Fahamu kuhusu ushauri wa kuvaa barakoa mbili

Fahamu kuhusu ushauri wa kuvaa barakoa mbili

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
1618908687364.png

Mataifa mengi ya Ulaya yameanza kuwashauri Raia wake kuvaa barakoa mbili ili kuongeza umadhubuti wa kukulinda dhidi ya maambukizi ya #CoronaVirus

Je, ni Wakati gani wa kuvaa barakoa mbili

Unapotembelea duka, duka la dawa, daktari au hospitali yoyote

Katika mkusanyiko kwenye bustani pamoja na marafiki na familia ambao hawaishi pamoja nawe

Katika tukio lolote la umma ndani au nje ya jengo kama vile soko la wakulima au maandamano

Unaposafiri kwenye basi, teksi au usafiri wowote ule ambao ni wa umma

Unapotembea kwenye barabara au njaa iliyo na watu wengi
 
Upvote 0
Barakoa kiufundi au kisayansi ni hatari sana kwa afya yako na hasa unapoivaa kwa muda mrefu. Inaweza pelekea mtu kupata magonjwa kama kansa ya mapafu kwa mujibu wa tafiti za karibuni.

Lakini kikubwa zaidi ni kwamba haisaidii kupunguza maambukizi ya huu ugonjwa wa korona kwa mujibu wa tafiti nyingine ambayo ilitumia emperical data iliyofanyika huko Denmark. Na ndio maana Sweden hivi karibuni wamepiga marufuku uvaaji wa barakoa kwa kuwa hakuna msingi wa kisayansi unaoonyesha unasaidia kupunguza maambukizi.

Ni tafiti moja iliyodai barakoa inaonekana inasaidia na hii ilitumia 'Computer Model' ambayo haikuwa na empirical data kama tafiti ya Sweden.

Kuhimiza watu kuvaa barakoa umekuwa ni wa kisiasa zaidi huko Ulaya na Marekani. Kuna madaktari wengi tu wataalamu washazungumzia 'ineffectiveness' ya barakoa kwenye kuzuia maambukizi. Na Dr. Antony Fauci alishasema kuvaa barakoa ni symbolic tu na hakuna scientific data ya aina yeyote.

Kimsingi barakoa inavaliwa kisiasa mbele za kamera na hao wenye kulitaka tatizo la COVID-19 lionekane kubwa ili ajenda ya chanjo iende mbele na makampuni makubwa ya dawa ya Ulaya, Marekani, China, na Russia yapate faida kubwa. Lakini agenda ya chanjo ni kubwa zaidi hii ni mada inayoihitaji uzi wake tofauti.

Asanteni na Ushahidi wa tafiti kuhusu athari ya barakoa kiafya na kutosaidia kwake kupunguza maambukizi ni huu hapa chini:

1. Effectiveness of Adding a Mask Recommendation to Other Public Health Measures to Prevent SARS-CoV-2 Infection in Danish Mask Wearers - ACP Journals
- Hii paper ndio pekee ambayo imetumia empirical data na kuhitimisha kuwa barakoa hazisaidia kwenye kuzuia maambukizi.

2.A Week After Saying ‘Wear Two Masks’, Fauci Says It ‘Won’t Make A Difference’ - A Week After Saying ‘Wear Two Masks’, Fauci Says It ‘Won’t Make A Difference’
- Hii ni article inayoonyesha duble standanrd kwenye sula zima la mask na kuvaa mask mbili. Antony Fauci mwanzo alisema kuvaa barakoa mbili hakuna tofauti yeyote lakini akaja na kauli nyingine tofauti akihimiza watu wavae barakoa mbili bila ushahidi wowote wa kisayansi na ndio maana nasema suala la barakoa Ulaya na Marekani ni la kisiasa na limebeba ajenda nyingine (watu waharakishe kukimbilia chanjo).

3. STUDY: Long term mask use breeds microbes that infiltrate the lungs and contribute to advanced stage lung cancer - STUDY: Long term mask use breeds microbes that infiltrate the lungs and contribute to advanced stage lung cancer
- Hii ni study iliyochapishwa mwezi ikionyesha hatari ya uvaaji wa barakoa kwenye kusababisa kansa.

4. The Empirical Case For A Mask Mandate Lacks Scientific Grounding - Zerohedge

5. Sweden Bans Masks: ‘No Scientific Evidence’ They Prevent COVID. - Sweden Bans Masks: ‘No Scientific Evidence’ They Prevent COVID | Principia Scientific Intl.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom