Fahamu kuhusu meditation/tahajudi

Themann

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2022
Posts
3,842
Reaction score
16,058
Watu mbalimbali wamekuwa wakianza
kupata ufahamu juu ya meditation na wengine tayari wameshaanza kujifunza kufanya kitendo kicho. Meditation ni kitedo cha muhimu kwani kina faida kubwa na wengi waliojitolea muda wao kujifunza meditation (mfano mimi), wamenufaika na meditation. Nimeona nielezee katika post hii na ninaamini itawasaidia wengi wambao wangependa kujua.

Kwanza kabisa, kabla ya kufanya meditation ni kufahamu lengo la meditation ni nini, ni muhimu ukufahamu akili ni nini, inafanyaje kazi, energy zinazomzunguka mtu, utambue vyema baadhi ya maelezo ambayo yatasaidia mtu kujua uelewa kidogo kuhusu meditation. Kutambua hivyo itakusaidia kufahamu jinsi meditation inavyofanya kazi katika ufahamu.

Tukianza na sababu ya meditationa ni kuweza kufahamu akili yako inavyofanya kazi, kujiepusha na mateso/shida ndogondogo, huepusha hasira, hukupa uwezo mkubwa wa kuwa m'bunifu mfano kama wewe ni mchoraji, mwanamuziki n.k, inakusaidia kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yako. Na kama utaweza kuwa na maamuzi mazuri katika choices mbalimbali katika maisha itakusaidia sana kwani msingi wa maisha ni choices tunazoweka kila siku na kila saa. Ukishaweka nia sahihi juu ya meditation kinachofuata ni kufahamu nini kinatakiwa kiwepo kabla ya kufanya meditation.

Pia katika imani nyingine kama Wahindi na Wabudha, viongozi wao wa imani wanapata nguvu ya kiimani, ufahamu na wanafunuliwa jicho la tatu kupitia meditation. Hata sayansi nayo inaamini Enlightenment inaweza kutokea katika meditation na kumfanya mtu afunguke kiimani. Meditation inabadili mpaka DNA na kumpa mtu enlightenment (Ipo siku nitaelezea experience/hali ya enlightenment inakuwaje).


Kuandaa Sehemu ya Meditation
Andaa sehemu nzuri na maalum ambayo utakuwa unafanya meditation. Mfano inaweza ikawa chumbani unapolala, chagua sehemu au eneo ambalo utakaa chini vyema bila usumbufu, penye hewa nzuri na safi (fresh air), penye hali ya hewa cool au ya kawaida. Ni vyema kuchagua sehemu ambayo hauitumii kwa shughuli nyingine au mfano ukiwa haupiti sana eneo hilo au huweki vitu unavyotumia eneo hilo. Ni kwa sababu itapunguza kuwazawaza pale utakapokuwa unataka kunyamazisha akili, inaepeusha kumbukumbu za eneo hilo kuja wakati wa meditation, pia ni vyema kwani meditation ni kama sala, ni kitendo kisafi hivyo ni vyema eneo la kufanyia sala na meditation kuwekwa katika hali nzuri.

Ukishachagua eneo unaweza ukaweka vitabu vyako vya imani katika eneo hilo, inategemeana na imani yako. Halafu ukishamaliza kinachofuatia tafuta mto wa kukalia ambapo utaukalia. Tafuta mto mzuri ambao ukiukalia hautaumia (kwani utakuwa unakaa kwa muda mrefu). Halafu tafuta nguo za kuvaa ambazo hazibani na zilizo comfortable. Chagua wakati maalumu ambao utakuwa unameditate. Ni vyema kutumia dakika 20 na kuendelea katika kumeditate. Pia meditate kila unapoamka na kila kabla ya kulala. Baadaye utakapoweza kumeditate vyema utaweza hata kumeditate kwa dakika moja katika kila lisaa.
Ukishajianda hivyo kinachofuatia ni kukaa na kumeditate.

Huo ni mkao mzuri katika meditation kwani una faida zifuatazo.
Unakusaidia damu kuzunguka maeneo ya juu ambapo ndipo sehemu zenye umuhimu katika meditation, zinasababisha energy kutoka kwenye dunia kupitia kwenye uti wa mgongo na kukupa utulivu wakati wa meditation, pose linasaidia chakula kumeng'enywa vyema kutokana na damu kuwepo katika utumbo mdogo vyema. Ni mkao mgumu kukaa, mwanzoni miguu huwa inakufa ganzi kutokana na kubanwa lakini amini nakwambia ukijilazimisha baada ya muda mfupi maumivu yanaisha kabisa na unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuumia kabisa.
Kuanza meditation

Ukiwa umeshakaa, kinachofuata ni kuanza meditation. Ukishakaa, relax hakikisha kila kiuongo kimerelax, unganisha mikono yako ubebane pamoja, hisi upendo mwilini mwako, shukuru kwa afya uliyonayo, shukuru kwa jinsi mwili unavyokulindia roho yako iliyohifadhiwa na mwili, hisi furaha, peace, and love within. Halafu vuta pumzi kubwa tano. Vuta pumzi ndani taaaaratibu, halafu pause kidogo then toa pumzi njee TAARATIBU TENA. Wakati huo weka mawazo kwenye pumzi. Baada ya kuvuta pumzi kubwa tano endelea kuvuta pumzi kikawaida huku ukiweka akili kwenye pumzi inavyoingia na kutoka.

Unaweka akili kwenye pumzi kwa lengo la kutoweka akili kwenye mawazo. Akili ya mwanadamu haiwezi kukaa bila mawazo. Unapomeditate unaweka wazo kwenye pumzi tu, unaangalia jinsi pumzi inavyoingia na kutoka na kufeel energy inayoingia na kutoka mwilini. Uwe umefunga macho.

