Kwenye meli au boti mfumo wa autopilot ulikuwa msaada mkubwa baada ya kugunduliwa.
Katika meli autopilot husaidia kazi ya kuingoza meli katika njia na uelekeo ambao muongozaji amepanga.
Mfumo huu ufanya kazi kati ya steering na rudder(kata kona ya meli) ambapo meli za kisasa inakuwa imeunganishwa na GPS na ramani ya kielectronic ambapo meli itafata njia elekezi.
Hii autopilot unashauriwa kutumia sehemu ambazo havina meli nyingi,makutano au hali mbaya ya hewa.
Licha ya kuweza kutumia autopilot watu waliopo zamu hawaruhusiwi kutoka sehemu ya kuongozea meli, lazima wawepo ili kama kuna emergency watoe mfumo wa autopilot na kurudi kawaida.
Hii unashauriwa utumie sehemu ya wazi baharini au ziwani,sio kwenye mpango au eneo la bandari.
Autopilot licha ya kusaidia sana, ajali nyingi zimetokea baada ya watu kujisahau na kuacha mfumo huu maeneo yenye hali mbaya ya hewa. Mfano ajali nyingi zinazotokea baharini ya kusini kwa China na ajali kubwa ya meli ya mafuta mwaka 1967 ya Torrey Canyon ambapo baada ya uchunguzi ripoti ilionyesha meli haikutolewa kwenye autopilot ilivyokaribia kwenye mlango wa baharini.