Fahamu kuhusu utawala na Jaribio la kumpindua Rais Daniel Arap Moi (1982)

Fahamu kuhusu utawala na Jaribio la kumpindua Rais Daniel Arap Moi (1982)

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Wakenya walimpa jina la utani la ''mwenye kirungu'', Daniel Toroitich Arap Moi, rais wa pili wa Kenya aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 24 kuanzia 1978 hadi 2002. Kifimbo alichotembea nacho kila mahali, ni ishara ya uongozi katika jamii yake ya Kalenjin.

Moi alizaliwa tarehe 2 Septemba 1924 katika kijiji kidogo cha Kurieng'wo katika mkoa wa Bonde la Ufa. Jina la Toroitich linamaanisha, mwana wa mchungaji wa ngombe. Baba yake alifariki Moi akiwa na umri wa miaka minne, akalelewa na mjomba wake alimsaidia kusoma hadi kuhitimu na kupata stashahada ya ualimu.

Daniel Arap Moi alikuwa miongoni mwa Wakenya wachache walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Majimbo la serikali ya wakolini wa kiingereza mwaka 1955.

Yeye hakushiriki moja kwa moja katika vuguvugu la Mau-Mau lililochukua silaha kupigania uhuru wa Kenya mnamo miaka ya 1950, lakini alimuunga mkono kiongozi wa vuguvugu hilo, Jomo Kenyatta, na alimtembelea alipokuwa gerezani.

Kuunganisha vyama
Moi alikuwa mwanachama wa chama cha KADU (Kenya African Democratic Party), tofauti na Jomo Kenyatta aliyekuwa katika chama cha KANU (Kenya African National Union). Aliunga mkono sera ya kuwa na utawala wa kimajimbo, huku pia akijikita katika kutetea maslahi ya jamii yake ya Kalenjin na makabila mengine madogo katika taifa la Kenye lenye makabila mengi. Kwa upande mwingine, Jomo Kenyatta alitoka jamii ya Wakikuyu ambao ndio wengi nchini Kenya.

Baada ya uhuru wa Kenya mwaka 1963, Kenyatta alimshawishi mpinzani wake Moi kuunganisha vyama vyao, ukawa mwanzo wa utawala wa chama kimoja. Moi alipata nafasi katika serikali ya Kenyatta, akiwa waziri wa mambo ya ndani. Mwaka 1967, Kenyatta alimteuwa Moi kuwa makamu wake, licha ya upinzani mkali wa wasomi kutoka jamii yake ya Wakikuyu. Kenyatta alifariki mwaka 1978 akiwa na umri wa miaka 84, na Moi akarithi kiti chake.

Historische Bilder zum Mau Mau Aufstand in Kenia (Getty Images)
Wapiganaji wa Mau Mau waliupa wakati mgumu utawala wa Wakoloni Waingereza

Mwaka uliofuata, urais wa Moi ulithibitishwa katika uchaguzi, ambapo alisimama kama mgombea pekee. Mwaka 1982, aliidhinisha utawala wa chama kimoja katika katiba ya Kenya.

Ukandamizaji dhidi ya wapinzani
Tofauti na mtangulizi wake, Daniel Arap Moi alikuwa karibu na wananchi, akifanya ziara katika maeneo mengi ya Kenya. Wakati huo huo lakini alikuwa akifanya kila njia kuwapendelea watu wa jamii yake ya Kalenjin kwa vyeo na mali. Ukandamizaji wa uhuru wa habari ilikuwa mojawapo ya nembo za utawala wake.

Kufuatia jaribio la mapinduzi lililoshindwa mwaka 1982, Moi alizidisha utawala kwa mkono wa chuma. Jaribio hilo la mapinduzi la wanajeshi wa kikosi cha anga lilifuatiwa na ukandamizaji mkubwa, ambamo zaidi ya watu 120 waliuawa, na wengine zaidi ya 900 wakawekwa kizuizini. Watu 12 waliokutwa na hatia ya kuhusika katika jaribio hilo walihukumiwa kifo.

