fahamu kwa nini baba kanumba amesema patachimbika kuhusu mgawanyo wa mali za marehemu kanumba

fahamu kwa nini baba kanumba amesema patachimbika kuhusu mgawanyo wa mali za marehemu kanumba

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Ni zaidi ya mwaka mmoja umepita toka kufariki kwa mwigizaji staa wa Tanzania Steven Kanumba, ambae aliacha kampuni ya kutengeneza filamu aliyokua akiimiliki pamoja na mali nyingine yakiwemo magari.
Baba mzazi wa Marehemu Mzee Kanumba anaeishi 87.5 Shinyanga amesema ‘kwenye mirathi tumeshirikiana na Mama Kanumba ingawa Jaji kachanganya baada ya kuwekwa watoto ambao sio wangu… mimi na mama Kanumba ni sahihi ila watoto ambao sio wangu tumeandaa Mwanasheria kuwaondoa wasiohusika na tumbo langu vinginevyo na wa tumbo langu waingie kwenye mgao wa mirathi’
‘Watoto walioshirikishwa na sio wangu ni Seth Bosco ambae ni mtoto wa shemeji yangu mdogo wake mama Kanumba, Tina Mshumbuzi, Bella Kajumulo yani haya majina unayaona yako tofauti, hawa wawili nilikuta Mama Kanumba ameshazaa.. kwa hiyo hawawezi kuingia kwenye kurithi ndio maana nafatilia Mahakama itende haki na watoto wangu waingie mule vinginevyo aisee patachimbika’ – Baba Kanumba
Kwenye sentensi ya mwisho Baba Kanumba amesema ‘Kanumba hakua na mke wala mtoto hivyo hawezi kuingia mwingine pale, mirathi ni ya watu wawili mimi na Mama Kanumba tuliemleta duniani Kanumba, sijawasiliana bado na Mama Kanumba…. tutawasiliana Mahakamani’
Baba Kanumba ambae hakuweza kuhudhuria maziko Dar es salaam kutokana na kuumwa, anasema kwenye mazungumzo ya mwisho na Marehemu siku kadhaa kabla ya kufariki, alimwambia kuhusu pesa zaidi ya milioni 50 alizokua nazo benki pamoja na nyumba aliyokua ameianza ujenzi Dar es salaam.

Kwani baba kanumba nae ni celebrity,hIi ingeenda jukwaa la sheria,nadhan wangeijadil kwa ufasaha zaidi
 
R.i.p steven kanumba. Daah kuna umuhimu wa kuandika mirathi mapema.
 
Mzee kama mngese mali sio zako unazitolea macho.ye anachagua wa kupata kama yeye ndio kanumba, wakati huo hakuwa na uhusiano mzuri na marehemu.mbwa
 
r.i.p steven kanumba. Daah kuna umuhimu wa kuandika mirathi mapema.
duh kweli majanga zee zima linaacha kufight nilataka mirathi...world is not affair i see
 
mie na swali tu STEVEN KANUMBA,BELLA KAJUMULO,TINA MSHUMBUZI ina maana mama kanumba kazaa na wanaume zaidi ya 3 tofauti??
Afu Seth Bosco jamaniii kafanana sana na marehemu mie nlijua toka nitoke baba mmoja mama mmoja
 
mie na swali tu steven kanumba,bella kajumulo,tina mshumbuzi ina maana mama kanumba kazaa na wanaume zaidi ya 3 tofauti??
Afu seth bosco jamaniii kafanana sana na marehemu mie nlijua toka nitoke baba mmoja mama mmoja
ajabu nini sasa amu....mi nataka kuza na wewee
 
Baba kanumba ana haki ya mirathi kwani ni mzazi. Kutokuelewana katika familia huwa kuko na hakukwepeki so ni mambo ya kawaida tu. Asipochukua mirathi ya mwanawe atachukua ya nani???ya mkwewe au?? mumuwache mzee wa watu kwani wakati anazaa hamkumsaidia kununua nepi.
 
mama mtu ndio aliomlea uyo baba kachangia mbegu tu,na toka mwanzo Kanumba alikuwa anampenda mama yake si baba yake
 
mama mtu ndio aliomlea uyo baba kachangia mbegu tu,na toka mwanzo Kanumba alikuwa anampenda mama yake si baba yake

Fuatilia utajua kuna kipindi kanumba alilelewa na baba yake na si mama tu, alishasema kuna kipindi alikuwa anachunga mbuzi huko msoma mama wa kambo akawa anamtesa (ila hakusema baba alimtesa). Hata hivyo yai bila sperm kuna mtoto?? au sperm bila yai kuna mtoto? mzee wa watu ana haki zote za kupatiwa mirathi. Mmama ni mjanja mjanja wa mjini ila mzee yuko imara hakipotei kitu.
 
Ni selebriti hehehe. Ameakti movie. Useless father. Sasa ndo naelewa kwa nini kanumba alimpa za uso. Opportunist!
Kwani baba kanumba nae ni celebrity,hIi ingeenda jukwaa la sheria,nadhan wangeijadil kwa ufasaha zaidi
 
mama mtu ndio aliomlea uyo baba kachangia mbegu tu,na toka mwanzo Kanumba alikuwa anampenda mama yake si baba yake

hilo ndo tatizo lenu kubwa nyi wamama,sheria ya mirathi inawatamka wazazi km warithi km marehem hakuzaa,sasa ww ukisema eti kachangia mbegu2,kwan ww ulizaliwa bla mbegu dume?!acha ding ale jasho lake coz alikunja goti vlvo ad kum2ngua mm kanumba
 
Back
Top Bottom