Fahamu madhara unayoweza kupata kwa kuweka mtandaoni picha ya tiketi yako ya ndege?

Fahamu madhara unayoweza kupata kwa kuweka mtandaoni picha ya tiketi yako ya ndege?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Kumbuka kila unapo post Ticket yako ya Ndege unahatarisha usalama wako kama ifuatavyo

a. Kwa kutumia Msimbo Pau (Barcode) ya tiketi, Wadukuzi wanaweza kupata taarifa zako na kuzitumia kukufanyia Ulaghai (Phishing).

b. Ni rahisi mtu kubadilisha au kuahirisha safari yako kwani anahitaji jina na PNR (Namba ya Kumbukumbu ya Abiria)

c. Taarifa zako ni muhimu kwa wizi wa Utambulisho, zinaweza kuwezesha udanganyifu kama kufungua 'Credit Card' au kufanya manunuzi bila idhini.

d. Tukio hilo pia linaweza kuwa kichocheo cha Wezi kuvamia nyumbani kwako kwani umeweka taarifa kuwa haupo
 
Slay queen na masharo wanataka kila mtu ajue kuwa wameenda China na Dubai. Hapa ni kama kupigia mbuzi kitaa.

Tena ilivyo mipumbavu unakuta jitu linapost ticket wiki nzima kabla ya safari.
 
Hii haiwahusu Matajiri wa JF wanaotumia private jet

1000011204.jpg
 
Back
Top Bottom