Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,595
- 6,264
{Tafsiri nyepesi}
"Autopilot" ni mfumo unaoruhusu chombo cha moto kama ndege, meli, gari n .k kujiongoza yenyewe pasipo mwendeshaji kugusa kitu.
Kwa upande wa usafiri wa anga zipo baadhi ya ndege ambazo hazina mfumo huu kabisa hasa ndege ndogo kabisa zile za zamani.
"Autopilot" inasaidia kumpunguzia Rubani majukumu ya kuongoza chombo muda wote pasipo kupumzika.
Kazi kubwa na za msingi za autopilot ni:
>Kushikilia mwelekeo wa ndege {#Course_Heading}
>Kushikilia kimo cha ndege {#Altitude_hold}
>Kushikilia mwendo ambao rubani atauchagua {#Holding_speed}
Rubani atakapochagua ndege yake iwe na kasi ya 250knots, uelekeo wa nyuzi 180° na kimo cha futi 25,000 basi mfumo wa autopilot utapaa kwa kufuata amri hizo hadi rubani atakapozima na kuiongoza mwenyewe "#manual flying"
Mara nyingi ndege ikipaa tu rubani uwasha "autopilot" na kuendelea na mambo mengine ya msingi na baadae kuzima "autopilot" pale anapokaribia kutua.
Lakini pia mifumo ya "autopilot" ya kisasa ina uwezo wa kufanya mambo mengi zaidi kama ndege kupaa yenyewe hadi kufikia kimo, uelekeo na kasi aliyochagua rubani, pia hata kufuata njia/ramani ambayo rubani amechagua kupitia kwenye ngamizi ya ndege.
Inapokuwa kwenye "autopilot" rubani hana haja ya kuzima tena ili kubadilisha uelekeo, kasi au kimo bali uingiza namba za kimo, kasi au uelekeo na ndege kufuata maamuzi hayo.
FAIDA
>Kupunguza kazi na uchovu kwa Rubani hasa masafa marefu
>Uiongoza ndege kwa sahihi kuliko kuiongoza kwa mkono.
>Kupunguza ulaji mafuta kwa kuwa ujiongoza kwa unyoofu zaidi pasipo kuyumbayumba.
>Kupunguza makosa ya kibinaadamu wakati wa kuipaisha kwa mkono.
>Kumpa rubani muda wa kufanya kazi nyengine za msingi kama mawasiliano, kuhakiki njia anazopita, kukagua mifumo ya ndege kama inafanya kazi kwa usahihi, kufanya hesabu za mafuta, kuangalia hali ya hewa pengine hata kwenda msalani au kupata mlo.
HASARA
- Ingawa mara chache hutokea
> Kusahaulisha marubani ujuzi wa kupaisha ndege kwa mkono hasa inapotokea dharura.
> Ni mfumo unao ongozwa na ngamizi (Computer) hivyo mara nyingine upata hitilafu na kupelekea ndege kwenda isivyokusudiwa
> Rubani kupitiwa na usingizi
Katika nyingi sasahivi mfumo wa vitufe vya autopilot {#autopilot_console} vipo mbele ya rubani, vifufe vya mawasiliano {#Communication_panel} vinakuwa chini na vitufe kuhusu umeme wa ndege vinakuwa juu {#overhead_panel}.
Tunawakaribisha wataalamu kuongeza, kupunguza au kuondoa makandokando kwa faida ya wasomaji wetu.
Crdt: Aviation Media Tanzania.