Fahamu kwamba Hotuba ya Rais Samia Suluhu haikugusia chochote kuhusu Katiba Mpya wala Tume Huru ya uchaguzi

Sahau kuhusu hio toka kwa mccm yeyeto.Hapo ni SAwa na kulala mlango wazi ukiamini wezi awatoingia.
Ccm haiwezi onja sumu katu
 
Sasa unataka aitaje vipi,wakati mwizi mwenyewe kajisema mahakamani nawakati huo huo hakimu anamwambia futa kauli yako wewe sio mwizi [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Punguza papara, tayari ameahidi ndani ya bunge tena through printed document kuwa atakutana na vyama vya siasa vya upinzani. Sasa huko mkienda msiishie kupiga juice na kuchekacheka.

Nendeni agenda hizo 2 muhimu za Tume huru ya uchaguzi pamoja na Katiba mpya.. Hakikisheni agenda mojawapo mnatoka na majibu ya Rais yenye timeframe.
 
Yote na yote ni heri kofia mbili zitenganishwe Ili kuzuia udikteta nchini.Rais akizingua anafukuzwa uanachama na mwenyekiti wa chama na uraisi wake unakoma hapo hapo.
 
Wacheni kazi ziendelee.
 
Kwa hiyo?
Chadema wenyewe hawaongdli tume mpya mpaka wakishindwa uchaguzi
 
Katiba mpya na Tume huru ni mwiba mkali kwa tabaka tawala.Haitakuwa njia rahisi kuvifikia.
 
Una maanisha kwamba mambo yale yale ya ukatili na utekaji bado yangalipo ?
 
Mkuu mnashindwa nini?

Mnafeli wapi ?!!!

Ingizeni kipengele cha KATIBA MPYA katika ilani yenu ya uchaguzi 2025.....

Wananchi wanaotaka KATIBA MPYA huwenda wakawachagua na sisi tusiotaka hiyo KATIBA tukashindwa!

#KaziIendelee
 
Mkuu mnashindwa nini?

Mnafeli wapi ?!!!

Ingizeni kipengele cha KATIBA MPYA katika ilani yenu ya uchaguzi 2025.....

Wananchi wanaotaka KATIBA MPYA huwenda wakawachagua na sisi tusiotaka hiyo KATIBA tukashindwa!

#KaziIendelee
Una uwezo mwembamba sana ! kwangu anayewaza kula tu kama wewe huwa namhurumia sana !
 
Una uwezo mwembamba sana ! kwangu anayewaza kula tu kama wewe huwa namhurumia sana !
🤣🤣Sawa "intelligent" RBC!

Nashukuru kwa huruma yako hiyo si jambo dogo mkuu!

Haya tunasubiri MASHINIKIZO ya kamati ya nje ya bunge la US na Amnesty Intl katika kutoka rumande kwa mh.Mbowe.....

#KaziInaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…