Hapo bado lugha za kigeni mfano kiingereza.
You also speak foreign language other than the fore mentioned?
Yes, French and Arabic, intermediate. Arabic ni ile ya Falestine au Palestina. Kuna tofauti kidogo kwa lugha hizi
Ni kama vile English ya Louisiana na ya Pennsylvania au English ya England vs Ireland
Kuna lugha ukifahamu moja automatic utafahamu ya pili. Kwa mfano, Kijita ni Kabila Kubwa kule Musoma eneo la Majita. Ukifahamu Kijita bila shaka utafahamu Kiluri au kikwaya, tofauti ni ndogo sana, ni 'clan' wanaziita tribe
Kule Tanga ukifahamu Kipare automatic Kisambaa kwasababu kuna mahusiano ya maneno sana.
Kisambaa ni kama '' ''Kriol ' ya Kipare. Unafahamu Jamica English ilivyo! Wagwan ! me can't bend etc
Tatizo la lugha ni kubwa kwa Kabila lako Mushi! Chagga si Kabila ni shirikisho la makabila. Hapo juu nimekuwekea (Rombo) kwasababu Kimachame, Uru n.k. ni tofauti Kabisa. Siyo kama ilivyo Kijita, Kiluri au Kikwaya
Suprisingly Kirombo kinafanana sana na lugha ya Kigweno. Yaani Warombo wapo karibu sana na Wagweno kuliko Wamachame, Wakirua n.k. Kuna mtu aliniambia Wagweno ni Warombo waliokimbilia Milimani.
Again, Wagweno ni 'sub tribe ya Wapare' yaani wapo Pare dominated region. Wagweno can speak broken Kipare But not vice versa.
Ninyi Wachaga mkifanya conference lazima mtumie kiswahili au kiingereza kwasababu hakuna lugha ya pamoja.