Fahamu kuhusu Ukungu

Mashima Elias

Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
18
Reaction score
52
Habari Wakulima na wasomaji wa makala za Kilimo.

Leo naomba tuelimishane kuhusu Ukungu.

Je Ukungu ni nini?

Ukungu sio ugonjwa kama inavyofahamika kwa walio wengi.

Wakulima wengi wanajua kuwa Ukungu ni ugonjwa unaoshambulia mazao kama nyanya, tikitimaji n.k na hata ukiwauliza dawa za kutibu au kukinga Ukungu wanaweza kukutajia, Kujua kuwa Ukungu ni ugonjwa sio tatizo kwao bali tatizo ni kutopata kufahamu vizuri kuhusu Ukungu.

Tuelimishane kidogo.
UKUNGU kwa maana rahisi ni hali ya unyevu kwenye angahewa. Mara nyingi ukungu hutengenezwa wakati hewa yenye joto inapokutana ghafla na ubaridi kwenye uso wa ardhi na kupelekea kutengeneza matone madogo ya maji yanayoning'inia hewani na wakati mwingine matone huwa makubwa yanayoonekana, hali hii ya unyevu inawawezesha viumbe hai wanaojulikana kama KUVU (Fungus) kukua na kuzaliana kwa kasi na kiwango kikubwa mno, basi Kuvu wanaozaliwa na kukua wapo wa aina mbalimbali.

Inawezekana hata neno KUVU likawa geni kwa baadhi yetu.

KUVU kwa kitaalamu (Fungus) ni jina la kisayansi limetokana na neno Fungi ambalo ni neno la kilatini. KUVU ni kiumbe hai ambacho si mmea wala mnyama, uainishaji wa kisayansi unavipanga viumbe hivi katika himaya ya pekee ndani ya Eukaryota. Katika jamii hii ya Kuvu kuna viumbe hai vikubwa kama uyoga lakini pia vidogo vyenye seli moja tu kama hamira au maungano ya seli kama koga.

Kwa mukitadha huo Kuvu ndiyo husababisha magonjwa mbalimbali kwenye mazao na Ukungu ndiyo unaowezesha maisha ya Viumbe hawa KUVU labda kuliweka sawa ni hivi UKUNGU unatengeneza hali ya unyevu ambao unawapa uhai viumbe wanaojulikana kama KUVU na Kuvu ndiyo husababisha magonjwa hayo tunayodhania kuwa ni ugonjwa wa Ukungu.

Makala ijayo nitaangazia Kuvu kwenye zao la nyanya.
Mambo muhimu ambayo katika makala ijayo tutajifunza ni kuelewa na kudhibiti Kuvu kwenye nyanya katika bustani.

1.Nitaelezea kuhusu mzunguko wa Kuvu.
2.Nitaelezea magonjwa makuu ya kuvu kwenye zao la nyanya.
3. Nitaelezea dalili za Kuvu kwenye zao la nyanya.
4.Tutaelimishana kuhusu mbinu za Kuzuia au kupunguza kuvu shambani.

Kwa ufupi, Kuvu katika zao la nyanya huishi na hupata lishe yao kutoka kwenye tishu zilizoambukizwa. Kuvu huzaa kwa spores ambayo ni miili midogo inayotawanywa na upepo, maji, au njia zingine. Spore huota na kusambaa katika miche ya nyanya yenye afya na kusababisha majani kuwa na madoadoa, kukauka au kuoza kwa mizizi, matunda na hata mmea wote.

Baadhi ya magonjwa ya kuvu kwenye zao la nyanya ni:
1. Mnyauko fusari
2. Baka jani Chelewa
3. Baka jani Tangulia

Imetayarishwa na
Mashima Elias
Afisa Kilimo
Email: mashimae@yahoo.com
 
Swali.
Kwanini madukani hakuna bactericide wakati magonjwa yanayosababishwa na bacteria yapo kibao kwa mimea
 
Swali.
Kwanini madukani hakuna bactericide wakati magonjwa yanayosababishwa na bacteria yapo kibao kwa mimea
Ni kweli mimea ina magonjwa mengi tu yanayosababishwa na bacteria, Kama ilivyo kwa wanyama wanavyopata shida za bacteria pia mimea inaweza kuteseka na viumbe hawa wadogo, Katika afya ya mimea inaaminika kuwa bacteria walio wengi wana faida nyingi ukilinganisha na hasara hususa ni bacteria wale wanaoishi kwenye udongo na wache ndiyo huleta magonjwa ya mimea hasa wale wanaobebwa na wadudu mimi nadhani pengine kutokana na umuhimu wao ndiyo maana hatuoni bactericides nyingi kwenye maduka lakini sio kwamba hazipo, bactericide zipo na mara nyingi katika afya za mimea wanatumia jina la Disfectant wale wenye Greenhouse huwa wanazitumia lakini pia Bactericide inawekwa kama kiambata katika sumu za kuua wadudu wanaosababisha magonjwa hasa yale yasababishwayo na bacteria.
 
Bado sjaridhika namaelezo yako mkuu,
Mfano,mnyauko fuzar unaotesa nyanya,migomba na mibuni husababishwa na bacteria,lakini watalaamu huwa mnasema hauna tiba.

Ingekuwa viral disease kama batobato kwenye mihogo hapo ningekubali maana virus huwa havina tiba
 
Kiongozi Mnyauko Fusari (Fusarium Wilt) siyo ugonjwa unaosababishwa na bacteria, Kiswahili kinakopa maneno ya kitaalamu, mfano fusari ni neno linatokana na neno la kitaalam Fusarium, Fusarium ni jamii ya viumbe ambao wapo kwenye himaya ya Fungi (Fangasi) na siyo bacteria, lakini upo mnyauko unaosababishwa na bacteria unajulikana kama Bacteria Wilt (Mnyauko bacteria) na wakulima wengi hawaelewi vizuri kuhusu mnyauko bacteria na Mnyauko Fusari, Mnyauko Fusari ndiyo hatari sana kwasababu vimelea vyake huhimili joto la hadi 80 Centigredi,

Lakini bacteria hawezi kuishi kwenye joto hilo, joto lake la kujidai ni 10 centigredi lakini huweza kuishi pia hata kwenye joto la hadi 37 Centgredi, Tunashauri Kung'oa kwasababu Mnyauko Bacteria ni ugonjwa unaoanzia kwenye udongo (Soil Born Disease) vivyo hivyo hata Mnyauko Fusari huanzia kwenye udongo na huingia kwenye mmea kupitia mizizi hivyo inakua ni ngumu sana kutibu kwasababu ukisumbua mizizi ni sawa na unaua mimea tu.
 
Bacterialcide zipo, ndio hizo disinfector
Na ambayo inatumika sanaa ni Chlorine na Hydrogen peroxide.

Ila tatizo ni kwamba kama ugonjwa ni soil borne disease, then uka treat soil basi utaua mpaka wale bacteria wenye faida kwa mmea.

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…