absolutely, upo sahihi, pia nimejifunza kua wengi wetu wanaishi bila kua na malengo wala kujua nini wanahitaji katika maisha, kuna mtu mmoja ni graduate wa sheria ila cha kushangaza alihangaika kutafuta kazi yoyote ili aweze ku survive na mwisho wa siku akaishia kua muhudumu wa super market, nikamuuliza sasa kwanini alipoteza miaka mi4 kusoma sheria? akaniambia kua alisoma kwakua alihisi akiwa mwanasheria atakua na maisha mazuri na matokeo yake kakwama na kushindwa kwenda law school ili afikie ndoto yake, pia vilevile mifumo ya elimu yetu inawaharibia watu wengi maisha kwa kuwafanya wawe watafutaji wa ajira baada ya watazamaji wa fursa na kuzifanyia kazi, mwisho wa siku tunakua na idadi kubwa ya watafuta ajira kuliko watengenezaji wa ajira wenyewe....
naamini umasikini wa mtu hauwezi isha kwa kutegemea mshahara kwakua kila mara mshahara hua hautoshi kutatua kero na mahitaji yote.
mimi naamini kila mtu ni mzuri na ana kipaji au uwezo flani wa kufanya kitu flani kwa ufanisi zaidi, ila tatizo mfumo wa malezi pamoja na elimu unawakaririsha watu kua bila kusoma sana na kuajiriwa na kulipwa mshahara hauwezi kua na maisha bora na matokeo yake imepelekea watu kurogana kugombania madaraka na kushinda kwa waganga ili ajira isiishe.
najiuliza kwanini mwanafunzi wa havard mark zukerberg alikataa ofa ya kuajiriwa na microsoft huku akiahidiwa mamilioni ya dola toka kwa bill gates na kuamua kukomaa na mradi wake wa face book? jibu ni lepesi sana aliisikia sauti ndani yake na kuifanyia kazi na matokeo yake leo ni kijana tajiri saana nadhani kuliko vijana wote wa umri wake.
kuna mtu mmoja aliwahi niuliza kwanini sitaki kuajiriwa na kwenda kufanya kazi kwenye taasisi yao? nikamjibu kua maisha ni kama maji na pia sisi nikama aina ya samaki, kuna vidagaa,samaki wa saizi ya kati na wale nyangumi sasa basi maji yangu ni marefu deep see, hivyo basi nitakomaa zaidi mpaka nifikie level ya maji yangu, na ujasiri huo niliupata baada ya kusoma vitabu vingi kama vile think and grow rich, retire young and retire rich, rich daddy and poor daddy, how to increase financial IQ na vinginevyo....
naendeleza mapambano huku nikiwa na imani kuu kua lazima nitafikia malengo yangu na kuacha legacy behind.
nachoamini ni kwamba kuzaliwa masikini sio kosa au uamuzi wa mtu bali kufa masikini ni maamuzi na makosa yetu yenyewe.
watu wengi wanafikiri utajiri ni lazima uwe na pesa kwanza kumbe unaanzia katika state of mind.
we become who we are from what we think.
nawasilisha.