Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Ulinzi kwenye maisha ni kitu muhimu sana ndo maana hata kwenye masuala ya Imani tunaambiwa tusome nyiradi Mbalimbali ili kuweka ulinzi kwenye nyumba na mwili wako maana mambo ya kutisha na kuogopesha kwenye huu ulimwengu ni vitu ambavyo reality.
Sasa leo nakuletea silaha ambayo inatumiwa sana na walinzi wa Rais nchini TANZANIA pamoja na Afrika kwa ujumla kwenye kulinda Viongozi Mbalimbali.
Silaha hii inaitwa Arad ni silaha nzuri ya kisasa ambayo ilitengenezwa mwaka 2019 nchini Israel kupitia Kiwanda cha IWI ambapo ndo Alama yake. Silaha hii haitumiwi na Kila mtu bali Kuna watu special ndo wanatumia silaha hii.
Silaha hii inatumiwa walinzi wa ma rais, polisi , na wanajeshi kwenye kazi maalum, vita ndo inatumiwa sana silaha hii ya kwenye mapigano ina uwezo mkubwa sana hii silaha.
Arad aka Assault rifle zimegawanyika katika makundi matatu 11.5 , 14.5 pamoja 16.5 , silaha hii ina uzito wa 2.86kg, ina uwezo wa kupiga risasi 700 mpaka 1000 kwa dakika 1.
Magazine yake inabeba risasi 30 pekee, inaweza tumiwa kwenye mazingira yoyote Yale baridi, jua Kali, matope, Mvua nk.