Robert Ouko (imago/Sven Simon)
Marehemu Dr Robert Ouko, mhanga wa utawala wa Rais Moi

Lakini pia Moi aliwachukulia hatua kali wakosoaji ndani ya chama chake, akimtuhumu waziri wa sheria Charles Mugane Njonjo kufanya uhaini. Baada ya kesi mahakamani, Njonjo alilazimika kujiuzulu mwaka 1983, akishutumiwa kutaka kuuangusha utawala wa Moi. Mhanga mwingine wa mkono wa Moi ni aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Robert Ouko aliyeuawa kikatili mwaka 1990, baada ya kukosoa waziwazi matumizi mabaya ya madaraka na kutaka uchunguzi ufanywe dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

Baada ya miaka 10 ya uchunguzi wa kamati ya bunge, ilibainishwa kuwa Ouko aliuliwa katika makaazi ya Rais Moi. Wakati wa uchunguzi huo, mashahidi kadhaa walikufa katika mazingira ya kutatanisha, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya kamati hiyo. Wapinzani wengine walioonja machungu ya utawala wa Rais Daniel Arap Moi ni Kennath Matiba na Raila Odinga, ambao walifungwa jela bila kufikishwa mahakamani.

Hatimaye akubali shinikizo, arejesha mfumo wa vyama vingi
Shinikizo kali la kimataifa lilimlazimisha Moi hatimaye kuridhia mfumo wa vyama vingi mwaka 1991. Mwaka 1992, Wakenya walipata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi uliovihusisha vyama vingi, lakini upinzani uliogawanyika ulikuwa neema kwa Moi, ingawa ilikuwepo pia minong'ono ya kughushi matokeo. Uchaguzi huo uliandamwa na machafuko makubwa.

Kenia Opposition Führer Raila Odinga NASA Koalition (Reuters/T. Mukoya)
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, alifungwa bila kufunguliwa mashtaka

Miaka mitano iliyofuata, Moi alishinda tena. Ingawa sehemu kubwa ya Wakenya iliunga mkono upinzani wapizani hao walishindwa kukubaliana juu ya mwakilishi mmoja wa kambi yao.

Mwaka 2002 Moi alikosolewa vikali pale alipojaribu kuahirisha uchaguzi wa bunge kwa sababu ya mazungumzo juu ya katiba mpya, akiwa na azma ya kuendelea kukaa madarakani. Kikatiba alikuwa haruhusiwi kugombea tena, na uchaguzi ulifanyika kama ilivyopangwa. Alisababisha pia mvutano mkali ndani ya chama chake kwa kumchagua mtoto wa mtangulizi wake, kijana Uhuru Kenyatta ambaye hakuwa na uzoefu, kama mgombea wa chama cha KANU.

Mkakati wake wa kutaka KANU iungwe mkono kwa sababu mgombea wake alitoka jamii ya Wakikuyu walio wengi uliambulia patupu, na ilichukua miaka mingine 11 kwa Uhuru kuingia Ikulu.

Utawala wa miaka 24 wa Daniel Toroitich Arap Moi ulifika kikomo tarehe 30 Desemba 2002. Urithi aliouacha wa ukabila na ubadhirifu unaiandama Kenya hadi wa leo.

=======================

Jumamosi tarehe 1 Agosti 1982 kundi la wanajeshi wa anga walivamia kituo cha redio ya Sauti ya Kenya wakidai kuwa wamepindua serikali. Kiongozi wao alikuwa Hezekiah Ochuka afisa wa ngazi ya chini akishirikiana na wenzake. Tangazo lao lilikuwa: "Serikali ya Kenya imepinduliwa na majeshi na sasa iko mikononi mwa majeshi. Viongozi wetu wamekuwa watu wafisadi wenye matumbo makubwa wasiojali maskini."

Tangazo lilisababisha watu wengi kuandamana mjini na kupora maduka wakilenga hasa raia wa asili ya Kihindi mjini Nairobi. Imekadiriwa ya kwamba zaidi ya maduka 1,000 yaliporwa na nyumba za Wahindi zilivunjwa na wanawake wao kunajisiwa.

Jeshi la ardhi na polisi wakandamiza uasi
Jaribio la mapinduzi halikudumu muda mrefu baada ya jeshi la ardhi pamoja na polisi kuingia kati na kukandamiza uasi baada ya masaa sita tu. Rais Moi alikuwa nje ya Nairobi na mipango ya kurusha mabomu kwa nyumba yake huko Kabarnak haikutekelezwa.

Hezekia Ochuka alikamata ndege akakimbilia Tanzania alipokamatwa na kurudishwa Kenya baadaye alipopelekwa mahakamani na kunyongwa baadaye kama msaliti.

