Fast Forward
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 551
- 709
Kwa ninavyoona od inatakiwa iwe on mda wote kutapunguza ulaji wa mafuta anaebisha afanye kwa vitendo aendeshe gari od ikiwa on na afike hadi speed 60 halafu azime od aone gari inavyokua kua nzito na kupungua mwendo
Od ikiwa on, inamaanisha gari itaweza kuingiza gea mpaka tano.na ikiwa off haitaingiza mpaka tano.hivyo dreva aangalie anataka kutumia eneo gani? Kwenye mlima au kwenye njia mbaya?
Umeeleza vyema kazi zake, tuambie taa ya OD ikiwaka inamaanisha nini na ikiwa imezimwa kwenye dashboard inamaanisha nini.
Well said, baada ya maelezo mazuri ulitakiwa kuwaambia wadau humu kuwa wakati OD inakuwa On taa kwenye dashboard inakuaje na wakati OD inakuwa Off taa kwenye dashboard inakuaje. Hilo ndilo limekuwa tatizo la wengi...
Mkuu hapa ndio maana huweza kukuletea majanga kwenye gear box au engine
Sababu unakuwa umetoka namba tano na kurudi namba tatu hapo lazima gari ivume mlio mkubwa unaoweza kupasua engine (block) au gear box
Tambueni ya kwamba over drive ina maana gani wala msiumize vichwa kwa vitu vinavyojulikana
kumbe kuna watu wanamagari halafu bado kuna vitu hawajui kazi zake
Mkuu unaendesha Gari bila hata kujua vitu vya "msingi" kabisa? kweli Shukuru Kawambwa hasa!!!!
Cruise ni cruise control. Ukiiweka on maana yake kama uko speed fulani unamaintain hiyo hiyo. Kama ni 50
hai tapanda au kushuka. Kama ni 160 the same. Ni kwa ajili ya highway. Ukishaweka unatoa mguu kwenye moto na ukikanyaga brake inajitoa yenyewe. Kwa huku uswazi itakuuwa mkuu.
Kimbunga
thanks ....hivyo basi OD inafaa zaidi kwenye long distance drive? na je ina effect yeyote kwenye fuel consumption?
mimi nilishawahi kutia od off nikiwa katika speed 100. Na ingine haikubuma.
Mkuu, nilishajibu swali la overdrive hapo nyuma, hebu angalia hapa chini;
Katika hali ya kawaida ni sawa kuacha gari kwenye OD wakati wote (taa ya O/D iwe off, haiwaki). Unaweza kuiondoa kwa sababu nilizotaja hapo juu.
Kumbuka:
Overdrive off - taa ya OD inawaka kwenye dashboard (ni vema katika mazingira yaliyotajwa hapo juu, lakini si vizuri ukiwa kwenye spidi za juu)
Overdrive on - taa ya OD haiwaki kwenye dashboard (ni vema katika spidi za juu)
Overdrive inatumika ili kuifanya gari ikupe namna fulani ya gia za juu na kama vile gia fulani ya ziada unapokuwa kwenye spidi za juu. Tuseme gari yako ya Automatic ikiwa na gia 6, Overdrive ni kama inakupeleka gia za 5,6 na namna fulani kama vile gia ya 7. Sasa mara nyingi, wengi huwa tunaendesha gari likiwa tayari kwenye Overdrive toka tunapoondoka (taa ya OD inakuwa haiwaki pale kwenye dashboard), yaani hatuweki Overdrive off. Hilo sio tatizo. Ina maana kwamba, unakuwa umeipa gari uamuzi wa kukuweka kwenye gia za chini ukiwa mwendo mdogo na zile za juu na ya ziada kila ikifikia spidi ya juu, hasa kuanzia 70km/hr. Hilo ni nzuri, kwa sababu gari itakapoingia kwenye Overdrive ina maana inapunguza mzunguko wa injini inapofikia spidi ya juu, na hii inafanya gari itumie mafuta kidogo, na hata muungurumo unakuwa wa chini.
Lakini sasa, ukiondoa Overdrive kwa kui-switch off (yaani taa ya OD inakuwa ON), ni sawa na kuiambia gari nataka usinipeleke kwenye zile gia za ziada za juu (kama ya tano, sita na saba) kwa sababu nataka injini inipe nguvu zaidi, na hasa pale ninapotaka ku-accelerate haraka, kama ku-overtake.
Kwa lugha nyepesi, ikiwa gari iko kwenye Overdrive, inaweza kukupeleka kwenye gia za juu wakati wewe bado unataka injini ikupe nguvu au acceleration ya haraka, ambapo unaweza kukuta gari haichanganyi vizuri wakati unataka ku-overtake haraka. Ni sawa na ukiwa na gari la manual, urudi gia namba tatu wakati wa ku-overtake, lakini wakati uko katikati ya ku-overtake ubadili gia toka gia ya tatu kwenda ya tano. Sasa ukiweka Overdrive off, ni sawa na unaiambia gari isije ikaingiza gia toka ya tatu kwenda ya tano kwa sabau tu imehisi tayari umefikia spidi ya juu kwa hiyo ikakuchagulia gia za Overdrive hata wakati bado unahitaji injini ikupe power ya ku-overtake.
Ila ni vizuri ukisha overtake urudishe gari kwenye Overdrive.
