Boney E.M.
JF-Expert Member
- Jan 22, 2007
- 425
- 36
Waingereza wanaagiza sana magari ya Kijapani, na kuna website nyingi tu ambazo zinazozungumzia hayo magari kiufundi pamoja na tafsiri ya user manuals zilizoandikwa Kijapani. Kwa mfano mimi nimefaidika sana kuhusu matumizi ya Pajero yangu kutoka katika hii site.Mara nyingi magari haya ya Kijapani au penginepo tunaagiza yaliokwisha kutumika hivyo kupata complete set ya manuals au booklets ni vigumu. Vipo vi gadget vingine watu hawajajua matumizi yake. Better uwasiliane na manufacturrer.
Kuwa makini:
(a) Kuna magari mengine taa zake za OD zinapowaka zinaashiria kuwa OD iko OFF.
(b) Kama unatumia Autotransimission, usitumie OD kwa safari za mjini ambapo unagemea kusimamasima mara kwa mara. Kufanya hivyo, utachakaza transimission yako haraka sana kwa sababu itakuwa inaruka kutoka gia ya kwanza hadi ya tano na kurudi gia ya kwanza kwa muda mfupi, jambo ambalo siyo zuri kwa hizi autotransimission. Ili uelewe jambo hilo, hebu fikiria kama unadandia mwamba wa juu wa goli; mwamba ule utapinda kidogo kabla ya kunyooka tena na kutulia. Sasa kama utaudandiadandia mwamba ule harakaharaka kwa kujirudiarudia basi baadaye mwamba unaweza kupinda kabisa usinyooke tana na hata kuvunjika.
Sielewi kwa Dar es Salaam bei zikoje, ila kwa jumla gharama za matengenezo ya autotransmission huwa ni kubwa sana.
Mbalamwezi thank you, umenipa darasa la haja leo maana wengine hivyo vibutton huwa tunaviona saaa ingine hata hujui faida na hasara zake , asante sana mkuuuKeizer, Ndege ya Uchumi salaam!
Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.
Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita motakaa nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe motakaa yako inakuwa umepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka uklisha maliza tena matumizi yake.
Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.
Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.
Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
Lughua, Huzaliwa, Hukua na Hufa vile vile
Nimekuwa kwenye kipindi kigumu hasa kuhusu namna ya kutumia button ya overdrve kwenye gari yangu.
Kuna mtu mmoja aliniambia niiache ikiwa inachungulia kidogo nje na kwenye dash board iwake taa inayosema overdrive off ndio matumizi sahii,
mwingine pia akanipa ushauri kuwa niitumbikize ndani na kwenye dash board kitaa kisiwake hapo ndio ntakuwa nimeitumia vyema.
Lakini hawa wote waliokuwa wananipa maelekezo hayo sio wataalam wa magari na wanasema wameelekezwa eitha na jamaa zao au marafiki.
Wanajamii wenye ujuzu haswa wa magari, naombeni msaada wenu, nisije nkakaharibu kagari kangu kabla hata sijakafaidi kiasi cha kutosha
mzee ulipotea kweli!stimu za jf ni kama zimekufa kabisa kwako TANGU INVIZIBO AKUPE BANBujibuji,
Ushauri wangu ni huu:
Tafuta user guide ya aina ya gari yako then soma maelezo ya kina ya jinsi ya kutumia gari hiyo. You can google and have information you want at your disposable. Mambo mengi yameandikwa ni kuwekeza muda wa kusoma tu, ndiyo unachohitaji.
(Ni bora yule anayekupa nyavu na kukufundisha kuvua kulikoni anayekuletea samaki)