Sababu za uasi
Idadi kubwa ya viongozi wa uasi walikuwa wanajeshi kutoka kabila la Waluo. Inaonekana ya kwamba jaribio lilisababishwa na azimio la Bunge la Kenya la tarehe 9 Juni 1982 lililofanya Kenya kuwa nchi ya chama kimoja. Sheria hii ilizuia jaribio la kiongozi wa Kiluo Jaramogi Oginga Odinga kuanzisha chama cha upinzani.

Yaliyofuata
Uasi ulisababisha ukandamizi mkali. Polisi ilipita katika nyumba za askari wa anga pia katika mitaa ya vibanda ambako maelfu walikamatwa. Jeshi la anga lilifutwa. Jumla la watu 145 waliuawa ama na waasi au baadae katika ukandamizi wake.

Viongozi wa Waluo walikamatwa pia; Jaramogi Odinga alifungwa katika nyumba yake na kushtakiwa lakini mashtaka yaliondolewa baadaye lakini mwanae Raila Odinga alifungwa jela kwa miaka sita hata bila kuhukumiwa.

Kwa jumla siasa ya rais Moi ilibadilika kuwa ya kidikteta baadaye na polisi ilipewa mamlaka pana kutafuta wapinzani hata kuwatesa na kuwakamata bila kuwapeleka mahakamani.

Chanzo: Wikipedia
 
kwanni wanaofanya majaribio hawajipangi kisawasawa tumeshuhudia kwa Jen. Niyombare

Gen Niyombare alikuwa anasumbuliwa na tumbo aka njaa, yule alipewa faranga na nchi flani ambayo inataka kuona Burundi wanakuwa kwenye machafuko ama kuona Burundi wanakuwa na rais kibaraka ili yeye huyo jamaa atumie Burundi kama lango lake kuu la kuingilia DRC kuchota madini. Fanya uchunguzi wako utagundukua kuwa hata hayo maandamano hayana lolote yapo tu mji mkuu wa nchi.

Shida ni kwamba Warundi wana njaa sana sasa wakisikia hata mluzi unapigwa mkoani basi wale wa wilayani inabidi wakimbilie nchi za jirani kuomba hifadhi ya wakimbizi angalau wale vyakula vya bure vya UN but honest speaking there is no reason of whatsoever to have influx of Burundian refugee in Tanzania maana hayo maandamano unayoyasikia yapo Bujumbura sasa Warundi walioko mipakani na mbali kote huko kwa nini wanakuja Tanzania kuwa wakimbizi,jibu ni rahisi tu ni kwamba Warundi wana njaa kali, Warundi hawana ardhi so wanaona bora waje kwenye makambi wakafe kwa cholera kuliko kukaa kwao wanakokufa kwa njaa.
 
Mkuu bornagain

Ukitazama kwa makini mapinduzi ya Burundi na maandamano yanayoendelea kwa kiasi kikubwa yanachochewa na umasikini uliotamalaki Burundi hii unaweza kusema ni sababu ya ndani (internal) ambvazo zinachagizwa zaidi na sababu za nje (external).

Bila ya kuwepo sababu za nje (externals) sababu za ndani hakika zisingekuwa na nguvu tuliyoiona.Ni hivi Burundi kwa muda mrefu imekuwa ikitawaliwa na na watutsi wachahche 15% huku kabila kubwa la wahutu 85% wakitengwa katika utawala.Jambo hili lilianzishwa na wakoloni na likaachwa kuendelea mpaka leo.Kabla ya makubaliano ya Arusha jeshi la Burundi lilikuwa likimilikiwa na watutsi tu so hata Rais anapokuwa mhutu inakuwa vigumu sana kuitwala Burundi iliyotamalakiwa na watutsi wachahche lakini wenye usemi mkubwa katka nyanza zote za utawala hasa kijeshi.Baada ya makubaliano ya Arusha jeshi la Burundi ikabidi lipokee waasi (wahutu) so nguvu za watutsi zikaanza kupungua kadri siku zinavyosonga mbele.Unaweza kusema kipindi cha utawala wa Nkurunziza kilishuhudia wahutu wengi wakiingizwa jeshini balance ikaanza kuwepo.Kama jeshi lingebakia kama zamani hakika Nkurunzinza asingeweza kurejea Bujumbura baada ya kupinduliwa akiwa Dar kwenye mkutano wa viongozi wa EAC.