Sasa, kuna wakati ni vizuri tu kui-switch Overdrive off muda wote. Kwa mfano gari ni automatic na limebeba mzigo mkubwa. Au kwa mfano unaendesha gari katika barabara mbaya ambapo hata kufika spidi ya 80km/hr ni shida, basi ni vema ku-switch overdrive off. Na pia ukiwa na mzigo mkubwa au hata bila mzigo unateremka mteremko mkali au mteremko kwenye barabara mbaya, au ya matope, ni vema kutoa Overdrive, na hata kuirudisha gia toka D kwenda 2. Ukiacha gari kwenye Overdrive inaweza ikafikia mahali ikawa kama unashuka mteremko mkali na gari ya manual wakati uko gia ya tano au sita, hata kama mwendo wako sio mkali. Gari inakuwa nyepesi sana, na inakuwa haina breki ya injini.
Kwa mfano, basi au lori ambalo lina gia automatic, dereva kushuka Kitonga wakati yuko kwenye Overdrive ni kutafuta ajali mbaya. Ina maana gari itakuwa inashuka mteremko na wewe unaipunguza mwendo kwa kutumia breki peke yake, bila injini kusaidia kupunguza spidi ya gari. Matokeo ni kwamba breki zitaanza kupata moto sana na kuungua (utasikia harufu mbaya sana kama vile clutch inaungua) na inaweza hata kutokea breki zikafeli. Ukigusa rim ya tairi utakuta ina mto vibaya sana na tairi inaweza kupasuka kwa kuyeyuka!
Kuna sehemu fulani kule Mbeya kwenda Tukuyu mteremko unaitwa Uwanja wa Ndege, ukiwa na lori au basi automatic ukashusha nalo ule mteremko ukiwa kwenye Overdrive, unaweza ukakuta inafikia breki hazishiki tena, zimeungua! Kushuka mteremoko kama ule na lori au basi liko kwenye Overdrive ni sawa na kushuka mteremko ukiwa na lori au basi la gia manual wakati uko gia ya sita, huku unapunguza spidi kwa breki!!!
Kwa loli au basi la automatic, unaposhuka milima ya Lushoto au Kitonga au Uwanja wa Ndege (kwenda kule Tukuyu) lazima u-switch off Overdrive, na hata zaidi uitoe gari kwenye D na kwenda kwenye 2.
Nadhani nimekusaidia kukuelewesha suala la Overdrive mkuu.
Kawaida taa ya Over Drive ikiwa on gari huwa nyepesi sana na inatafuna sana mafuta...taa ikizima means Over Drive iko off na ndio normality yake....make sure km upo mjini au sehemu ambayo huhitaji kuendesha speed kali taa ya OD iko off ili ku-serve mafuta???
Ngoja niwachambulie kuhusu taa kuwaka na overdrive yenyewe:
Kuhusu taa:
Taaa yoyote inapowaka wakati engine iko on, humaanisha kuwa kuna hitilafu inabidi irekebishwe. Unapoweka switch on kwenye dashboard, taa mbali mbali huwaka na unapowasha gari, taa zote huzima. Mathalani taa ya airbag ikiwaka au ya betri ikiwaka au ya oili ikiwaka, au ya over drive ikiwaka, inaonesha kuwa eneo hilo linashida na inabidi ufanye kitu ili taa hiyo ijizime.
Kuhusu over drive:
Tuchukue mfumo wa gari ya manual ili kuelezea maana ya over drive. Gari za zamani za manual zilikuaw na gear mwisho nne, lakini kutokana na kukua kwa teknolojia, wakagundua mtoto wa gearbox ambaye uki mu engage, gari inahama kutoka kutumia gearbox ya kawaida kwenye gear namba nne, na kuanza kutumia mtoto wa gear box ambaye kwenye gari ya manula itakuwa gear namba tano hadi sita kwa baadhi ya magari lakini kwenye gari ya automatic unapotumia mtoto wa gearbox ina maana unatumia gear ya over drive!
Kwa hiyo ili engine izunguke kidogo kwenye speed kubwa na ili uweze kuokoa mafuta, kwa gari ya manual utatumia gear namba tano, na kwe gari ya auto utatumia over drive. Kwa hiyo unapozima gear ya over drive, inamaana unaacha kutumia mtoto wa gearbox na hivyo gari itatumia gear kubwa kubwa, na hilo husababisha engine kuzunguka sana na mafuta kwenda kwa wingi. Kwa kifupi unapoendesha gari, taa ya over drive inabidi iwe imezimika wakati wote isipokuwa kwa vipindi maalum ambapo gari itahitaji nguvu ya ziada kama vile kuovertake au kupandisha milima.
Mkuu OIL CHAFU,mimi gari yangu ikiwa highway na OD ipo OFF yaani taa inawaka gari huwa nyepesi sana hata relaxibility yake inakuwa ipo vizuri sana,sasa nikibonyeza button ya OD kuwa ON taa inazimika na gari inaunguruma kwa nguvu...speed inaongezeka na rotation ya mafuta inapanda sana...je hapo haili mafuta? Mfano..wiki mbili zilizopita nilienda safari ya 440km,wakati naenda niliweka OD OFF muda wote mpaka nafika nilitumia lita 35 wakati narudi niliweka OD ON na nilitumia lita kama 42 hivi. Je hapa imekaaje mkuu.? Ufafanuzi tafadhali
Umeeleza vyema kazi zake, tuambie taa ya OD ikiwaka inamaanisha nini na ikiwa imezimwa kwenye dashboard inamaanisha nini.