Ni vigumu kwa mara za mwanzo kwa sababu, ni vigumu kutuliza akili katika wazo moja kwa muda mrefu ila we jitahidi kufocus kwenye pumzi tu. Baada ya muda, wakati hauwazi wala haufuati kinachokuja akilini ukiwa unaweka mawazo yako katika kutazama tu jinsi pumzi inavyoingia na kutoka mwilini utaanza kuhisi umeme unakuzunguka mwilini, au kichwa kinakuwa kizito, au umeme unapanda na kushuka kwenye uti wa mgongo na utaanza kuhisi mwili mzima umerelax, hapo utakuwa katika hisia ya meditation. Ni hisia nzuri maana zinakufanya unarelax na mwili unajitengenezea umeme wake.
 
Sitaki… mwisho upotee
Ubaki wanakutafuta duniani na akhera hujafika 😂
Huwezi kupotea, kwenye meditation tunenda kihisia mpaka kwenye bustani nzuri tunatulia hapo, mtu mbili tu...
 
Hii kitu huwa natamani nijaribu kufanya ila nasikia unaweza kupitiliza mazima huko ahera madukani
 
Mmh ipo siku isiyojulikana nitajaribu
 
Pindi ninapoona mauza uza kama haya yanazidi kupamba moto, nabaki nikijisemea tu Rakims ulaumiwe huko uliko!

Nilifanya tahajudi ya pumzi

Nilifungua jicho la tatu ingawa halikuwa dhumuni langu

Mimi kweli ni mtu wa kuona vitu vya ajabu kweli? [emoji3064]

Jicho lifunguke pasi na mimi kuhitaji, nione yasiyoeleweka halafu mwisho wa siku nizinduke nijikute katikati ya watu[emoji3064]

Hivi mimi ni wa kuishi maisha mawili mawili kweli?[emoji3064]

Hivi mimi ni wa kupata OBE? Kuelea elea juu juu wakati ninapopatwa na usingizi?[emoji3064]

Hivi mimi ni wa ku undergo astral projection ya bila kuona mwili?[emoji3064]

Hivi mimi ni wa kupata lucid dreams za bila mpangilio?[emoji24]

Ubaya wa haya ma vitu, ukifahamu kimoja, utajikuta unatamani kujua yote! Na ukielewa yote, umekwisha!

Mimi ni mtu wa kuogopa ndani kweli?[emoji3064]

Hivi mimi ni mtu wa kutembea huku naelea elea![emoji24]

Meditation
Lucid dreaming
Astral projection

Sivihitaji tena katika maisha yangu, unaweza sahau kama kuna kuchakata mbususu!

Bora nichakate mbususu tu!!

Em Mshana Jr njoo useme kitu!
 
mhhh
 
Ndugu, naomba utuelezee kiundani. Ushaniogopesha hapa. Mtu mzima unaogopaje ndani mwako?
 
Ndugu, naomba utuelezee kiundani. Ushaniogopesha hapa. Mtu mzima unaogopaje ndani mwako?
Ukifikia high stage ya meditation, kuna moto utauskia mgongoni upande wa chini ambao utapanda kuja juu! Hapo utakuwa umefungua chakras (kwa wanavyodai)

Kuna roho utaanza kuziona!

Ndugu, mchezo huu ni kama punyeto, ingawa unakuathiri huku unaona, ila utakuwa unaufanya sana!

Mwisho wa siku utaona kuwa wewe na maisha ndio basi tena!

Asikudanganye mtu eti meditation inatuliza akili! Ni bora ulale ndani hata siku 2 mfululizo kuliko kufanya huu ujinga!

Yaliniathiri sana, Rakims ulisababisha niwe psychologically affected! Namshukuru Mungu hata hizi ndoto za lucid zimekoma kabisa!

Narudia tena! Ni hatari!
 
Cc Therealmike25 mbona unawaeleza tu faida za meditation na unasahau kuwaeleza kwa kina hasara zake? Hujui kuwa ukiwa na uwezo wa kuihisi na kuiskiliza pumzi yako kwa umakini unamuamsha mungu wa kike, Goddess? Ambaye yuko kwenye hiyo chakras inayounganisha mgongo kwa upande wa nyuma chini, sehemu za siri na nyayo za miguu? Mbona umekaa kimya ukashindwa kuwaeleza madhara watakayopata kama huyo Mungu wa kike ataamka? Mbona huwaelezi kuwa kuna kitu kinaitwa ulimwengu wa kiroho wenye vitu vya ajabu wataanza kuuona? Mkuu, waeleze kuhusu jicho la tatu, hiyo chakras iliyoko kwenye paji la uso!

Ubaya wa meditation ukiifanya, utakuta unatamani kufanya na yoga, na utakapoziunganisha zote, umekwisha!
Sikuona faida nyingine pasi na kusoma aura za watu tu! Hasara ni nyingi mno, mie sio mtu wa kunikutanisha na roho zilizokufa kitambo eti zizungumze na mimi!

Tena ngoja nitengeneze uzi niyaelezee haya yote kiundani zaidi!

Achana na hivi vitu kwa amani ya moyo wako:
•meditation
•yoga
•austral projection
•lucid dreaming technics

Na ushetani mwingine wa kujitizama kwenye vioo kiroho!
 
Yaliniathiri sana, @Rakims ulisababisha niwe psychologically affected! Namshukuru Mungu hata hizi ndoto za lucid zimekoma kabisa
Hapa naona uko responsible wewe kwa maamuzi uliyoyafanya mwenyewe na usipende pia kulaumu mtu kwa maamuzi binasfi uliyojiamulia mwenyewe....
 

Mkuu nitakuja na athari zake pia soon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…