h).

Ukizidisha toka 120km/h na kuendelea, basi na RPM zitaongezeka na mafuta yatanywewa mengi tu.

Auto zinafaa sana kwenye foleni kama za Dar, ambako unaepuka sana matumizi ya kilachi (clutch), maana unajikuta mguu wa kushoto unakuwa busy kukanyaga kanyaga ndani ya mita pengine 200 tu katika dk 45 pale Moroko saa mbili asubuhi.

Manual zinafurahisha long trips, unajidai na unajisikia hasa unaendesha. Unaweza kuiamuru gari kwenye milima iende upesi zaidi, si kama auto ambayo inapanga yenyewe. Unaweza kumpita mwingine kwa wepesi wa hali ya juu, si kama auto ambayo itabidi uondoe OD ndo uongeze kasi ya kumpita.
 
Sasa hivi magari ya manual ya kutoka Japan yanauzwa bei ghali zaidi kuliko ya automatic.
 
Kwa mawazo yangu (nina magari yanayotumia manual na automatic), gari la automatic ni nzuri sana kwa safari ndefu. Infact unaweza kubadilisha gear, k.m.

Kama unataka ku overtake, sio kwa kutumia OD, bali kwa kukandamiza accelerator kwa nguvu ghafla. Kitendo hicho (kickdown) kitabadilisha gear na kuweka gear yenye nguvu ya kuweza kuongeza kasi na ku overtake.
 

Ni hakika Dingi unenavyo, na kwa namna hiyo hiyo pia unaweza kubadili gia kwenda ndogo kwa kuachia pedeli ya mafuta kila kipimo cha mwendo kinapofikia mafunda ya 20, mfano ikifika 20km/hr ukiachia pedeli ghafla (kick up) itaingia namba 2, ikifika 40km/hr ukaachia pedeli ghafla itaingia namba 3, ikifikia 60km/hr itaingia 4, na ikifikia 80km/hr itaingia namba 5, OD.
 
Mkuu mbalamwezi, nashukuru kwa elimu uliyotoa, mie nilikuwa sijui hata ina maana gani,wala hata kuitumia.

Big up wazee wa humu jamvini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…