Sio wewe tuu pakee yako wasio jua matumizi ya OD.. tupo wengi[emoji1][emoji1]
Mie sio kama sijui mkuu, ila mfumo wa gear katika gari umetengenezwa kwa kuzingatia mazingira tofauti ya uendeshaji.
Kuna mambo mawili!
1.Speed
2.Torque
Ili kuondoa engine strain katika maeneo ambayo nguvu kubwa ya kusogea inahitajika (torque) mfano vilimani,kwenye matope n.k dio wakaweka gia kubwa maana engine itatengeneza nguvu kirahisi zaidi ila kwa speed ndogo. 1-2-3 ndio gia zenye torque kubwa kuliko speed.
Il kwa kuwa kuna mazingira ambayo muendeshaji atahitaji kuongeza mwendo basi kukawa na gear za nyongeza ambazo common ni 4-6! Hizi gear zina less torque na huruhusu engine huzalisha speed zaidi hasa katika maeneo ambayo ni tambarare ambapo hapaitajiki nguvu nyingi ili chombo kusogea.
Katika maboresho ya magari na kuzingatia safety & economical driving wakaona waweke dedicated button O/D or O/D off ambayo kupitia ECU itaweza kutenganisha High torque gears na Low torque gears.
Sasa kwa mujibu wa ECU ukiweka O/D maanake ume lock gearbox kwenye high torque gears 1-2-3!
Unapolazimisha speed katika O/D engine itatumia nguvu nyingi kuliko mzunguko wa matairi. Matokeo yake utapoteza mafuta mengi na kuiumiza engine bila sababu.
Utapoweka O/D maanake utakuwa umeondoa lock ya Low torque gears hivyo Speed itaongezeka kadri ya torque inavyopungua na kupungua kadri ya torque inavyoongezeka freely. Inshort engine rotation ita match na gearbox katika mazingira yote.
Hii ndio concept ya O/D on/off!
Kwa kukupa mfano halisi, kama ulishawahi kuendesha mountain bikes enzi za ukuaji. Utakumbuka ukiweka gear laini sehemu ambayo haina kilima au mchanga na ni tambarare kama kwenye lami, utatumia pumzi nyingi sana kuikimbiza baiskeli na utazungusha sana miguu hatimae kuchoka mapema tofauti na ungeitumia ukiingia kwenye dimbwi la maji,kilima, tope au mchanga!
Reason behind: Lami ni Less torque area. Hivyo kuweka high torque gear au gia laini (Jembe dogo) kutakuchosha haraka maana utapiga mizunguko mingi ya pedeli ili kusogea umbali mdogo.
Ila endapo utabadili gia na kuweka low torque gear au gia ngumu (jembe kubwa) kwenye lami basi itatumika nguvu kidogo ila baiskeli itakamata mwendo haraka sana.
Faida za kutumia O/D off ni kwenye engine braking. Mfano unataka kupunguza speed kwenye mteremko mkali. Wale ndugu zangu wa Rombo na Usangi watanielewa kirahisi.
Ukiweka overdrive off ghafla. Engine haitaruhusu speed zinazozidi gear ya 3 hivyo mzunguko wa matairi unakuwa limited kwa speed ya tatu in most cases 55km/h au chini ya hapo!
Kwahivyo kwa mtu ambaye gari imefeli brakes ama tairi zimepasuka akiwa speed kubwa sana inaweza kuwa nafuu kwake ku control gari maana itapunguza speed kwa haraka mno kisha ataweza kushika brake gari isimame kirahisi.
NB: Katika mwendo mkali huwa kuna muda breki zinapata moto sana na zina tendency ya kugoma kushika hasa kama ni mtu wa kushindilia mguu kati.