Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Overdrive inakua on wakati gani? Wakati taa ikiwa inawaka kwenye dash board au ikiwa haiwaki. Maana nikibonyeza hicho kitufe kuingia ndani kwenye dash board inaniandikia od off na gari inakuwa nyepesi sana na inachanganya haraka sana, ila nikipress kitufe kikawa juu kwenye dash board haiwaki na gari hua nzito, gari ni rav4, so ni yapi matumizi sahihi na yanayosave mafuta? Maana maelezo ya hii thred yananichanganya tu
 
Naombeni msaada kwenye hili, O/D (over drive)inafanyaje kazi kwenye gari?
Hawa wote wanakudanganya tu, mafuta makala yangu kuhusu 'Namna ya kutumia N, P, R, D, 2 na L' utajifunza na nahakika hutauliza tena mtu yeyote. Goodluck
 
Kwa kiswahili chepesi ninavyoelewa over-drive ni gear no tano katika gari za automatic na inafanya Kazi kuanzia kwenye speed 65-80
Samahani, mnakuwa munahadithiwa na nani mambo kama haya? Gear namba 5 na inafanya kazi kuanzia speed 65-80? Mhhh....

Kawaida gari ya automatic ikifika certain rpm inabadili gear, kwa mfano gear namba moja ikifika rpm 1800 inaingia gear ya pili, sasa ukiweka over drive, badala ya kubadili gear at 1800, inaweza kufika 3000rpm gear haijachange
 
Mkuu for further references, chukulia taa yoyote kwenye dashboard ikiwa haijawaka ujue inafanya kazi. Ukiona taa overdrive off manake hio over drive iko off, kama haipo iko basi ipo on. Uendeshaji unachangia kuona kama inachanganya fasta au slow. Jaribu kuieka on, kisha be hard on gas, utaona utakavoondoka. Watu wengi urndeshaji wao ni mwendo wa kawaida, sasa hii ikiwa on, ukiwa soft on gas utaona gear inachelewa kubadilika na utaona kuwa haichanganyi, kumbe tatizo ni wewe huitumii ipasavyo. Nilikuwa naendesha super custom nkiweka OD on basi mnyama anakwenda haraka kuliko ikiwa off. Siku izi utakuta kitu ECT PWR, kazi take ndo io io wamebadili jina tu naona
 
Over drive ni 5th gear kwa mfano gar yako ina gear tano,,unapoendesha zitajipanga mpaka gear 4 sasa ili uingie namba tano,,hapo ni lazima uweke OD ndio maana yake,,
 
Sijakufahamu kwenye red mkuu
 

Mkuu hujamwelewa Luginyo swali lake. Kwa ufupi anataka kujua akiweka OD kwenye dashboard kunakuwa na alama yoyote au hakuna? Hili ni swali linalotutatiza wengi. Wengine wanasema OD ikiwa off dashboard inaonyesha. Ikiwa on kwenye dashboard huoni kitu na kinyume chake. Sasa ni kuchanganyikiwa tu. Ikiwa una elimu nalo hilo tafadhali tujuze.
 

Hapo kwenye bold mkuu umenichanganya maana GX100 Mark II ina OD na ECT PWR. Naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Hapo kwenye bold mkuu umenichanganya maana GX100 Mark II ina OD na ECT PWR. Naomba ufafanuzi tafadhali.
Ni same same mkuu. Hazina tofauti ufanyaji kazi wake, kila moja ikiwa on utaona inakaa kwenye gear longer than ikiwa off. Tofauti yao ni kuwa ECT PWR ukiiona kwenye dashboard basi ujue ipo on na OD ukiiona kwenye dashboard ujue ipo off
 
Naomba haswa kujua kwa wataalamu hii over drive inatakiwa ikaeje ili iwe off.
 
Unapo endesha gari batani usiibonye na maanisha iwe juu..na kwenye dash isiwake warning light yake.lkn ukibonyeza batani inamaana hapo umeiweka OFF.

Yaaani ni hivi unapoendesha gari na haujabonyeza batani gari itabadili gia zote kama ni tano itamaliza..

Lkn ukibonyeza batani kwenye dash board itawaka taa inayosena od off inamaana hapo gari haiwezi maliza gia.
 
E
 
Mmegusa penyewe, hii kitu huwa inanifikirisha sn
 

Overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi. OD hukupa mwendo wa kasi, uliotulia lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (revolutions per minute rpm). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.

Mfano katika gari ya kawaida yaani 180km/h ili ufikishe spidi 120 basi RPM inaweza ikawa 4000rpm katika barabara ya tambarare. Lakini ukiweka overdrive unaweza kutembea spidi hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara ya tambarare.

Utatambuaje kama Overdreive (OD) ipo on au off?

Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako, inamaanisha kuwa overdrive ipo off na pindi kitaa hicho kisipoonekana basi tambua kuwa overdrive ipo on. Overdrive imewekwa kama chaguo (option) la kutumia wakati ukiwa unatembelea spidi chini ya 60km/h.

Unaweza kutumia ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukishamaliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.

Katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea gari kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo

Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au on na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gia kubwa na mwendokasi chini ya 60km kwahiyo unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa

Chanzo: Mwananchi
 
Bado sijakuelewa mkuu, binafsi huwa napenda kuweka O/D off kwenye dashboard ikiwa nipo kwenye highway na safari ndefu au pindi ninavyotaka ku overtake gari ambayo nayo ipo speed. Naomba niambie kama nipo sahihi?
 
Isipoonekana kwenye dashboard ile alama ndo umeeka overdrive?tueleweshane maana nahic cjaelewa bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…