Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Boss gari lina gear 4,tena baada ya hapo kuna gear namba ngapi?!
Maana kama haujajua hata kwenye list ya gear pale huwa kuna ile gear inaandikwa nadhani ni D2 ambayo ukiweka mzunguko wa gari unaongezeka.... So hebu nipe ufafanuzi
Ndugu yangu Overdrive ni GEAR ya mwisho katika gearbox
usiangalie hapo juu unapoendesha, sisi tunazungumzia ndani kabisa ya gearbox kuna gea ya mwisho .km ni 4 au ni 12 kwa Scania ndio huitwa Over drive gear
kuna mahali tulizungumzia humu ndani tukamaliza
labda nirudie

kwenye engine kuna gear namba 1 mpaka ya mwisho km ni 3,4 au 12 ile ya mwisho huwa ni ndogo kuliko mzunguko wa Crankshaft (Driver gear) inayozungushwa na piston, kwa hiyo mzunguko wake kwa diameter uatakiwa uwe mdogo ili gari ikimbie na kutumia mafuta kidogo na sio Overdrive ni ya kuanzishia gari katika 0 km/h au kupandia milima, hata baiskeli wana overdive gear
Overdrive or OD is the highest gear in the transmission in an automatic car. It brings the RPM of the engine down at a given road speed to facilitate better speed and fuel efficiency. It also helps your car to provide the best performance in higher speed cruising. Overdrive helps when you drive at more than 50mph.
 

Attachments

  • 1591710801523.png
    6.7 KB · Views: 3
Maana kama haujajua hata kwenye list ya gear pale huwa kuna ile gear inaandikwa nadhani ni D2 ambayo ukiweka mzunguko wa gari unaongezeka.... So hebu nipe ufafanuzi
D2 maanake Driving gear 1 - 2, yaani gear itacheza kwenye 1 na 2 na haitoingia 3.
 
Haya mambo ya Overdrive hakuna kwenye Subaru,

Unakanyaga tu mafuta kidogo , kitu kipo spidi 130
 
Mkuu Over drive inakuja unapotaka kwenda speed zaidi ya 80,so gari inakuwa na uwezo wa kuingia gia no 5


Overdrive or OD is the highest gear in the transmission in an automatic car. It brings the RPM of the engine down at a given road speed to facilitate better speed and fuel efficiency. It also helps your car to provide the best performance in higher speed cruising. Overdrive helps when you drive at more than 50mph.
 
1. Kuna watu wana lalamika gari halina nguvu hasa anapo kanyaga mafuta kwenye mwinuko.

2. Kina watu break zimefeli na wana shangaa kwa nini?

3. Kuna watu wana lalamika magari yao kutumia mafuta zaidi.

Sasa fata yafuatayo hutajua.

Kama speed yako ni chini ya 50KM/Hr hakikisha OD/OFF inasoma kwemye dashboard.

Kama unashuka mlima au unatumia break hakikisha OD /OFF inasoma kwenye dashboard.

Kama una kanyaga mafuta ili kuongeza mwendo wa gari hakilisha OD/OFF inasoma kwenye bashboard.

Kama unapanda mlima hakikisha OD/OFF inasoma kwenye dashboard.

Kama una overtake hakikisha onaweka OD OFF.


Wapi OD inatakiwa kuwa ON.

Ni pale tuu speed imezidi 50 na huhitaji kukanyaga mafuta wala break.

Kusave mafuta kwenye highway.

Weka od off ikisha shika speed kuanzia 80 rudisha OD ON , utahisi gari haina engine.. [emoji1][emoji1]

Onyo
Kwa watu wa automatic ambao hawajui kutumia mikono yote miwili wakati wa iuendesha unaweza ishia machakani maana garinukiibadili kwenda oberdrive inakimbia utadhani imekata roho.

Gari ikiwa kwenye OD ni zaidi ya gari manual ikiwa kwenye neutral.

Unapo tumia break wakati OD ipo ON umaziukiza break kwa sababu hazipati msaada wa engine.
 
Sasa unasevuje mafuta wakati unatembelea gia 3 tu!

Kwangu gear ya tatu ni 33km/h to 53km/h. Gari inaanza kudai gia ya nne kuanzia 54km/h-73km/h. Kutoka 74km/h mpaka mwisho wa speed ni gear namba 5 tu!

Ukiweka OD OFF huwezi kuipata ile highest gear mkuu which is bad for fuel economy, rotation per minute itakuwa kubwa kuliko speed!

Mie huwa naizimaga na kuiwasha nikiwa speed ila nataka ku overtake. Gari inavuma inarudi gia ya chini kisha inakamata gia ya mbele inachomoka kama mkuki!
 
1. Kuna watu wana lalamika gari halina nguvu hasa anapo kanyaga mafuta kwenye mwinuko.

2. Kina watu break zimefeli na wana shangaa kwa nini?

3. Kuna watu wana lalamika magari yao kutumia mafuta zaidi...
Hiyo namba 1 ina uhusiano gani na OD.
 
Hujaelewa mkuu, samahani.

Jaribu maelekezo niliyotoa.

