JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kodi ni malipo yanayotozwa na Serikali kwa wananchi, kampuni, au taasisi zilizopo ndani ya nchi au zilizopo nje ya nchi lakini zimesajiliwa ndani ya nchi. Lengo kubwa la kutoza kodi ni kuitengenezea mapato serikali iliyopo kwa ajili ya kufikia malengo yake katika kutoa huduma za Jamii na maslahi ya wananchi kwa ujumla.
Katika utozaji wa kodi serikali inaongozwa na nadharia zifuatazo:-
Nadharia ya uwezo wa watu kulipa kodi
Hapa Serikali inabidi itoze kodi kulingana na uwezo wa wananchi kulipa kodi hiyo haitakiwi kumuwekea mwananchi kiwango ambacho hana uwezo wa kukilipa.
Nadharia ya Faida inatokanayo na kulipa kodi
Watu wanalipa kodi kutokana na faida wanazopata kutoka kwenye huduma za kijamii zinazotolewa na serikali. Huduma hizi zinatolewa kutokana na kodi wanazolipa wananchi hivyo kutokana na faida wanazopata wananchi ndivyo nao wanapata nguvu ya kulipa kodi.
Nadharia ya kujitolea kwa wananchi
Wananchi wanalipa kodi kwasababu ya kujitolea kujenga taifa Lao na kujiwekea mazingira mazuri ya kuishi kwenye Taifa Lao.
Kwa nchi ya Tanzania utaratibu wa kodi unaendeshwa kwa Sheria kadhaa kama vile Sheria ya kodi ya mapato ambapo hii inaeleza kuwa mtu analipa kodi kutoka kwenye kipato chake anachoingiza kila mwaka na kipato kinachotozwa kodi ni :-
- Kipato kutoka kwenye Ajira
- Kipato kutoka kwenye biashara
- Kipato kutoka kwenye uwekezaji
Upvote
0