Mashima Elias
Member
- Dec 22, 2010
- 18
- 52
Habari Wakulima na wasomaji wa makala za Kilimo.
Leo naomba tuelimishane kuhusu Ukungu.
Je Ukungu ni nini?
Ukungu sio ugonjwa kama inavyofahamika kwa walio wengi.
Wakulima wengi wanajua kuwa Ukungu ni ugonjwa unaoshambulia mazao kama nyanya, tikitimaji n.k na hata ukiwauliza dawa za kutibu au kukinga Ukungu wanaweza kukutajia, Kujua kuwa Ukungu ni ugonjwa sio tatizo kwao bali tatizo ni kutopata kufahamu vizuri kuhusu Ukungu.
Tuelimishane kidogo.
UKUNGU kwa maana rahisi ni hali ya unyevu kwenye angahewa. Mara nyingi ukungu hutengenezwa wakati hewa yenye joto inapokutana ghafla na ubaridi kwenye uso wa ardhi na kupelekea kutengeneza matone madogo ya maji yanayoning'inia hewani na wakati mwingine matone huwa makubwa yanayoonekana, hali hii ya unyevu inawawezesha viumbe hai wanaojulikana kama KUVU (Fungus) kukua na kuzaliana kwa kasi na kiwango kikubwa mno, basi Kuvu wanaozaliwa na kukua wapo wa aina mbalimbali.
Inawezekana hata neno KUVU likawa geni kwa baadhi yetu.
KUVU kwa kitaalamu (Fungus) ni jina la kisayansi limetokana na neno Fungi ambalo ni neno la kilatini. KUVU ni kiumbe hai ambacho si mmea wala mnyama, uainishaji wa kisayansi unavipanga viumbe hivi katika himaya ya pekee ndani ya Eukaryota. Katika jamii hii ya Kuvu kuna viumbe hai vikubwa kama uyoga lakini pia vidogo vyenye seli moja tu kama hamira au maungano ya seli kama koga.
Kwa mukitadha huo Kuvu ndiyo husababisha magonjwa mbalimbali kwenye mazao na Ukungu ndiyo unaowezesha maisha ya Viumbe hawa KUVU labda kuliweka sawa ni hivi UKUNGU unatengeneza hali ya unyevu ambao unawapa uhai viumbe wanaojulikana kama KUVU na Kuvu ndiyo husababisha magonjwa hayo tunayodhania kuwa ni ugonjwa wa Ukungu.
Makala ijayo nitaangazia Kuvu kwenye zao la nyanya.
Mambo muhimu ambayo katika makala ijayo tutajifunza ni kuelewa na kudhibiti Kuvu kwenye nyanya katika bustani.
1.Nitaelezea kuhusu mzunguko wa Kuvu.
2.Nitaelezea magonjwa makuu ya kuvu kwenye zao la nyanya.
3. Nitaelezea dalili za Kuvu kwenye zao la nyanya.
4.Tutaelimishana kuhusu mbinu za Kuzuia au kupunguza kuvu shambani.
Kwa ufupi, Kuvu katika zao la nyanya huishi na hupata lishe yao kutoka kwenye tishu zilizoambukizwa. Kuvu huzaa kwa spores ambayo ni miili midogo inayotawanywa na upepo, maji, au njia zingine. Spore huota na kusambaa katika miche ya nyanya yenye afya na kusababisha majani kuwa na madoadoa, kukauka au kuoza kwa mizizi, matunda na hata mmea wote.
Baadhi ya magonjwa ya kuvu kwenye zao la nyanya ni:
1. Mnyauko fusari
2. Baka jani Chelewa
3. Baka jani Tangulia
Imetayarishwa na
Mashima Elias
Afisa Kilimo
Email: mashimae@yahoo.com