Sababu za nje ni wazi Rwanda ya Kagame mtutsi inakerwa na hali ya mambo ya Burundi hasa utawala wa Nkurunzinza mhutu ingawa mama mtutsi.Hali ya Burundi haina tofauti na hali ya Rwanda kwa maana makabila ya watutsi wachache na wahutu wengi.Rwanda inakadiriwa watutsi wapo chini 15% lakini ndio walioshika uchumi wa Rwanda katika sekta zote.Jeshi la Rwanda RPF watutsi ni 90% sasa hapo akitokea Rais mhutu unategemea nini hasa ukizingatia uhasama wa kikabila baina ya makabila mawili?

Kagame anataka Burundi inayoongozwa na mtutsi ambayo itaweza kumsaidia katika harakati zake za kusimika utawala wa himaya ya kitutsi (Hima empire) Nkurunzinza ni kikwazo kikubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii dhidi ya maslahi ya watutsi.Nkurunzinza ni kikwazo kwa ajenda za Rwanda,Uganda na Kenya katika jumuiya ya Afrika Mashariki.Mara zote Burundi imekuwa ikisimama na kuunga mkono serekali ya Dar hata kwa mambo ambayo yangeweza kuisaidia Burundi yenyewe.

Kuondoa utawala wa Nkurunzinza kungeifanya serekali ya Kigali kupumua na kuiweka katika wakati mgumu Tanzania hasa linapokuja suala la utangamano wa EAC.Usishangae ni kwanini Dar iliangaika sana serekali ya Bujumbura ilipopinduliwa.

Gen Niyombare alikuwa anasumbuliwa na tumbo aka njaa, yule alipewa faranga na nchi flani ambayo inataka kuona Burundi wanakuwa kwenye machafuko ama kuona Burundi wanakuwa na rais kibaraka ili yeye huyo jamaa atumie Burundi kama lango lake kuu la kuingilia DRC kuchota madini. Fanya uchunguzi wako utagundukua kuwa hata hayo maandamano hayana lolote yapo tu mji mkuu wa nchi.

Shida ni kwamba Warundi wana njaa sana sasa wakisikia hata mluzi unapigwa mkoani basi wale wa wilayani inabidi wakimbilie nchi za jirani kuomba hifadhi ya wakimbizi angalau wale vyakula vya bure vya UN but honest speaking there is no reason of whatsoever to have influx of Burundian refugee in Tanzania maana hayo maandamano unayoyasikia yapo Bujumbura sasa Warundi walioko mipakani na mbali kote huko kwa nini wanakuja Tanzania kuwa wakimbizi,jibu ni rahisi tu ni kwamba Warundi wana njaa kali, Warundi hawana ardhi so wanaona bora waje kwenye makambi wakafe kwa cholera kuliko kukaa kwao wanakokufa kwa njaa
 
Last edited by a moderator:
Wakikuyu ndio walisababisha like jaribio,tukirudi katika historia,tuna ambiwa kwamba Kenyatta aliingia msituni kupigania uhuru wa wa Kenya.

Wakina Jaramogi wao walitumia njia za mwalimu nyerere kumuondoa mkoloni bila kumwaga damu,ikafikia hatua Kenyatta alikamatwa na kufungwa,wenzake wakina odinga waliendelea na harakati za ukombozi. Ikafikia hatua mkoloni akakubali kuachia ngazi na jaramogi awe waziri mkuu,lakin kwa kuwa mwenzio Kenyatta alikuwa bado yupo korokoroni wakasema bila Kenyatta kuachiwa huru no Uhuru.

Wakoloni wakamuachia Kenyatta,wakapata Uhuru,hapo ndipo true colors za mkikuyu zikaanza kuonekana.
alianza kuwagawia na kujimikikisha madhamba makubwa makubwa na pia kuwapa nafasi kubwa kubwa serikalini wakikuyu wenzake.

Hapo ndipo ukabila ulipoanzia. I stand to be corrected
 
I stand to be corrected

Sasa wamaanisha Wakikuyu ndio chanzo cha ukabila Kenya?
 
Mkuu bornagain

Ukitazama kwa makini mapinduzi ya Burundi na maandamano yanayoendelea kwa kiasi kikubwa yanachochewa na umasikini uliotamalaki Burundi hii unaweza kusema ni sababu ya ndani (internal) ambvazo zinachagizwa zaidi na sababu za nje (external).