Weka OD OFF kisha kanyaga mafuta hadi speed ya above 70KM kisha rudisha OD ON, utakuja ujiambie.

Achana na theory, fanya uone tofauti.

Labda niambie kwanini kama tairi limebast wakati upo na speed kubwa unashauriwa kuweka OD OFF na usikanyage break
 
Sidhani kama itafika 70km/h ntatumia mafuta mengi sana mkuu! Kanuni yangu sikanyagi mafuta past 2rpm kwenye gia ndogo.
 
1. Kuna watu wana lalamika gari halina nguvu hasa anapo kanyaga mafuta kwenye mwinuko.

2. Kina watu break zimefeli na wana shangaa kwa nini?

3. Kuna watu wana lalamika magari yao kutumia mafuta zaidi...
Hapo kwenye kuovertake pako sahihi kweli!!? Unless mi sijaielewa hyo OD maana yake.
 
Sio wewe tuu pakee yako wasio jua matumizi ya OD.. tupo wengi[emoji1][emoji1]
Mie sio kama sijui mkuu, ila mfumo wa gear katika gari umetengenezwa kwa kuzingatia mazingira tofauti ya uendeshaji.

Kuna mambo mawili!
1.Speed
2.Torque

Ili kuondoa engine strain katika maeneo ambayo nguvu kubwa ya kusogea inahitajika (torque) mfano vilimani,kwenye matope n.k dio wakaweka gia kubwa maana engine itatengeneza nguvu kirahisi zaidi ila kwa speed ndogo. 1-2-3 ndio gia zenye torque kubwa kuliko speed.

Il kwa kuwa kuna mazingira ambayo muendeshaji atahitaji kuongeza mwendo basi kukawa na gear za nyongeza ambazo common ni 4-6! Hizi gear zina less torque na huruhusu engine huzalisha speed zaidi hasa katika maeneo ambayo ni tambarare ambapo hapaitajiki nguvu nyingi ili chombo kusogea.

Katika maboresho ya magari na kuzingatia safety & economical driving wakaona waweke dedicated button O/D or O/D off ambayo kupitia ECU itaweza kutenganisha High torque gears na Low torque gears.

Sasa kwa mujibu wa ECU ukiweka O/D maanake ume lock gearbox kwenye high torque gears 1-2-3!
Unapolazimisha speed katika O/D engine itatumia nguvu nyingi kuliko mzunguko wa matairi. Matokeo yake utapoteza mafuta mengi na kuiumiza engine bila sababu.

Utapoweka O/D maanake utakuwa umeondoa lock ya Low torque gears hivyo Speed itaongezeka kadri ya torque inavyopungua na kupungua kadri ya torque inavyoongezeka freely. Inshort engine rotation ita match na gearbox katika mazingira yote.

Hii ndio concept ya O/D on/off!

Kwa kukupa mfano halisi, kama ulishawahi kuendesha mountain bikes enzi za ukuaji. Utakumbuka ukiweka gear laini sehemu ambayo haina kilima au mchanga na ni tambarare kama kwenye lami, utatumia pumzi nyingi sana kuikimbiza baiskeli na utazungusha sana miguu hatimae kuchoka mapema tofauti na ungeitumia ukiingia kwenye dimbwi la maji,kilima, tope au mchanga!

Reason behind: Lami ni Less torque area. Hivyo kuweka high torque gear au gia laini (Jembe dogo) kutakuchosha haraka maana utapiga mizunguko mingi ya pedeli ili kusogea umbali mdogo.

Ila endapo utabadili gia na kuweka low torque gear au gia ngumu (jembe kubwa) kwenye lami basi itatumika nguvu kidogo ila baiskeli itakamata mwendo haraka sana.

Faida za kutumia O/D off ni kwenye engine braking. Mfano unataka kupunguza speed kwenye mteremko mkali. Wale ndugu zangu wa Rombo na Usangi watanielewa kirahisi.

Ukiweka overdrive off ghafla. Engine haitaruhusu speed zinazozidi gear ya 3 hivyo mzunguko wa matairi unakuwa limited kwa speed ya tatu in most cases 55km/h au chini ya hapo!

Kwahivyo kwa mtu ambaye gari imefeli brakes ama tairi zimepasuka akiwa speed kubwa sana inaweza kuwa nafuu kwake ku control gari maana itapunguza speed kwa haraka mno kisha ataweza kushika brake gari isimame kirahisi.

NB: Katika mwendo mkali huwa kuna muda breki zinapata moto sana na zina tendency ya kugoma kushika hasa kama ni mtu wa kushindilia mguu kati.
 
Hapo kwenye kuovertake pako sahihi kweli!!? Unless mi sijaielewa hyo OD maana yake.
Ku overtake huwezi zima overdrive mkuu! Huyu jamaa huenda hajui concept behind O/D!

If you need more torque then zima kidogo halafu washa, hii ni incase una overtake kwenye muinuko. Ila kama pako tambarare au mteremko we gandamiza mguu tu kama gari iko vizuri itaitika.
 
Watu wakifuata maelezo ya mleta mada watapotea kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…