Bila ya kuwepo sababu za nje (externals) sababu za ndani hakika zisingekuwa na nguvu tuliyoiona.Ni hivi Burundi kwa muda mrefu imekuwa ikitawaliwa na na watutsi wachahche 15% huku kabila kubwa la wahutu 85% wakitengwa katika utawala.Jambo hili lilianzishwa na wakoloni na likaachwa kuendelea mpaka leo.Kabla ya makubaliano ya Arusha jeshi la Burundi lilikuwa likimilikiwa na watutsi tu so hata Rais anapokuwa mhutu inakuwa vigumu sana kuitwala Burundi iliyotamalakiwa na watutsi wachahche lakini wenye usemi mkubwa katka nyanza zote za utawala hasa kijeshi.Baada ya makubaliano ya Arusha jeshi la Burundi ikabidi lipokee waasi (wahutu) so nguvu za watutsi zikaanza kupungua kadri siku zinavyosonga mbele.Unaweza kusema kipindi cha utawala wa Nkurunziza kilishuhudia wahutu wengi wakiingizwa jeshini balance ikaanza kuwepo.Kama jeshi lingebakia kama zamani hakika Nkurunzinza asingeweza kurejea Bujumbura baada ya kupinduliwa akiwa Dar kwenye mkutano wa viongozi wa EAC.

Sababu za nje ni wazi Rwanda ya Kagame mtutsi inakerwa na hali ya mambo ya Burundi hasa utawala wa Nkurunzinza mhutu ingawa mama mtutsi.Hali ya Burundi haina tofauti na hali ya Rwanda kwa maana makabila ya watutsi wachache na wahutu wengi.Rwanda inakadiriwa watutsi wapo chini 15% lakini ndio walioshika uchumi wa Rwanda katika sekta zote.Jeshi la Rwanda RPF watutsi ni 90% sasa hapo akitokea Rais mhutu unategemea nini hasa ukizingatia uhasama wa kikabila baina ya makabila mawili ?.Kagame anataka Burundi inayoongozwa na mtutsi ambayo itaweza kumsaidia katika harakati zake za kusimika utawala wa himaya ya kitutsi (Hima empire) Nkurunzinza ni kikwazo kikubwa kiuchumi,kisiasa na kijamii dhidi ya maslahi ya watutsi.Nkurunzinza ni kikwazo kwa ajenda za Rwanda,Uganda na Kenya katika jumuiya ya Afrika Mashariki.Mara zote Burundi imekuwa ikisimama na kuunga mkono serekali ya Dar hata kwa mambo ambayo yangeweza kuisaidia Burundi yenyewe.

Kuondoa utawala wa Nkurunzinza kungeifanya serekali ya Kigali kupumua na kuiweka katika wakati mgumu Tanzania hasa linapokuja suala la utangamano wa EAC.Usishangae ni kwanini Dar iliangaika sana serekali ya Bujumbura ilipopinduliwa.

Mkuu nimekusaluti yaani umemaliza kila kitu hujamung'unya maneno, upo vizuri sana
 
Asante kaka, ila nimeona Nyerere aliwasamehe wote na kuwapa kazi za ubalozi, kweli alikua na roho mzuri maana wetu Moi aliwanyonga tu.

Sio hivyo tu. Mwalimu alimtuma Waziri wa ulinzi wakati huo aongee na baadhi ya Watuhumiwa. Na moja ya maswali ni kutaka kujua sababu ya msingi kwa nini walitaka kupindua.

Miongoni mwa mengine walielezea jinsi hata wapiganaji waliofariki vita ya Kagera makaburi yao yalivyosahauliwa. Baada ya miezi michache makaburi ya kaboya yalisafishwa na kuwekwa katika hali nzuri.

Kiongozi wa mapinduzi, Thomas Lugakingira yeye alipoulizwa na wanausalama maalum akiwa central police station angeifanyia nini Tanzania, aliomba kalamu, karatasi na kikombe cha kahawa akaandika kwa muda wa masaa manne nini ingekuwa sera zake.

Baadaye alitoroka lakini kuna taarifa miongoni mwa yale aliyoyaandika yalifanyiwa kazi na Serikali iliyofuata.

Kama asingemrudisha Ochuka pengine kungekuwa na mgogoro mbaya sana na Kenya, kwa sababu Kenya nayo ilikuwa na watuhumiwa wa uhaini 1984 Watanzania.
 
sasa wamaanisha wakikuyu ndio chanzo cha ukabila kenya?

Ndio manake historian inajieleza, Kenyatta alilijenga taifa katika Tanaka LA makabila. aliwajali Sana kabisa lake,hapo ndipo chuki zilipoanzia. Ni Kama Rwanda na Burundi ,wakoloni waliwapendelea Sana Watusi,ikajenga chuki miongoni mwao na Wahutu.
 
Back
Top Bottom